Nakiri kwamba naendelea kujifunza siasa za Tanzania

Kambona alitaka tuwe kama Kenya. Hivi unadhani wakenya wote wanafurahia maisha ya kuwa wakenya??? Thubutu!!! Ukichunguza sana utagundua Nyerere alisaidia Sana kupunguza utofauti mkubwa wa kipato ambao uleta dhuruma kwa wasio na mali na wenye mali kuzidi kujilimbikizia mali!
 
Tatizo la nchi hii ni kuwa tumechelewa kwenye Elimu na Umasikini. Bila kupata suluhisho la hivyo demokrasia,katiba mpya nk ni bure. Hivi vitu ni muhimu katika kuleta mabadiliko ya kiuchumi na kijamii vinginevyo itabaki kuwa mtaji wa watawala. Ukitaka kumtawala mtu mnyime elimu na hapo mbakizie umasikini. Uchambuzi huo ungejikita kwenye hayo mambo mawili yaani ujinga na umasikini ni shida kubwa.Lowasa alikuwa sahihi.
 
Watanzania wote wanafurahia maisha ya kuwa Watanzania??
 

Bila machafuko ama mapinduzi ya kijeshi, tutaendelea na mifumo hii hii mibovu.
 
Kila kunavyo kucha watanzania tunajua ukweli na chanzo cha umasikini nchini.

Ikiwa Mw Nyerere alikuwa na mtazamo wake kwa nia njema bahati mbaya mtazamo huohuo ndio umeleteleza shida nyingi nchini .

Ipo sababu watanzania kuleta mabadiliko ya kweli ya kimufumo na utawala ,tukianza na upatikanaji wa katiba mpya , mifumo ya chaguzi zetu.

Ni hatari sana kiongozi wa nchi,jimbo,kata,au mtaa kupatikana kwa mifukoni mwa watu au mtu mmoja kwa faida yake.

Viongozi hao hawawezi kuwa na masilahi na nchi ,badala yake watataka kurudisha faida kwa walio wapa nafasi na kuwasahau wananchi .


WATANZANIA TUSIJIVUNIE VYWAMA VYETU ,BALI TUWAPIME WANAO TAKA KUTUONGOZA NA TUJIRIDHISHE KUWA WANATUFAA
 
CCM ni laana
 
Elimu inasingiziwa Sana

Tatizo kubwa la nchi hii ni NJAAAAAAA.

Watu wanaumizwa hata kusussa wanashindwa. Wakioewa vibia vya buku buku au elfu 20 wanagawa mpaka mikundu sembuse kura?
 
Mwandishi ametaja makabila matatu hayo ,kwa kurejerea matamshi ya Nyerere kwani yeye ndiye aliye weka [emoji359] kwa maneno na vitendo .
 
Nchi zilizofata siasa za ubepari ndio zimeendelea kama kenya, uganda, congo, zimbabwwe wapo kama Dubai matatizo kama maji umeme elimu njaa magonjwa waliyafuta sababu ya ubepari... Nyerere ndio katufikisha hapa...sawa great thinkers endeleeni na mjadala
 
Taifa ambalo limeshindwa kuweka strong foundation,basi haliwezi kuwa na taasisi imara bali uimara wake hutegemea maoni ya mtu binafsi kama msingi wa kila jambo.

Mwl.Nyerere alikuwa na tabia na hulka ya kuingia na matokeo yake kabla ya jambo kutoa,na jambo hili ndo wangine wamefuata mfumo huo huo.

Hii mada inahitaji utulivu wa akili mkubwa.
 
Mkuu Malcom kiaje?

Umeweka bandiko murua sana na umetumia haki yako ya kuelimika kuchambua hilo.

Hata mie juzi niliweka mada kuhusu "Kleptocracy" ambayo ni zao la hiyo mitandao mizito uloitaja.

Hayati Mwalimu alilia sana khasa aliposikia Mkapa RIP auza NBC ambayo ni marehemu Nsekela ndie alieiimarisha kuwa benki kubwa ya biashara nchini, lakini ile ilikuwa ni twasema " architect of his own downfall".

Lakini marehemu Mkapa nae alikuwa ashatekwa na moja ya mitandao hiyo na ndo hao (wanamitandao) walipojawa na hofu tukaanza kuwapoteza watu muhimu katika nchi hii kama mzee Kombe.

Twahitaji kuuma risasi au raisi wa 2025-2030 ahitaji kuuma risasi awezeshe kuwepo na kura ya maoni itayoridhia mabadiliko ya katiba.

Pili, aseme liwalo na liwe arudi kwenye mipango ya JPM kuhusu nchi hii na abomoe mitandao yote kwa kutumia (samahani kwa kusema hili) "Putin Style" au "Xi Jingping Style".

Hii mitindo waweza kuichanganya au kutumia mmojawapo kulingana na mahitaji yako.

Nasema iwe Putin Style kwa maana kwamba vyombo vyetu vya usalama bado sana na ni lazima vipewe nafasi virudi katika ile "level" inotakiwa ambayo itazuia mtu kama CDF kutoa kauli tata mikutanoni.

"Going forward" hio ndo njia sahihi kwani Putin aongoza zaidi ya raia milioni 147 na Jingping raia zaidi ya bilioni 1, seuse sisi Tanzania wenye raia milioni 60?
 
Sithani kama ujamaa pekee ndoyakulaumiwa nchi kutosonga mbele. Swali ni je? baada ya sisi kuingia kwenye ubepari mpaka sasa tumekuwa matajiri?
 

Umeanalyse vizuri sana, hakika Mimi namkubali sana Nyerere 95% ila moja kati ya foundation mbaya alojenga ni hii ya ukabila ijapokua alikua sahihi in other side.
Mimi ni mchaga halisi Toka Babu pande zote mbili huko zamaaani, ila wazo la Nyerere kutaka kabila kubwa lisishike nchi, hasa kipindi kile bado nchi ni changa, na tunaimarisha umoja kama taifa ni sahihi. Imagine mpaka leo at least makabila hayo makubwa ndio zaidi yamedominate kwenye fursa kubwa nchini.... Ilihali hata hawakuwahi kuongoza nchi. Sasa Je ingetokea wameongoza nchi ingekuaje na mifumo yetu ilivokuwa mibovu? Nidhahiri tungekuwa kama Kenya saizi na chuki isingeweza kuzimwa Kwa urahisi tungekuwa tunatifuana saizi. Mfano mzuri ni usukuma ulivotaka kuanza kutuvuruga nakuona nchi nimali yakundi...juzi tu hapa. Kama taifa tujitadhmini tulipo nakutafuta suluhu nzuri hasa kujenga taasisi imara, ambapo mtu yeyote pande yeyote aongoze nchi Kwa kigezo Cha kuwa anastahili nafasi hio na SI udini, ukabila au ubara/Zanzibar.
 
Hakuna shida kwa mtu kutamani kuwa raisi wa nchi bila kujali atokea kabila lipi.

Tatizo ni pale huyo raisi mtarajiwa atakidhi vipi matarajio ya wapiga kura na si yake yeye binafsi.

Sasa kama alivyosema mleta mada haya makundi mazito ya mitandao ambayo tayari yapo ndio yamekuwa tatizo kubwa linomkabili raisi yoyote yule.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…