Nakiri kwamba naendelea kujifunza siasa za Tanzania


Kwakweli makundi mazito ya mtandaoni ni kutumia tu mabavu, maana mengine yana "hidden agenda" na Kwa wananchi tulio wengi hatuwezi chambua mambo, wanasema disclose analysis kuona je! Mtoa mada anania gani au anataka kutuaminisha nini?
 
Mafuriko lazima yawabebee hadii waseme🤓
 
Tatizo ccm imeshajikulia ni wafalme.sijui kwa nini sehemu zilopita sera ya komunist zimekuwa nchi hatari sana.watu wanashabikia urusi lakini sio mtu mzuri alivotengeneza nchi nyingi kuwa mambo mabaya.
Ccm inajiona putini
 
Tanzania is a potentially failed state. Sijui hata tulifikaje hapa kirahisi hivi.​
 
.. Roho la kubagua na linatutafuna... Hailelezeki eti Leo hii mama ni Rais ?
Na siku hizi tuna Indian, school, sijui Yemeni nk.
Ngoja na makabili mengine waanzishe Shule zao
 
Inatia kinyaa kutenga muda wako kuizungumzia Tanzania
 
Na siku hizi tuna Indian, school, sijui Yemeni nk.
Ngoja na makabili mengine waanzishe Shule zao
Mbona kuna Catholic Schools and Universities hapa Tanzania lakini hatusikii mkilalamika hivi. Katiba yetu ya Tanzania haikatazi kabisa watu kuanzisha shule za jumuiya, inachokataza ni kuanzisha shule hizo kwa nia ovu ya kufanya ubaguzi wa rangi, dini, jinsia au kabila. Jambo ambalo mimi hujanionesha mpaka sasa, ni kwamba hizo India na Yemen Schools zimekataza Admission za watoto wa jamii nyingine, wabantu au waarabu.

Pale Masaki, Msasani kuna shule inaitwa French-School International, ambayo ilianzishwa mwaka 1967 kipindi Mzee Nyerere yupo na ipo mpaka leo. Wanasoma watoto wa jamii zote ambazo zipo hapa nchini. AU shule kama HOPAC, ni ya kilokole na watoto wanatakiwa kuingia shule wakina na King James Bible, lakini mle ndani utakuta hadi waislamu, wahindu, wabudha na wapagani wanasoma. Hapa tatizo lenu ninyi haswa ni lipi ?

Labda kama wewe hujui, lakini wazazi wa kichagga walishawahi kuanzisha shule yao, English Medium kule Ifakara Morogoro miaka ya nyuma kidogo. Ile shule ilikuwa imejaa watoto wa kichagga, lakini wengi wa wanafunzi wa pale walikuwa siyo wachagga. Eneo lile lilikuwa halina English Medium, hivyo kuanzishwa kwa ile shule kuliinufaisha jamii nzima kwasababu walisoma watoto wote kwa bei nafuu. Hivi kwanini ninyi wapenda UJAMAA huwa hamyazingatii haya ?

Mwaka jana kwenye sakata la bandari nilisikia waislamu wakiwa wanalalamika kwa TEC kwamba, mbona wao walipewa maeneo ya kuanzisha vyuo vikuu na wanalipwa ruzuku za mahospitali kila mwezi, na kutaka MoU baina ya serikali iangaliwe upya. Huwa najiuliza sana kuhusu uelewa wa hawa watu. Hivi vyuo kama St. Augustine, Tumaini Makumira, Bugando huwa vinapokea tu wanafunzi wa Kikatoliki au wanafunzi wote? AU hizo hospitali ambazo wanazilalamikia huwa zinatibu wagonjwa wakristo peke yake?

Hii nchi kuna shida kubwa pahala.....​
 
Ume andika kwa uchungu Sana mkuu hakika nime wai kujiuliza Sana kwanini makabila haya Yana baguliwa Sana

Nilicho kuja kugundua sikuamini ...

Nikwamba wanatengwa kwa uzalendo wao tu na ujuzi wao wa mambo mengi na Kuto kuku bali mambo ya ufisadi,mauwaji,kuoneana, nk no more
 
Kwa hiyo hizo Indians na Yemen school ni Kwa wote au sasa sijui zikija za wachagaa, na Banyakyusa, Bahima, Bahaya nitakuwa za wote au .
Hopac ni hela yako, French school ilikuwa ni Kwa ajili ya watu toka nchi zinazoongea kifaransa au MTU ambaye anataka kujua kifaransa ukitilia maanani ni mojawapo ya lugha za Umoja wa mataifa.
 
Kwani kuna shule kwa ajili ya jamii moja peke yake hii Tanzania ? Binafsi sijaziona, hebu nitajie baadhi.​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…