Nakiri Ole Sabaya kunishinda ujanja na kuweza kunidanganya. Nilimuona mzalendo kweli kweli

Nakiri Ole Sabaya kunishinda ujanja na kuweza kunidanganya. Nilimuona mzalendo kweli kweli

Kidogo kidogo mmeanza kutoa ugali kichwani na kurudisha bongo za binadam.
Marehemu pombe aliwabrainwash sana mataga, mmeona watendaji wake jinsi walivyo na majambazi, hiyo ndiyo tabia aliyokuwa nayo John enzi za uhai wake
 
Wewe ni kijana muungwana. Binadamu anayekiri mapungufu yake hadharani ni mtu anayejiami. Nakupongrza kwa hatua hii.

Ushauri wangu kwako,na watu wengine ambao mliingia kwenye mtego wa viongozi laghai kwa kutekwa na propaganda zao...anza kusaka ukweli(truth) ili ufanye informed judgement.
Swadakta/ewalah
 
Unabahati shukuru ulimbukeni wako maana ungekuwa upinzani ungekuwa tumeshakusahau,na kwa taarifa yako ndio ulembukeni umetoka hivyoo,Karibu mjini kiakili na mwili ,kuanzia sasa tumia busara na hekima kabla ya kuongea au kutenda
 
Siyo kwamba huyu jamaa hakujua uhuni wa Sabaya,alijua toka mwanzo ndiyo maana hadi majuzi wakati kakamatwa alikuwa anamtetea.Ambacho mleta mada hakuwa na uhakika nacho ni je Serikali ya sasa ipo serious na hii ishu au lah.Baada ya kugundua kuwa mambo yamebadirika naye kaamua kubadirika na kuhamia sehemu inayotoa ugali kwa sasa.Hili sio la kushangaà ni kawaida kwa wanaCCM,asiyekwepo na Lake halipo
 
Ulikuwa ni ujinga wako tu,maana mapungufu yote ya Magu na hilo genge lake la kina Makonda, Sabaya, Polepole, Bashiru, Kabudi,Ndugai nk tulikuwa tunayaweka wazi hapa jukwaani, tena mengi yenye ushahidi wa wazi. Kama ulishindwa kutambua udhalimu ule, hata akitokea kiongozi mwingine mchafu zaidi ya Magu na kukuambia na mzalendo utaamini, kwani una uwezo mdogo wa kutambua mambo.
 
"Vetting" kwa viongozi pale wateuliwapo ni mchakato muhimu sana, na unapaswa kufanyika kabla kiongozi mteule kuapishwa na kukabidhiwa ofisi za umma. Mamlaka za uteuzi huweza kufanya makosa na kumteua mtu kwa sababu za kimaslahi wanazozijua wao wenyewe nje ya vigezo stahili vya ushindani, weledi, stadi, ujuzi, elimu na uzoefu wa muhusika.

Mchakato huu unapaswa kuwekwa kiaheria, ili jopo la majaji liundwe na kuweza kujiridhisha juu ya sifa za kimaadili na kiuadilifu za kiongozi mteule. Kwa kufanya hivyo tutaepuka kupata viongozi ndezi kama huyu Lengai ole Sabaya.

Kwa masikitiko makubwa na kwa mara nyingine tena tunazidi kushuhudia na kutilia mashaka umakini katika teuzi dhaifu za mwendake hasa kwa viongozi vijana. Aliwadekeza mno wengine wakifanya matendo ya kifedhuli mbele ya macho yake huku yeye akifurahia.

Kwake wale waliowachapa watu viboko sawa! Waliowa waweka watu kolokoloni Kwa masaa 48 sawa! Kundi la watu wasiojulikana sawa! Waliotoa lugha za matusi na sizizokuwa za staha sawa! Kuharibu mali za watu sawa! Na mengine mengi yenye kufanana na haya.

Mwendazake! Mwendazake! Mwendazake! Kweli ulijaribu, kuthubutu ama hata kutamani kubadilisha katiba ya nchi na kuondoa ukomo wa uongozi!? Acha tu zibaki kuwa ni tetesi.

Mfumo wenyewe wa kufanya vetting unachaguliwa na hao hao viongozi waovu. Hivi ungeweza kuamini kuwa usalama wa taifa ndio wangesimamia uchafu wa hali ya juu wakati wa uchaguzi? Sasa kama usalama wa taifa wanakuwa sehemu ya uchafu kwenye nchi, hapo unategemea kuwa na viongozi waadilifu?
 
Wazalendo wengi mliojitokeza kipindi cha Magufuli ilikuwa ngumu kuwatofautisha na wajinga.
 
Nliuchukia 2015 kwa sababu ya wanasiasa..
 
Wewe mpaka mtu anashutumiwa kukata mtu masikio wewe unakaza fuvu kusema ni mzalendo ?🤣🤸🐒👇
IMG_20210605_141625.jpg

NB: Huyu alifumaniwa na mke wa mtu akakatwa masikio hiyo iaeleweka, ila kukata masikio ukiwa unatimiza majukumu ya jamuhuri hiyo haivumiliki
 
Akili zimekurudia

Awamu ya 5 ilikuwa inaongozwa na majambazi watupu
 
Nilipokuwa naandika "Magufuli is a country bumpkin" nilikuwa namaanisha mengi sana.

Hapa lazima tujiulize.

Je, haya madudu yalivyokuwa yanaendelea, Magufuli hakujua?

Kama hakujua basi alikuwa ni mzembe wa hali ya juu kutojua maasi ya mteule wake wa karibu kabisa.

Ama alijua akapotezea tu?

Kama alijua akapotezea tu, basi alibariki uovu huu.
 
Ogopa sana wanaotanguliza uzalendo na Mungu mbele...Ogopa sana watu wa Camera maACTION na mapicha picha ya kuonyesha "UZARENDO"......Bashite kutwa alikuwa mbele ya camera mara kujenga hospital ,mara kutetea wajane mara kutibu TEZI dume kumbe alikuwa anawahadaa wanyonge.
Dini na so called ucha Mungu ulitumika sana kama kigezo cha kuficha maovu na kupata kiki kisiasa.
 
Back
Top Bottom