Mkuu
Kiranga USHAHIDI ni namna ambayo inatumika kuthibitisha au kukanusha ukweli wa jambo ambalo linachunguzwa, Kif.cha 3(1) Sheria ya Ushahidi Na. 6 1967.
Sasa Kila anayedai jambo fulani kwa Mtu Fulani ana dhima ya kuthibitisha kwa ushahidi uliopo. Katika jitihada ya kuthibitisha au kukanusha jambo kuna hatari nyingi ambazo huweza kupotosha kweli na haki. Ili kuepuka au kupunguza tu hatari kama hizo kuna kanuni ambazo zinatakiwa zifuatwe kabla ya kuukubali au kuukataa ushahidi fulani.
Ushahidi unaokubalika ni ule tu unaothibitisha au kukanusha jambo linalodaiwa kwa mujibu wa sheria, kif. Cha 7 (I)(h)(j) Sheria ya Ushahidi.
Mtu ana fahamu tano kuu; kuona, kusikia, kugusa, kuonja na kunusa. Aina zote hizo huweza hutumika katika kuthibisha au kukanusha kweli ya jambo linalobishaniwa kif. Cha.3(1) na 62(I)(h)(j) cha Sheria ya Ushaihdi, i.h.j).
Nakupa mfano:
Kiranga ameshitakiwa kwa kuchoma nyumba kwa kukusudia.
Josh J anaweza kuwa alimwona
Kiranga akichoma nyumba hiyo. Au anaweza kuwa alisikia harufu ya mafuta ya taa kabla ya kulipuka moto uliounguza nyumba hiyo; au anaweza kuwa alimsikia
Kiranga akipanga kuichoma nyumba hiyo. Aina zote hizo za fahamu zina uzito katika kuthibitisha kosa hilo la uchomaji nyumba.
Hali ya akili ambayo shahidi anaielewa pia huweza kuwa ushahidi. Kwa kawaida shahidi anaweza kuthibitisha au kukanusha ukweli mintaarafu ya hali ya akili yake mwenyewe lakini sio ya mtu mwingine.
Hali ya akili ya mtu inaweza kuthibitishwa kufuatana na mwenendo au kauli yake binafsi. Hivyo basi shahidi anaweza kudai hana akili timamu kwa kauli yake mwenyewe. Lakini hawezi kusema kwa uhakika kuwa mtu fulani hana akili timamu isipokuwa kama anatoa maoni ya kitaalam, mathalan daktari, au anafahamu mwenendo wa mtu huyo ambao unathibitisha utovu wa akili timamu.
Kama sijaeleweka Utanisamehe Mkuu Wangu