Unamsoma vibaya rais wako mkuu 'Stroke'.
Yupo "serious" kweli kweli na kuibadili CCM wakati huu kutoka CCM ya maigizo ya chama kilichowahi kuwa chama cha ukombozi; chama cha wafanyakazi na wakulima na kukifanya kuwa chama cha mafisadi, mabwenyeye na kila takataka unayoweza kuifikiria mwenyewe.
Hadi hapo atakapokuwa ameimaliza kazi hii, hutaitambua tena CCM kwamba iliwahi kuwa chama chenye kusimamia maslahi na haki za waTanzania
Katika viongozi wote waliowahi kuiongoza CCM, ukimwondoa Mwalimu Nyerere, hakuna mwingine aliyewahi kukibadili chama hiki kiasi atakachokifikia Samia.