Nakosa amani na ngozi yangu

Nakosa amani na ngozi yangu

Miss Cullen

Member
Joined
Jul 27, 2017
Posts
5
Reaction score
3
Ndugu wa humu ndani na watu wa jamvi hili,

Mimi ni msichana ambae ni mweupe wa asili tangu kuzaliwa lakini kitu ambacho kinanikera ni kwamba nina weusi mkubwa katikati ya mapaja pamoja na mabaka, sijui ulianza vipi sikumbuki maana mimi ni mwembamba sivaagi nguo za kubana wala skin tight yaani kifupi sifanyi chochote cha kufanya huo weusi uwepo ila nilianza kuuona baada ya kujitambua nikiwa bado mdogo mdogo(nahisi nilizaliwa hivyo)

Nimetumia vitu vingi lakini hakuna hata kimoja kilichonisaidia mpaka sasa nishachoka jamani, hii hali inanifanya nikose kujiamini na kufikiria mara mbili mbili linapokuja suala la kuwa na mpenzi maana naona ni kitu cha aibu na aibu mtu akikuta nipo tofauti na muonekano wangu wa nje, hivi wakaka huwa mnafikiria nini mnapokuta msichana ana rangi za ajabu katika mwili wake kama weusi mapajani au mabaka tofauti na ulivyotegemea?

Sina amani na raha kiukweli natamani sijui nipate dawa gani ya kuondoa hio tofauti katika mwili wangu.
 
Hauna ulemavu wowote. Jiamini tu, ukienda kwenye mchezo wa kule kiwanja cha 6 x 6 wewe dondosha magwanda yako chini bila hofu ubaki na nguo za kuzaliwa nazo kisha mpe mechi ya ushindani huyo jamaa yako kiasi mechi ikiisha analala fofo kwa uchovu kutwa nzima. Hiyo ni kama ukiwa na upara, kovu, ulemavu wa mkono ukaanza kuficha ficha unakosa kujiamini na kuilaani siku uliyozaliwa, lakini ukiacha watu waone na kujua unakuwa hauna aibu na unaishi kwa furaha na amani. Kwa taarifa yako wanawake wengi sana wakivua magwanda wengi ni weusi sana makalio, mapajani na kuzuka mitaa ya kati. Wanaume wengi wanafuata ile kitu ya kati rangi ya huko haina tija mradi kwa nje unalipa na kitakalio kipo, pia kama haujajichubua.
 
Duuh pole sana bibie..jikubali tu...wanaume wengine tunawakubali jinsi mlivyo..usijichoke
 
Huu uzi ungekaa jukwaa la Dr ungepata msaada haraka kwa wataalamu kama akina Watu8
Hii sio issue ya kwenda kwa Dokta. Makemikali ya kujichubua ya nini? Hiyo kitu ni ya kuzaliwa nayo. Ajiamini tu, kwani kashakimbiwa na mtu kisa hiyo rangi nyeusi ya huko mitaa ya kati kwake?
 
mwone mtaalam wa magonjwa ya ngozi akifanyie vipimo labda kuna underlying problems,otherwise enjoy the life and be proud the way ur,atakayekupenda atapenda upendo wako sio ngozi yako,kumbuka tunaishi once furahia maisha .
 
Pole sana jf kuna madactari fake sasa kama huyo alokushauri shahawa kasomea chuo gani?

Kuwa na subira wenye ujuzi wako lunch watakuja.

Nbkama huo weusi ulikuwepo tangu utoton sidhani kama vitatoka dia? Kama weusi huo ni kama vile vi alama vinavyotokea shingon au mgongoni kuwa na amani ukimpata akupendae atakupenda na rangi hiyo
 
Usiwaze lady.. mwanamume atakayekususa kwa ajili ya hyo issue basi itakuwa hakukupnda toka moyoni... But picha tafadhari ili nitathmini 🙂🙂🙂
 
Pole sana jf kuna madactari fake sasa kama huyo alokushauri shahawa kasomea chuo gani?

Kuwa na subira wenye ujuzi wako lunch watakuja.

Nbkama huo weusi ulikuwepo tangu utoton sidhani kama vitatoka dia? Kama weusi huo ni kama vile vi alama vinavyotokea shingon au mgongoni kuwa na amani ukimpata akupendae atakupenda na rangi hiyo
Ahsante kwa ushauri wako
 
Kwani kuna mapele kama ukurutu mpaka uogope?embu jiamin mabaka sio tatzo kabsa.
 
kuna mwanasaikolojia mmoja aliwahi kusema mwanaume akiingia 6 kwa 6 anakuwa na hofu ya kushindwa kumridhisha demu na mwanamke anahofia kutokana na umbile lake
 
mwone mtaalam wa magonjwa ya ngozi akifanyie vipimo labda kuna underlying problems,otherwise enjoy the life and be proud the way ur,atakayekupenda atapenda upendo wako sio ngozi yako,kumbuka tunaishi once furahia maisha .
Niliwahi kwenda kwa daktari wa ngozi na kuniambia Melanin imezidi
 
Mtu akikupenda hilo baka ataona kama tattoo tu...usiumize kichwa kwa mambo madogo namna hiyo,achia body tu
 
Back
Top Bottom