Nakubali Yanga ni ya kwanza kucheza Nusu Fainali Confederation, nakataa Yanga sio Bingwa mara 29

Cashman

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2018
Posts
3,017
Reaction score
5,294
Kweli ninakubaliana na hoja za Wanayanga kuwa wameweka Rekodi ya kufika Nusu Fainali na sasa wanaikaribia Fainali ya Mashindano CAF Confederation.

Nikiwa natumia ubongo huo huo kukubali hayo, nikiwa na akili timamu, na kwa mantiki ile ile, nakataa Yanga sio Bingwa mara 29 kwa sababu Ligi Kuu (Premier League) haina misimu 29 tangu ianze. Zamani hatukuwa na Premier League tulikuwa na Ligi Daraja la kwanza.

Mambo mengine yote yaliyobaki ni propaganda. Tuishi humo.
 
Makolo mnapata tabu sana. Yan mtu anaamka sa 9 usiku anaacha usingizi wake, sijui km ana mke maana kwa akili hizi atakua kakuonea huruma tu. Haya anakuja kuandika huu utumbo yan kaacha yote hayo.

Haya basi tuambie wewe Yanga ni bingwa mara ngapi na Makolo pia ni mara ngapi?
 
Basi tukubaliane kitu nyinyi kama kweli mlifika fainali huko 74 kweusi lile kombe halikuwa linaitwa klabu bingwa so tukubaliane hamkuwahi kufika fainali ya klabu bingwa ubishi uishe
 
Inawezekana ukianza kuhesabu toka mfumo wa sasa ulipoanza kufanya kazi ukakuta Simba amekuwa bingwa mara nyingi kuliko Yanga. Embu fuatilia uje uwaumbue....
 
utopolo mnakurupuka sana...
jamaa kawajoke kiaina ila nyie mmejaa kwenye kumi na nane zake bila kujielewa...
hapo anataka kufikisha massage kwamba kama Simba alifika fainali ya Kombe la caf mwaka 1993 lakini utopolo mnapinga et halikuwa na hadhi kwa sababu mfumo na utaratibu umebadilika... na mnaenda mbali zaidi kwa kusema hilo kombe la caf aliloshiriki Simba ni la zamani sana halikuwa na hadhi ukilinganisha na hili shirikisho..
sasa anataka kupima uelewa wenu kuhusu hili kombe lenu la NBC la 29 kwamba kwa nini mhesabie na makombe ya zamani ambayo Yanga mlichukua kipindi hicho ligi inaitwa daraja la kwanza na sio PL?
 
Kombe hili, walisha liita ni la WALIOSHINDWA! Mwaka huu, wanalitambulisha kama ni BORA KULIKO KLABU BINGWA! Ukitaka kuujua upunguani wao, Rais wao kafanya mahojiano na chombo kimoja cha habari huko SA, tunapewa taarifa kuwa "KAHUTUBIA TAIFA"!!


Sent from my TECNO CF7 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…