Labda wewe na huyo mleta uzi ndio mnashindwa kuelewa.
Fainali aliyocheza Simba mwaka 1993, ilikuwa ni Caf cup na wala haikuwa fainali ya kombe la shirikisho. Kwa kipindi hiko kombe la shirikisho lilikuwa linaitwa Africa cup winner's cup.
Kwa uthibitisho zaidi, ni kwamba mwaka 1993 hiyo ilifanyika fainali mashindano matatu, Zamalek akabeba kombe la Africa cup of champions club mwaka huo huo 1993, huku Al Ahly nae mwaka 1993 akabeba kombe la Africa cup winner's cup. Na Stella ambao wakacheza fainali na Simba mwaka huo huo 1993 ndio wakabeba kombe la CAF cup.
Katika mechi ya ufunguzi wa pazia jipya la msimu wa mwaka 1994, mechi ya caf super cup ilipigwa kati ya Zamalek (bingwa wa klabu bingwa) VS Al Ahly (bingwa wa shirikisho) na Zamalek akabeba kombe la super cup. Kama hiyo fainali aliyocheza Simba mwaka 1993 ingekuwa na hadhi sawa sawa na shirikisho basi ungeona bingwa wa hilo kombe akicheza CAF super cup.
Kuhusu makombe ya Yanga kufika idadi ya 29, ni kwamba wamehesabia makombe yote waliyopata kwa mashindano ya ligi kuu ya Tanzania bara. Ligi iliipitia katika mifumo mbali mbali ya mabadiliko lakini ilikuwa ni ligi hiyo hiyo ya Tanzania bara hivyo Yanga wakahesabia makombe ya ligi kuu Tanzania bara. Pia ikumbukwe kuwa kuna wakati ligi ilikuwa inahusisha timu kutoka Zanzibar (kombe la muungano)
Pamoja na kuwepo kwa kombe la muungano, ligi ya Tanzania bara ilikuwepo, na ligi ya Zanzibar pia ilikuwepo kisha zile top 3 kwa kila ligi walikuwa walishirikii kombe la muungano. Hivyo kuna kipindi Yanga alikuwa bingwa wa ligi kuu ya Tanzania bara lakini hakuwa bingwa wa kombe la muungano lakini kwenye orodha ya makombe yao wamehusisha ni ligi kuu bara pekee.