cutelove
JF-Expert Member
- Oct 3, 2017
- 3,448
- 7,972
Wakati vita ikishika kasi kule Ukraine dhidi ya Putin ,nashangaa baadhi ya watu kwenye majukwaa ya mitandao ya kijamii wakimuunga mkono kuivamia Ukraine na inasikitisha sana badala ya kukemea
Wengi hutetea uvamizi wa USA na NATO kwenye mataifa mbalimbali duniani ikiwemo Libya ,Iraq nk
Ukweli ni kuwa uvamizi unaokuwa unafanywa na NATO na USA huwa ni wa halali kabisa,ukiangalia nchi zilizowahi kuvamiwa kote kuna migogoro ya kisiasa na kijamii ndani ya nchi hizo ,na mbaya zaidi kuna makundi kwenye nchi hizo huwa yanapata mateso ya kibinadamu yamekithiri na kupindukia haki za binadamu na kuhatarisha usalama wa kikanda na kidunia kwa ujumla
Na kama unasema huwa wanawaonea, kwa nini USA na NATO wakisha vamia wanakaribishwa na wananchi kwa vigelegele na nderemo na magari ya kijeshi yanatandikiwa nguo yapite juu kwa heshima?
Wapi USA na NATO wamewahi kuvamia wananchi wakashirikiana na jeshi la nchi yao kuwapiga au kuweka upinzani wa uvamizi?
Twende Ukraine, Moscow anamvamia Ukraine ,nchi inakuwa moja na kwa hamasa ambayo inatia machozi ya huruma na furaha na maajabu ambayo hujawahi kuyaona kwenye uvamizi wa USA na NATO
Hakuna mwananchi hata mmoja wa Ukraine ambaye amesema hatumtaki Rais wao ,hakuna hakuna ,hakuna na hakuna tena
Nchi ya Ukraine imekuwa moja tuache yale majimbo yanayotaka kujitenga lakini miji mikubwa ya Ukraine imeshindikana kutekwa,si watoto,wamama na wazee wanawapa wanajeshi wao moyo wa kupigania nchi yao ?
Cha msingi ni kwamba Putin hajui na hana sababu ya kuivamia Ukraine, na siku zake hapa duniani zinahesabika angalia sasa dunia inavyomtenga kwa kila nyanja ,ushujaa wake unaanza kufifia kama mshumaa
Putin ni mtu katili duniani hapaswi kuigwa na mtu yeyote,yaani imefikia muda sasa unapangiwa namna ya kuishi na nyie ni Taifa huru,Kuna siku Kenya itajiunga na NATO halafu Tanzania tuivamie Kenya kwamba kwa nini anajiunga na NATO, huu ndo upumbavu wa standard gauge