Nakubaliana na Marekani na NATO kuvamia nchi mbalimbali duniani

cutelove upo sahihi kwa kiasi fulani, lakini sio 100% ila hawa wanaokujiu hawajibu hoja wanaishia kukutukana na kukuuliza maswali badala ya kukosoa hoja yako moja kwa moja

Ni kweli kuwa vamizi za Marekani za hivi karibuni, mfano Libya, Ghaddaffi alikuwa kwanza na bifu ya muda mrefu na mataifa ya magahribi, alikuwa akifadhili magaidi waliolipua viwanja vya ndege pamoja na majengi ya ubalozi njchi za Ulaya na aliwahi kukoswa koswa kuuawa na hao NATO kwa mabomu miaka ya nyuma kabla ya maandamano ya kumtoa, hapo ndipo alipojirudi na kuanza kuwa karibu na nchi za Ulaya, lakini wananchi wengi walipokuwa wanaanandaamana kumtoa alikuwa akiwapiga mabomu na kuapa hatatoka madarakani, hili sio propaganda sababu hata media za kiarabu na kichina zote zilikuwa zikiripoti watu kuuawa kwa mabomu

Taliban na Afghanistan hawa waliichokoza marekani wenyewe kwa kipindi kirefu kwa madai ya kiongozi wao Osama bin Laden kuwa Marekani na Ulaya ni kitovu cha uovu ambao ni kinyume na dini ya Kiislam, huyu ilikuwa ni haki yake pia

Syria, Syria nae ilikuwa ni case kama ya Libya tu, maandamano kisha wananchi wakaanza kuuawa, jeshi likagawanyika, wakataka kumpindua Assad, Russia akaingilia kati kumsaidia Assad kuuawa wananchi, ndipo Marekani nae akaingilia

Saddam Hussein huyu ndio kidogo inaweza kuwa walimuonea kwa sababu walisema alikuwa na silaha za maangamizi lakini hawakumkuta nazo, lakini Saddam pia alikuwa na madhambi mengi na bifu klubwa na nchi za Magahrib, ikiwamo kufanya mauaji ya kimbari dhidi ya Wakurdi na kuivamia Quwait na kusababisha vita ya Ghuba

ila sio kweli kwamba Marekani anakuwa motivated na sababu nzuri, Marekani nae ana maslahi yake binafsi na kuna nchi nyingi za kidikteta anaziunga mkono akiona zinalinda maslahi yake na amekuwa akiangusha hata Serikali za kidemokrasia kabisa, sema ngoja nikomee hapa
 
Mkuu ungeendelea na mifano ya nchi za kidemokrasia ili tuongeze maarifa,maana ni hivi karibuni tumekuwa tunaona ufaransa inajitahidi kuondoa uasi na makundi ya kigaidi kule West Africa lakini naye akawa ameanza kushindwa kumbe coup d'etat za kula west zinasaponsa na mkono wa Urus

Kwa hiyo ni asilimia mia moja kuwa Putin angependa robo Tatu ya Dunia iwe under dictatorship ya kijeshi kuliko serikali za kiraia
 
Communism all property are owned by the community ,Oxford dict

Tunarudi mule mule mali za jamii.
Mkuu wewe una "kipaji"....

Khaaa 😳😳

Yaani bado unang'ang'ana kuwa COMMUNALISM ndio COMMUNISM?!!🤣

Hongera mkuu wangu 👍
 
Mwanamke na vita wapi na wapi hemu nenda chit chat uko bhana
 
Egypt kulikuwa na Rais wao dikteta Hosni Mubarak, huyu alikuwa rafiki wa Marekani sababu alikuwa hana sera kali dhidi ya Israel, Egypt ni nchi ya jirani na Israel
Yule Dikteta Mubarak akapinduliwa kwa maandamano na akachaguliwa Rais mwingine kutoka chama cha Muslim Brotherhood anaitwa Mohamed Morsi

Hii Muslim Brotherhood ni chama ambacho kina msimamo mkali dhidi ya Israel

Yule Morsi alifanyiwa figisu nyingi na jeshi la Egypt likishirikiana na Marekani na baada ya muda alipinduliwa na kushtakiwa, akafia gerezani

Sasa hivi Egypt kuna Rais mwingine ambaye ni dikteta kuliko hata Mubarak na amebadilisha Katiba kujiongezea muda ila Marekani wanamuunga mkono sababu hana misimamo mikali dhidi ya Israel

Marekani wakati wa vita baridi ameondoa au amefadhili kuondolewa kwa Serikali nyingi tu ambazo zilikuwa na mrengo wa ujamaa na kuweka serikali za kidikteta tu ilimradi zilikuwa zinapinga sera za kijamaa huko latin America na kwingineko

Ni kweli Ulaya na Marekani wana value ubinadamu kwa kiasi kuliko Urusi, lakini kuna saa ni mashetani pia na unafiki mwingi
 
Asant mkuu
 

Kwa hiyo unataka kutuaminisha kwamba kwa sasa wananchi wa Libya wanakula maisha kuliko kipndi kile cha Ghadaff!!???
 
Hujui kitu ww umeandika pumba tu
 
Nikupe hongera na nimezipenda hoja zako.

Warsaw pact na NATO yalichagizwa baada ya heightened tension between the two great powers that emerged from the WWII, US na USSR. Mvutano huu ukaelekea mpaka kwenye arms race. Huu mvutano haukuishia kati yao tu bali ulileta athari na maeneo mengineyo ya dunia.

Baada ya bay of pigs invasion kufeli mwaka 1961 kipindi cha Keneddy, Nikita Khrushchev aliingia mkataba wa siri na Cuba, Fidel Castro kuweka makombora ya nuclear Cuba ambayo yatakayomfanya US afikirie kuivamia Cuba na maslahi mengine ambayo tutayaona mbeleni. Bay of pig invasion ni mpango wa mapinduzi uliyoandaliwa na US chini ya CIA ili kuipindua serikali ya Fidel Castro nchini Cuba.

Hii ilikuwa ni ufungua kwa USSR kuitumia dhidi ya US kwa sababu USSR alikuwa targeted to them from sites in Western Europe pamoja na US. Mwaka 1961 zaidi ya makombora 100 ya nyuklia ya US yaliyokuwa na uwezo wa kuisambaratisha Moscow yaliwekwa Italy na Turkey ambao ni karibu na USSR. Ili USSR ijilinde zaidi ikambidi na yeye Bay of pigs invasion iwe ni ufunguo kwake kwa kumshawishi Cuba kwa kuingia naye mkataba wa Ulinzi. Hivyo naye akaweka makombora ya nyuklia Cuba ambapo ni karibu na US. Marekani hili lilimsumbua sana.

Ili kuiepusha dunia kuingia kwenye vita ya 3 ya dunia US na USSR zilibidi ziingie mikataba ambapo USSR masharti yake kuwa Marekani hatoivamia Cuba na Makombora ya nyuklia ambayo ni tishio kwa USSR yaondolewe nchini Italy na Turkey. Kwa upande wa Marekani sharti lake ni kuwa makombora ya nyuklia yaliyowekwa nchini Cuba ambayo ni tishio kwa usalama wa Marekani yaondolewe. Hivyo, mkataba ukafanyika.

Germany Reunification inahusu muunganiko wa Ujerumani mbili. Hapa kuna mafungamano yalifanyika kati ya Urusi na nchi za west. Baada ya WWII Ujerumani mashariki ilikuwa chini ya uangalizi wa USSR na Ujerumani magharibi ilikuwa ipo chini ya uangalizi wa west.

Ili kuziunganisha ziwe nchi moja kama awali inabidi pande zote mbili zikubaliane yaani upande wa west na Urusi. Lakini kabla ya hili tukio tayari Ujerumani magharibi ilishaingia kwenye NATO. Mbali na hili tayari tulishaona hatua waliyofikia ya kuwekeana karibu mizinga ya nyukilia hali ambayo ilileta taharuki baina ya nchi zote mbili na dunia kwa ujumla.

Kwenye hili Urus ikahitaji ipatiwe usalama wake kwanza kwa sababu ikishakuwa nchi moja inakuwa NATO, na NATO iliundwa dhidi yake. West+(Marekani) wakawaahidi Urusi kuwa ikisaidia kuunganisha hizi pande mbili ahadi yao ni kuwa NATO hawatosogeza urefu hata wa hatua moja kuelekea east (Ulaya ya mashariki). Hivyo 1992 Ujerumani zikaungana. Lakini west waliivunja ahadi yao. Wakatanua zaidi muungano wa NATO na kuelekea zaidi mashariki ambapo ndipo ilipo Urusi.

Amerika hakukubali USSR chini ya Urusi kuweka makombora ya nyuklia na nchi jirani na mipaka yake, Cuba. Iliamua kupambana kwa namna yoyote ili kulinda usalama wa nchi yake. Ilifanya hivyo ili kulinda maslahi ya usalama wa nchi yake.

Urusi hakuanza tu kwa kuivamia Ukraine. Alitafuta kwa namna zote hii hali waimalize kwa diplomasia ila west wakampuuza na kumdharau. Unafikiri usalama wa nchi yake aulinde kwa namna gani? Nafahamu Ukraine ni nchi huru. Lakini uhuru wa kuhatarisha usalama wa nchi jirani yako basi huo uhuru utazamwe tena. Na mfano kama huu ndiyo uliyoigharimu Tz kuingia vita na Uganda. Kwa sababu tuliwaficha maadui wa Uganda ambao serikali ya Uganda iliona ni tishio kwao tena kwa nchi jirani.

Kama alichokifanya Marekani ndicho anachokifanya Urusi. Ikiwa Ukraine itaingia NATO itahatarisha usalama wa nchi ya Urusi kwa sababu Marekani itaweka mizinga yake ya nyuklia. Mbali na hivyo kuna silaha za kibaiolojia. Vipi kama akiunda magonjwa na kuyarushia upande wa Urusi? Muhimu tusijisahaulishe kama hizi nchi bado kuna sintofahamu baina yao. Muhimu inabidi Ukraine akae vyema na jirani yake. Kwa sababu Urusi ni jirani yake na haiwezi kufutika. Njia nzuri na salama ni kutengeneza diplomasia ambayo itakuwa salama kwa nchi zote mbili. Kwa hili nakubaliana na sababu za Urusi na naziona mashiko.

Hata kama NATO ikisema kuwa hizo ni fikra za Mrusi kuwaanadhania tunamzunguka kwa lengo la mbeleni kuwa rahisi kumvamia kijeshi. Lakini kwa nini wasiheshimu fikra zake ikiwa ni kweli NATO wanamalengo ya kuifanya dunia kuwa sehemu salama?

Unakubaliana na sababu za uvamizi wa NATO kwa nchi nyengine, its okay! Naheshimu mawazo yako. Marekani alisema Sadam Hussein ana silaha za maangamizi kwenye baraza la UN. Mwisho wa siku akashindwa kutuonyesha hizo silaha za maangamizi zipo wapi? Waliivamia Libya. Obama akaomba radhi kuwa katika maamuzi aliyoyafanya kuyakosea na kujuta hilo lipo!

Ukiwa na swali niulize ila nitafanikiwa kulijibu baadaye Mungu akipenda. Kwa sasa nimebanwa na majukumu.
 
Uzuri wa NATO wapo wazi ,acha hawa majamaa madikteta yanayoficha kila kitu kwa wananchi
Maana ya dictator ni ku-dictate yaani kulazimisha mambo.

Maadamu kadhia ina mhusu Putin, tumuongelee Putin. Tusaidiane pengine kina kitu nimeshindwa kukiona kwa Putin. Wapi na tangu lini Putin ni dictator?

Kuhusu NATO; hawako wazi. Bali NATO wanataka ukisikie kile wanachotaka wao mkisikie na mkione kile wanachotaka wao mkione.

Ukiwa kama una swali niulize. Ila kwa baadaye Mungu akipenda nitalijibu.
 
Toa mada hajitambui. Na hajuwi Kama Kuna Vita baridi Kati ya Russia na Marekani na NATO. Kwa miaka mingi, na Super Power ni Marekani na Russia.
 
Gentleman Comment, shukran sana Mkuu.
 
Kweli akili ya mwafrika ya mwafrika tu.
Huko alikovamia vipi migogoro iliisha?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…