Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Kuna clip iko kwenye mitandao ikionyesha mahojiano aliyofanyiwa mchungu Msigwa na Darmpya tv, ambapo mchungaji Msigwa anasikika akiongelea swala la critical thinking.
Msigwa anasikika akisema, wakati wa Mwalimu, vijana wa chuo kikuu walikuwa na uhuru wa kusema chochote wawapo maeneo ya chuo na walikuwa na kinga ila kinga hiyo ilikuja ondolewa enzi za Mwinyi baada ya wanafunzi wa chuo kikuu wakati huo kumkosoa mzee Mwinyi.
Kwa maelezo yake, Msigwa anasema Mwalimu aliruhusu mijadala vyuo vikuu na kwamba vyuoni ni sehemu ambapo watu wana-think critically tofauti na sasa ambapo wanafunzi wa vyuo vikuu hawawezi hata kuuuliza maswali ya how,why, n.k.
Msigwa amesema wanafunzi hawa sio wa kulaumiwa kwani hata walimu wao nao hawa-think critically huku akitaja kutishwa kuwa ni moja ya sababu ya walimu wao kuwa hivyo.
Msigwa anahoji kama ma-proffesor wetu wanaka chini na kuumiza vichwa kuhusu hatima ya Tanzania yetu kiuchumi, n.k katika miaka 30 ijayo huku akitoltea mfano wa nchi kama Israel ambayo inauza "brain" duniani na wamarekani wanaowaza nishati mbadala ya mafuta kwa miaka 30 ijayo.
Kwa mfano, Msigwa anahoji tumejiandaa vipi kuacha kuitegema bandari kama chanzo cha mapato ikitokea miaka ya mbeleni zinabuniwa ndege kubwa zinazoweza kubeba mizigo mikubwa na kwa gharama nafuu kutokana na kukua kwa teknolojia akitolea mfano wa wamarekani wanaowaza/wanaobuni nishati mbadala ya mafuta ikitokea mafuta yanatoweka duniani.
Msigwa kaongea mengi yanayoeleza ni jinsi gani watanzania wa leo hatuwazi critically.
Binafsi naungana na Msigwa kwasababu moja kubwa: Watanzania wa leo hii sehemu kubwa ya mijadala yetu mitandaoni ni kujadili matukio, maandiko na kauli au matamshi ya watu maarufu (wanasiasa, wasanii, n.k)yanayopatikana mitandaoni na kwenye vyombo vya habari na sio kujadili au kubuni mambo yanaweza kuleta suluhu ya matatizo yetu kama nchi.
Kwa maneno mengine,tunatumua muda mwingi au niseme interest zetu ni kulalamikia matatizo tuliyonayo huku tukitumia muda mchache kuandika, kujadili na kupendekeza solution za matatizo yetu, tunasahau matukio yanakuja na kupita, wakati matatizo yetu yako pale pale huku watawala nao wakiwa hawana solution ya baadhi ya matatizo tuliyonayo.
Kama anavyosema Msigwa, kwa sasa hatuna mijadala sababu mojawapo likiwa ni uoga lakini pia kwa sasa level yetu ya ku-think critically imeshuka.
Kwenye mitandao kwa sasa, mtu aki- post habari kuhusu tukio fulani au kauli ya mwanasiasa fulani, watu wanakuwa interested sana kujadili ila mtu akija na idea kuhusu namna gani tunaweza kutatua tatizo fulani katika jamii na nchi kwa ujumla, mijadala huwa ni ya kiwango cha chini sana(wa kukosoa na kuungana mkono ni wachache mno).
Kwa mfano, hivi sasa watanzania tunatakiwa tuwe na mjadala utakaosaidia kupatikana kwa vyanzo vipya vya mapato, ila hilo alipo, badala yake tunalalamika kukamuliwa kodi huku TRA nao wakiwa wameishiwa ubunifu wa kupata vyanzo vipya vya mapato na matokeo sasa wanatuhumiwa kutoza kodi kubwa inayoua mitaji ya wafanyabiashara(hakuna mwenye solution juu ya vyanzo vipya vya mapato badala yake wote tunalalamika!)
Mimi naamini vyanzo vya mapato nchi bado viko vingi tu, tatizo ni watu kushindwa kukaa chini na kuumiza vichwa ikiwa ni pamoja na kushirikishi wananchi na wataalumu katika mijadala ya pamoja yenye lengo la kubuni vyanzo vipya vya mapato.
Hata mnapoona wasomi na wanaoitwa wataalamu wanakimbilia kwenye siasa, mjue kweli level of thinking imeshuka, hivyo wanashindwa kutumia elimu zao kujiongezea vipato halafu mkabaki mnategemea watu wa aina hiyo ndio wawaletee maendeleo.Kama mnaamini hivyo, mjue tu huko ni kujidanganya mchana kweupe.
Watanzania tubadilike, dunia inatuacha nyuma.