Nakubaliana na mchungaji Msigwa kuwa level of thinking Tanzania imeshuka

Nakubaliana na mchungaji Msigwa kuwa level of thinking Tanzania imeshuka

Kwenye mada yako ulikumbuka kusema hao walimu wenye miaka chini ya 35 wapelekwe wapi?

Au vyuo viache kuzalisha walimu wenye umri chini ya huo? kama vyuo vikiwazalisha mahitaji yao kimaisha (kula na mengine) watayapata kwa nani?

Inaonekana huo uzi wako ulikuwa na maswali mengi sana kuliko majibu.

N.B: Kama unataka mada yako usiejulikana ipate wachangiaji wengi sharti ihusu tukio lenye kuvuta hisia za watu, mfano; Ndugai kasema nini kuhusu Chadema, au Bunge limepitisha sheria gani ya ajabu, au viongozi gani wa upinzani kapatwa na jambo gani ( kufukuzwa uanachama n.k)

Lakini ukileta mada fikirishi wewe usiejulikana pole sana, hutapata wachangiaji wa kutosha, wenye hiyo privillege ni wachache kama Pasco sababu ya ukongwe wake humu jf
hata kama sikufika vya kutosha basi great thinkers wenzangu wangesaidia kufika huko na sio kupuuzia uzi na kutukana
 
Kwenye mada yako ulikumbuka kusema hao walimu wenye miaka chini ya 35 wapelekwe wapi?

Au vyuo viache kuzalisha walimu wenye umri chini ya huo? kama vyuo vikiwazalisha mahitaji yao kimaisha (kula na mengine) watayapata kwa nani?

Inaonekana huo uzi wako ulikuwa na maswali mengi sana kuliko majibu.

N.B: Kama unataka mada yako usiejulikana ipate wachangiaji wengi sharti ihusu tukio lenye kuvuta hisia za watu, mfano; Ndugai kasema nini kuhusu Chadema, au Bunge limepitisha sheria gani ya ajabu, au viongozi gani wa upinzani kapatwa na jambo gani ( kufukuzwa uanachama n.k)

Lakini ukileta mada fikirishi wewe usiejulikana pole sana, hutapata wachangiaji wa kutosha, wenye hiyo privillege ni wachache kama Pasco sababu ya ukongwe wake humu jf
Mkuu, kuhusu mada yake, nafikiri ilikuwa ni jukumu letu sisi wachangiaji/wasomaji kumsaidia mawazo kwa nia ya kuboresha na hata kukosoa kama ulivyofanya hapa ili mwisho wa siku lipatikane wazo bora(penye wengi hapaharibiki neno-wahenga).

Kuhusu kuleta mada fikirishi huku haujulikani, ulichokisema ni kweli kabisa. Kama sio maarufu, unaweza kuja na mawazo mazuri sana juu ya jambo fulani na usipate wachangiaje huku mtu maarufu hata akija na mada isiyo na mashiko, bado atapata wachangiaji wengi hata kama asilimia 90 watakuwa wanamponda /wanamksoa ila mada yake bado itakuwa hapa jukwaani kwa muda mrefu.

Kwa kifupi hili ndio tatizo, na kibaya kwa sasa watu maarufu hawasikiki sana wakitoa maoni yao hivyo hali hii inakuwa ni sawa na kuongeza tatizo juu ya tatizo.

Yaani wakati watu wasio na umaarufu mawazo yao hayana uzito kwenye media na mitandao, watu maarufu wenye ushawishi nao wako kimya kushauri, kukosoa, kukemea, n.k wakihofia usalama wao na wengine wakihofia kupoteza vibarua vyao.Kwahiyo, kwa sasa tuko katika mkwamo fulani tofauti na miaka ya nyuma ambapo ilikuwa kila wakati tunaleta mada humu juu ya nani kasema hivi au kashauri kile.

Kwa sasa wasemaji wa mara kwa mara waliobaki ni kina Askafu Bagonza, Hilder Newton, Kigogo2014, Maria Sarungi na Fatima Karume na wengineo wachache wanaojitahidi kukosoa na kushauri mara moja moja kama kina Zitto, Lissu na wengineo wachache.
 
Great thinkers haina maana ya upambanaji,au patriotism. Great thinker ni mawazo tu yenye hekima lakini sio lazima wawe wapambanaji.
Mchungaji labda kajichanganya,ingekuwa vizuri akaandika jarida ili tumunukuu vizuri.

Sio kweli kwamba Great thinkers ilipotea baada ya Nyerere kustaafu,labda amesahau wakati Mwabulambo na Sita walimpomtamkia Mwakimu Nyerere AFADHALI YA MKOLONI alifunga chuo na wengine akawalamba viboko.

Kwa maana Nyerere hakuvumilia challenge ya mawazo au mwelekeo.

Lakini wakati huo sio kweli Thinking capacity inayozaa Great thinkers inadolola,bali wanasiasa wanashindwa kufanya kazi zao.

Hakuna mtu anakula rami ya kutengeneza barabara kwa kuwa ina mafuta ndani yake,bali watu wanatumia zaidi mafuta ya alizeti kwa sababu ya kuepukana na matatizo ya blood pressure.
 
Mkuu, kuhusu mada yake, nafikiri ilikuwa ni jukumu letu sisi wachangiaji/wasomaji kumsaidia mawazo kwa nia ya kuboresha na hata kukosoa kama ulivyofanya hapa ili mwisho wa siku lipatikane wazo bora(penye wengi hapaharibiki neno-wahenga).

Kuhusu kuleta mada fikirishi huku haujulikani, ulichokisema ni kweli kabisa. Kama sio maarufu, unaweza kuja na mawazo mazuri sana juu ya jambo fulani na usipate wachangiaje huku mtu maarufu hata akija na mada isiyo na mashiko, bado atapata wachangiaji wengi hata kama asilimia 90 watakuwa wanamponda /wanamksoa ila mada yake bado itakuwa hapa jukwaani kwa muda mrefu.

Kwa kifupi hili ndio tatizo, na kibaya kwa sasa watu maarufu hawasikiki sana wakitoa maoni yao hivyo hali hii inakuwa ni sawa na kuongeza tatizo juu ya tatizo.

Yaani wakati watu wasio na umaarufu mawazo yao hayana uzito kwenye media na mitandao, watu maarufu wenye ushawishi nao wako kimya kushauri, kukosoa, kukemea, n.k wakihofia usalama wao na wengine wakihofia kupoteza vibarua vyao.Kwahiyo, kwa sasa tuko katika mkwamo fulani tofauti na miaka ya nyuma ambapo ilikuwa kila wakati tunaleta mada humu juu ya nani kasema hivi au kashauri kile.

Kwa sasa wasemaji wa mara kwa mara waliobaki ni kina Hilder Newton, Kigogo2014, Maria Sarungi na Fatima Karume na wengineo wachache wanaojitahidi kukosoa na kushauri mara moja moja kama kina Zitto, Lissu na wengineo wachache.
Hiyo mada yake kama ningeiona ningechangia, tatizo usipokuwa na jina huku thread yako itashushwa chini kila baada ya dakika kadhaa mpaka itapotea kabisa, tofauti na wale wenye majina kama ulivyosema hata kama wakija na mada za hovyo, zitapewa airtime ya kutosha, hata two consecutive days thread itabaki juu tu, and because of this, nadhani huku kuna application ya ule msemo wa "mkono mtupu haulambwi".
 
Tunawasubir Hao kina msigwa wataalam wa kufikir wafikirie kivip kina halima mdee na na wenzake kwa nn wataendelea kua wabunge na watabaki kua wanachama wa chadema!?
Hili ndio jibu lenyewe la mada.viva Msigwa vivaaah
 
Msigwa anasahau kuwa haya yote yametokana na kuwa na katiba mbovu ambayo inampa mtu mmoja umungu mtu bila sababu, tulitegemea bunge itakuwa ni sehemu sahihi lakini nalo ni tawi la CCM hakuna tena mijadala ya maana.
 
Umenena vyema sana, binafsi naweza nikasema kwamba hoja kama hii ili iweze kuwa na mashiko! Wewe Mr Salary Slip uwe ni mstari wa mbele kuungana na serikali pale inapo fanya vyema na kuikosoa pale inapo fanya vibaya. Mada za CCM mara Chadema mara CUF zisiwe na kipaombele haswa wakati kama huu badala yake vipaombele vyetu iwe ni namna ya kuonyeshana fursa za hapa na pale na jinsi gani mtanzania wa kawaida anaweza kuyatumia vyema mazingira anayoyaishi kumpatia kipato na jinsi gani au mbinu ipi sahihi anaweza itumia kujipatia mtaji.

Binafsi ninaamini watanzania wengi wana IQ nyingi tu, ila hao wanasiasa kama huyo Msigwa swala la kuchanganya siasa katika maisha ndilo linalomfanya adhanie kwamba wa Tanzania tunalow thinking capacity.

Kuikosoa serikali kwa kila jambo, haimaanishi kwamba ndio kigezo pekee cha kuipima thinking capacity ya watu.

Angejaribu kuugeuza mtizamo wake wa kawaida na kuanza kuifikiria Tanzania kwa mapana na maono ya mbali, kunawakati ataona amefanya jambo kubwa ambalo linaweza kuinua matumaini ya walio wengi hususani katika kuzichangamkia fursa ambazo zipo maeneo yao lakini hawazioni ila wanahitaji msaada wa mtu kama yeye kutokana na status aliyokuwa nayo hapo awali.

Luge Mutahaba anaweza kuwa ni miongoni mwa watu wanaoweza kukumbukwa sana na vijana wa kisasa kutokana na talanta yake vivyo hivyo pia! Hata Msigwa na yeye, anaweza kuwa kama Marehemu Luge Mutahaba kama ataamua kuweka siasa pembeni.
 
Hoja ya Msigwa haina nguvu ok anasema kipindi cha Nyerere thinking ilikuwa kuwa sasa mbona uchumi ulikuwa chini?

Thinking kuwa kwa wenzetu iko private sector hawawezi tu solution kwa kujaza tu hali wanatafuta new business ventures

Msigwa mwenyewe na Chadema wenzie wana thinking kubwa ya kitu gani nje ya porojo za kisiasa?

Charity begins at home
 
Msigwa anasahau kuwa haya yote yametokana na kuwa na katiba mbovu ambayo inampa mtu mmoja umungu mtu bila sababu, tulitegemea bunge itakuwa ni sehemu sahihi lakini nalo ni tawi la CCM hakuna tena mijadala ya maana.
Uingereza na Israel hawana katiba za nchi mbona wamerndelea?

Visingizio vya kitoto
 
Msigwa anasahau kuwa haya yote yametokana na kuwa na katiba mbovu ambayo inampa mtu mmoja umungu mtu bila sababu, tulitegemea bunge itakuwa ni sehemu sahihi lakini nalo ni tawi la CCM hakuna tena mijadala ya maana.
Mimi naona kwa sasa sisi wananchi wa kawaida tuitumie mitandao kuibua fursa, kuonyesha vyanzo vya mapato, kushauri ,n.k kwani tusitegemee hili Bunge la sasa kuja na mawazo kama hayo, na bahati mbaya wanasiasa wa upinzani hata wakitoa mawazo mazuri kasi gani ni vigumu kufanyiwa kazi kutokana na chuki ya kisiasa iliyopo hivyo ni bora sisi wananchi tukabeba jukumu hilo.

Kikwazo kingine ni serikali kutosikiliza ushauri hata kutoka kwa wana-CCM wenzao, mfano mtu kama Hussein Bashe alikuwa anatoa mawazo mazuri sana Bungeni ili serikali haiyafanyii kazi huku yenyewe ikiwa haina jipya/suluhisho la matatizo yetu ya kiuchumi, n.k.

Kwa mfano, ubunifu wa vyanzo vya mapato na fursa mpya za kiuchumi ni moja ya mambo ambayo naamini kabisa watunga sera wameshindwa kuyatimiza na badala yake ni kutozana makodi makubwa kutoka vyanzo almost vile vile vya miaka nenda miaka rudi.
 
Angeweza ku-think critically CHADEMA isingeserereka kwa huo mserereko! Kuna tofauti Kati ya muuza maneno ya ujanja ujanja na mtendaji mwenye maono na nia thabiti!
 
Angeweza ku-think critically CHADEMA isingeserereka kwa huo mserereko! Kuna tofauti Kati ya muuza maneno ya ujanja ujanja na mtendaji mwenye maono na nia thabiti!
We ndio wale wale!!
 
Wapo watu wa aina tofauti katika maisha, wapo waliozaliwa kujisimamia na wale waliozaliwa kusimamiwa. Watu hawa wana utofauti mkubwa sana katika kufikiri kwao na hata mitindo ya maisha yao.


Siyo wote wenye uwezo wa kudadavua hoja ngumu na hata wakati mwingine hoja nyepesi.

Kuna watu wanafikiria kufanya jambo, kuna watu wanafanya, na pia lipo kundi la watu ambao wao kazi yao ni kutazama tu mambo yakiwa yanatendeka.

Niseme tu ukweli humu jf kuna watu wana uelewa MKUBWA sana siyo siri.

Pamoja na yote lazima tufike hatua tukubali utofauti wa uwezo wa kufikiri wa kila mmoja. Mada za ajabu zinapewa kipao mbele kwasababu ni nyepesi na hazihitaji mtu kufikiria sana ndiyo maana wengi wapo huko, ila zile mada ambazo mtu unahitaji kufikiria sana zina wachache kwasababu watu hao pia siyo wengi.


Ni kweli asilimia kubwa ya sisi watanzania suala la kuhoji vitu kwa lengo la kuelewa au kujifunza ni utamaduni ambao wachache ndiyo wanao.

Jf ya sasa ni tofauti na ile iliyonisukuma mpaka kujiunga rasmi.

Kuna watu walikuwa wanatoa elimu kuhusu vitu mbalimbali muhimu sana katika maisha na wachangiaji walikuwa very bright katika kuhoji.
 
Kuna clip iko kwenye mitandao ikionyesha mahojiano aliyofanyiwa mchungu Msigwa na Darmpya tv, ambapo mchungaji Msigwa anasikika akiongelea swala la critical thinking.

Msigwa anasikika akisema, wakati wa Mwalimu, vijana wa chuo kikuu walikuwa na uhuru wa kusema chochote wawapo maeneo ya chuo na walikuwa na kinga ila kinga hiyo ilikuja ondolewa enzi za Mwinyi baada ya wanafunzi wa chuo kikuu wakati huo kumkosoa mzee Mwinyi.

Kwa maelezo yake, Msigwa anasema Mwalimu aliruhusu mijadala vyuo vikuu na kwamba vyuoni ni sehemu ambapo watu wana-think critically tofauti na sasa ambapo wanafunzi wa vyuo vikuu hawawezi hata kuuuliza maswali ya how,why, n.k.

Msigwa amesema wanafunzi hawa sio wa kulaumiwa kwani hata walimu wao nao hawa-think critically huku akitaja kutishwa kuwa ni moja ya sababu ya walimu wao kuwa hivyo.

Msigwa anahoji kama ma-proffesor wetu wanaka chini na kuumiza vichwa kuhusu hatima ya Tanzania yetu kiuchumi, n.k katika miaka 30 ijayo huku akitoltea mfano wa nchi kama Israel ambayo inauza "brain" duniani na wamarekani wanaowaza nishati mbadala ya mafuta kwa miaka 30 ijayo.

Kwa mfano, Msigwa anahoji tumejiandaa vipi kuacha kuitegema bandari kama chanzo cha mapato ikitokea miaka ya mbeleni zinabuniwa ndege kubwa zinazoweza kubeba mizigo mikubwa na kwa gharama nafuu kutokana na kukua kwa teknolojia akitolea mfano wa wamarekani wanaowaza/wanaobuni nishati mbadala ya mafuta ikitokea mafuta yanatoweka duniani.

Msigwa kaongea mengi yanayoeleza ni jinsi gani watanzania wa leo hatuwazi critically.

Binafsi naungana na Msigwa kwasababu moja.kubwa: Watanzania wa leo hii sehemu kubwa ya mijadala yetu mitandaoni ni kujadili matukio, maandiko na kauli au matamshi ya watu maarufu (wanasiasa, wasanii, n.k)yanayopatikana mitandaoni na kwenye vyombo vya habari

Kingine, tunatumua muda mwingi au niseme interest zetu ni kulalamikia matatizo tuliyonayo huku tukitumia muda mchache kuandika, kujadili na kupendekeza solution za matatizo yetu, tunasahau matukio yanakuja na kupita, wakati matatizo yetu yako pale pale huku watawala nao wakiwa hawana solution ya baadhi ya matatizo tuliyonayo.

Kama anavyosema Msigwa, kwa sasa hatuna mijadala sababu mojawapo likiwa ni uoga lakini pia kwa sasa level yetu ya ku-think critically imeshuka.

Kwenye mitandao kwa sasa, mtu aki- post habari kuhusu tukio fulani au kauli ya mwanasiasa fulani, watu wanakuwa interested sana kujadili ila mtu akija na idea kuhusu namna gani tunaweza kutatua tatizo fulani katika jamii na nchi kwa ujumla, mijadala huwa ni ya kiwango cha chini sana(wa kukosoa na kuungana mkono ni wachache mno).

Kwa mfano, hivi sasa watanzania tunatakiwa tuwe na mjadala utakaosaidia kupatikana kwa vyanzo vipya vya mapato, ila hilo alipo, badala yake tunalalamika kukamuliwa kodi huku TRA nao wakiwa wameishiwa ubunifu wa kupata vyanzo vipya vya mapato na matokeo sasa wanatuhumiwa kutoza kodi kubwa inayoua mitaji ya wafanyabiashara(hakuna mwenye solution juu ya vyanzo vipya vya mapato badala yake wote tunalalamika!)

Mimi naamini vyanzo vya mapato nchi bado viko vingi tu, tatizo ni watu kushindwa kukaa chini na kuumiza vichwa ikiwa ni pamoja na kushirikishi wananchi na wataalumu katika mijadala ya pamoja yenye lengo la kubuni vyanzo vipya vya mapato.

Hata mnapoona wasomi na wanaoitwa wataalamu wanakimbilia kwenye siasa, mjue kweli level of thinking imeshuka, hivyo wanashindwa kutumia elimu zao kujiongezea vipato halafu mkabaki mnategemea watu wa aina hiyo ndio wawaletee maendeleo.Kama mnaamini hivyo, mjue tu huko ni kujidanganya mchana kweupe.

Watanzania tubadilike, dunia inatuacha nyuma.
Kwa kifupi tu nikupongeze kwa kuanzisha uzi wenye hoja nene na nzito. Msingwa ameongea jambo la msingi sana. Katika wanasiasa wa Tanzania na chadema especially huwa ninavutiwa sana na hoja binafsi za msigwa na namna anazungumza hoja zake.

Hili alilolisema msigwa ni swala mtambuka. Tupo na elimu na mfumo wa elimu usio na tija kwetu kama taifa. Tumekalia tu kujisifu tuna elimu na mapambio yasiyolenga ukweli, ila mjadala uliopo sasa ambao sijui ni kwann tunaogopa kuuanza ni swala elimu inatusaidiaje sisi kama raia na taifa kwa ujumla.

Katika eneo la ajira hii elimu imeshafeli, so kwa wale waanopeleka watoto shule ili waje kuajiriwa ni mission impossible.

Tukija upande wa kupata maarifa hii elimu inaongeza tu ugumu wa kutumia maarifa badala ya kukupa uwezo w kutumia maarifa yako.

So kimsingi msigwa anatumia platform yake ya siasa vema sana kwa kuongea mambo ya msingi badala ya upuuzi wa Chadema this, chadema that..... Amefocus kwenye mambo ya msingi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtu anajibatiza kabisa kuwa yeye ni mpinzani kwamba yeye kazi yake ni kupinga tu,sasa mtu kama huyo utajadiliana nae vp hoja zengine tofauti na zile za kulaumu na kutafuta mchawi?

Na kibaya hao ndio wako wengi humu na hivyo mada zenye kuwavutia ni ambazo zinawapa uwanja wa kukosoa tu na kulaumu,na bora wangekuwa wanakosoa yeyote kwa jambo lolote wanaloona halipo sahihi ila hali haipo hivyo ni kinyume chake.
 
naunga mkono hoja kuhusu watanzania wengi kushughulika na vitu vidogo. mfano wangu upo humuhumu jf kwa 'great thinkers', nilikuja na thread fikirishi kabisa inayohusu haja ya kuajiri walimu wa kike kuanzia miaka 35 badala ya hii 18,19,20....25. mada ilichangiwa na wadau wachache sana huku nikipata kiji'like' kimoja tu. katika hao wachacheee waliochangia, asilimia 98 waliishia kunitukana tu....tena wengine matusi ya nguoni. 😵😵

ajabu ni kuwa threads za kidukulilo za kumiliki visiwa sehemu mbali mbali duniani na magari ya kifahari zaidi ya ronaldo na messi zinapata ma'likes' na 'replies' nyingi ajabu.

kitu kingine nilichogundua humu ambacho kinaendana na ulichoandika mtoa mada ni kuwa hata humu, kwa ma'great thinkers', mada huangaliwa kwanza imetoka kwa nani ili ajibiwe au isomwe......kama hauna jina humu si ajabu mada zako hata kufunguliwa zisifunguliwe. ni dalili tosha ya ulichokisema.....tatizo la kukosa critical thinking limetuvamia hadi humu.
Ni kweli kabisa, tuna ushabiki sana na uteam humu jf jambo ambalo ni utoto sana kwa platform kama hii ambayo inatakiwa watu tuwe na mijadala fikirishi na yenye mantiki.

Tukiendelea na hizi akili za kimakundi hii platform haitakuwa na maana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom