Nakubaliana na Rais Mwinyi kwamba Manaibu Waziri wanaongeza gharama za Serikali naamini Rais Magufuli atafanya hivyo pia!

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Kiukweli sehemu moja muhimu ya kupunguza matumizi ya Serikali ni kuwaondoa manaibu waziri kwani zaidi ya kujibu maswali bungeni huwa sioni kazi nyingine ya maana wanayofanya.

Katika hili nakubaliana kabisa na Rais wa Zanzibar Dkt. Mwinyi la kutoteua manaibu Waziri katika baraza lake.

Ni imani yangu utaratibu huu una baraka za chama na hata Rais Magufuli atafanya vivyo hivyo.

Maendeleo hayana vyama!
 
Zanzibar ni ndogo sana mkuu hamna haja ya manaibu ila kwa mainland inakuwa ngumu kidgo Tanganyika ina eneo kubwa manaibu muhimu.
 
Kwa Maoni yangu Wafuatao inatakiwa wafutwe kabisa kwenye mfumo wa serikali watafute Kazi zingine za kufanya.

1. Manaibu waziri. (Mawaziri na makatibu wa wizara wanatosha kabisa kusaidiana Kazi na zikaenda)

2. Wabunge wa viti maalamu (Wabunge waliochaguliwa na wananchi na wale 10 wa Rais wanatosha kabisa kuwawakilisha vyema wananchi wao).

3. Ma driver wa Wabunge (Ilitakiwa kila Mbunge aajiri driver wake Kama anahitaji kuendeshwa na Wala siyo kuitwisha mzigo serikali angali inampa pesa ndefu kwa Kazi ya kupiga meza na kusinzia kwenye Bungeni).

Ni hivyo tu nalog Off.
 
Bwashee umefail sana. Zanzibar na Rwanda inawezekana kuwa na wizara bila manaibu mawaziri kadhalika na makatibu wakuu bila kuwa na manaibu. Ila Tanganyika sio rahisi mkuu. Hili linchi ni likubwa sana bwashee. waziri hawezi hata kidogo kufanya kazi nchi nzima hasa wizara kama ya fedha, Afya, elimu na wizara nyingine nyeti zinazohitaji ukaribu sana kama kilimo. Akifanya hivyo atakuwa amekurupuka na nitampa miezi miwili ataanza upya japo anajiona kichwa ngumu.
 
Hamna kitu mkuu Zanzibar chini ya utawala wa mabeberu weusi waliokalia kijeshi kila kitu ni shauri kwa bwana.
 
Manaibu waziri wapo kwa mujibu wa katiba. Asipowateua amevunja katiba
 
Ukishakuwa na TAMISEMI huitaji manaibu waziri kwa sababu hawana kazi za kufanya na ndio maana muda wote huwaletea figisu mawaziri ili wachukue nafasi zao.

Nitajie kazi za naibu waziri!
 
Nimekuelewa bwashee!
 
Kabsaaaa
 
Zanzibar ni mikoa miwili tu, bahati yao inaitwa nchi, sioni umuhimu wa manaibu Waziri hata Mawaziri wanatakiwa wawe saba tu.
Kule kunatakiwa wakuu wa wilaya wawili tuu, wilaya ya Pemba na wilaya ya Unguja. Pemba iwe mkoa wa Tanga na Unguja iwe mkoa wa dar. Basi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…