Nakuchukia Baba yangu

Nakuchukia Baba yangu

"Kijana wa kiume kadri anavyokuwa ndivyo anavyoendelea kumsamehee Baba yake". Ni nukuu ya walioona mengi wanawake wana mitihani migumu tusisahau hata mama zetu ni wanawake. japo siyo justification ya kina baba kutotimiza wajibu
 
Mimi sio nabii ila nimeshuhudia maandiko kadhaa ukiisifia yanga na kuwa na matumaini nayo hata pale inapofanya vibaya,be a man.
So long as baba yako yupo hai kuna siku utajua ukweli ndugu,Usichukie asili yako.
mengine ni changamsha genge tu mkuu!
 
Wakuu,

Nimelelewa na mama yangu kwa asilimia 90 mpaka hapa nilipo.

Baba yangu aliondoka nyumbani mwaka 2011 akamuacha mama yangu akiwa amejifungua wiki mbili akaenda kusikojulikana na mwanamke mwingine, akatuacha hakuna chakula wala matumizi yoyote ya mama na sisi wanafunzi, Ilibidi mama aanze vibarua ili tule na tusome mimi na dada yangu ninaemfuata.

Hata sisi tulipotoka shule ilibidi twende kwenye vibarua kwa ajili ya chakula na madaftari, sabuni na matumizi mengine.

Nimepitia mateso makuu sana mpaka nimefika hapa nilipo kwa sababu ya baba yangu! Siku nyingine nitawaletea mkasa mzima ila kifupi namchukia mno baba yangu!
We mjinga kweli. Mungu anakupitisha kwenye darasa na ushafaulu unawalaumu wengine. Mi cjawah kulelewa na baba yangu na kuna mastori mengi mabaya nilipewa juu yake namaliza msingi 93 mpaka nakuja kumuona kamanda ni 2009 alikuwa mshikaji wangu wa kufa na nilijifunza mengi sana kwake. Ushaur wangu kwako acha kuishi historia mzee. Acha kuishi life ya mtu. Una wajibu kwako binafs kwa mungu wako na kwa familia yako huna muda wa kuwaza mabaya ya mtu. Tengeneza historia yako na muombe Mungu sana ili kabla siku zako haziajisha akusaidie kutimiza ndoto zako. Maisha ni mwalimu na muda ni dawa. Ukipata muda kama hutajali ukipata muda kaa na mzee wako mfurahishe halafu muulize mzee, kwa mfano mtu akikurudisha kwenye umri wa miaka 25 leo ni kitu gan hutafanya na kipi utafanya ambacho ulifanya kikakuharibia plan zako. Utaona atakavyotiririka. Nakukumbusha tena kuwa na chuki au malalamiko au kushtaki mtu ni kazi ya shetan. Maadamu unaish hata wewe unaweza kufika alipopita mwenzio. Kikubwa kila kitu mshukuru Mungu amekupitisha hiyo shule usirudie anapoona alipokosea. Tunawekewa historia tujifunze sio kuchukia na kulaumu. Fanya maisha yawe bora kwako na kwa wengine. Usichangie kuiharibu dunia plz. Kwasababu pamoja mabaya yote hakosi Zuri lolote so tumia hilo zuri ili ukue kiakili. Mabaya muachie. Hongera kwa kukua.
 
Wakuu,

Nimelelewa na mama yangu kwa asilimia 90 mpaka hapa nilipo.

Baba yangu aliondoka nyumbani mwaka 2011 akamuacha mama yangu akiwa amejifungua wiki mbili akaenda kusikojulikana na mwanamke mwingine, akatuacha hakuna chakula wala matumizi yoyote ya mama na sisi wanafunzi, Ilibidi mama aanze vibarua ili tule na tusome mimi na dada yangu ninaemfuata.

Hata sisi tulipotoka shule ilibidi twende kwenye vibarua kwa ajili ya chakula na madaftari, sabuni na matumizi mengine.

Nimepitia mateso makuu sana mpaka nimefika hapa nilipo kwa sababu ya baba yangu! Siku nyingine nitawaletea mkasa mzima ila kifupi namchukia mno baba yangu!
Kwa umri wako wa miaka 14 bado haujajua maisha na huenda utakapojua wanayopitia wanaume huenda ukamsamehe na kumuelewa baba yako.

Nakushauri usimchukie baba yako zaidi jitahidi kumuheshimu na kumkubali jinsi alivo.
 
sio miaka 14 mkuu, wakati mzee anaondoka sisi ndo tuliokuwa tunaenda vibaruani kumlisha mama na mahtaji ya shule.
 
Hakuna justification za kumchukia baba yako wewe.
Bora kukaa neutral.Unatamka kabisa unachukia baba yako ,unaandika kabisa unaichukia asili yako.

Nani amemchukia baba yake dunia hiii akatoboa?

Hizo ni superstition tu, lakini ukweli utabaki kuwa pale pale, if you're an asshole you don't deserve to be a dad. Ndio maana baadhi ya nchi felons hawaruhusiwi kuishi na watoto wao.
 
Nimesoma tena, yupo yeye na dada yake. Yeye ndio kafuata, kwahiyo yeye ndio mdogo aliechwa na wiki 2? Vyovyote iwavyo, yeye kajuaje Baba yake kaondoka na mwanamke mwingine?
Ana wazimu huyo kasimuliwa tu anakuja kuandika anamchukia babà yake, kabisa uichukie asili yako
 
Nimesoma tena, yupo yeye na dada yake. Yeye ndio kafuata, kwahiyo yeye ndio mdogo aliechwa na wiki 2? Vyovyote iwavyo, yeye kajuaje Baba yake kaondoka na mwanamke mwingine?
yeye (mleta mada ambaye ni mimi) wakati mama yake amejifungua wiki mbili baba yake akakimbia, yeye (mimi) pamoja na dada yake (yangu) wakati wakisoma (tukisoma) wa(tu)lilazimia tukirudi shule tunaenda kwenye vibarua kwa ajiri ya chakula na mahtaji ya shule.
 
Wewe ulijuaje kama ameondoka na mwanamke mwingine?
 
Back
Top Bottom