Nakuchukia Baba yangu

Mtafute baba ako umsikilize nae ana lipi la kusema kwa upande wake.
 
Kwanza pole sana kiongozi, hii huwa inaumiza mno.

Nawaona watu wanajaribu ku-excuse tabia zisizofaa kwa kisingizio labda mama yako ndiyo alikua na shida.
Hata kama ingekua ni ukweli, kwani ukikorofishana na mkeo ndiyo unaacha kua baba na kujitoa kabisa kwenye kuhudumia watoto wako? Baba unawezaje kumtelekeza mama watoto wako na kichanga cha wiki mbili 😢 na watoto wengine saba.

Watu kama mzazi wako wapo wengi na ni mwiba sana kwenye jamii. Kaa naye mbali huyo mzee, ni mwanaume mwenye uwezo wa kuzalisha ila siyo baba!
 
Mkuu mahusiano yana Mambo mengi we unaweza kumuona Baba yako ana roho mbaya kumbe amerogwa wanawake wabaya sana kwenye Mambo ya ndoa.
 

Hii story amekupa maza. Sasa tafuta muda upate version ya mzee halafu uje tujadili
 
Kumbuka kuna ishu ya kubambikiwa mtoto uko kwenye ndoa. Hapo busara ni dogo kumtafuta mshua asikilize na story ya upande wa pili.
 
Nadhani kumchukia baba yako sio ishu hata kidogo haimuongezei wala kumpunguzia kitu.

Watoto wengi huegemea kwa mama zao na hasa mama akiwa pa mdomo sana . Wanawake waliowengi wakiwa na waume zao wana tabia ambazo ni ngumu kuvumilia na wao hujiotesha mapembe!

Nasimama upande mmoja na mshua wako!
#Team #Kataa ndoa , NDOA NI UTAPELI
 
Kumbuka kuna ishu ya kubambikiwa mtoto uko kwenye ndoa. Hapo busara ni dogo kumtafuta mshua asikilize na story ya upande wa pili.
Mtoa nyuzi amesema mzee alirudi na ameozesha watoto wake wa kike wa3 na kuchukua mahari. Kama kungekua na ishu ya kubambikiwa watoto iliyomfanya awatelekeze, je angerudi kwenye haya?
 
mama yangu tangu aolewe na baba mwaka 1986 hadi leo hawawahi kuzaa na mwanamme mwngn tofauti na baba yangu mimi, na tuko watoto 8 je mama ni singe maza?
Usibebwe na mkumbo wa mitandao ya kijamii.
Sio singo maza ni mama yako alaah.
 
Mtoa nyuzi amesema mzee alirudi na ameozesha watoto wake wa kike wa3 na kuchukua mahari. Kama kungekua na ishu ya kubambikiwa watoto iliyomfanya awatelekeze, je angerudi kwenye haya?
Whatever it is, sio sawa kutoa hukumu kwa kusikiliza upande mmoja, sana sana kwenye ugomvi wa wazazi ambao wewe ulikua bado mdogo
 
chuki haitakusaidia chochote,bali itazidi kukuumiza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…