Nakuja Dar kusaka maisha! Treni ndio imeanza safari kutoka Kigoma kuja Dar, Mwenye kazi naomba tuwasiliane

Labda ulivomwambia aje alale kwako ndomana akakufata PM[emoji16]. huenda yupo serious, tusubiri hio kesho tumskie yaliyomsibu. Mhh sijui simu yake imeisha chaji au vp

Sent using Jamii Forums mobile app

😂😂😂bas naye hakuwa anasoma comments zetu...mie nilishamwambi sipPend dar..lol nakuaje tena huko...nimemwambia lakini ukikosa kbs pa kulala anialert
 
Baada ya kupigana hapa na pale humu JF nikiwaomba mnisaidie hata kibarua ili nipate hela ya kula nitakapofika Dar, Maombi yangu yanaonekana ni upuuzi!
Watu wananiita mimi ni Muongo, na wengine wakasema mimi ni Tapeli!

Treni kabla haijafika Dar, nikalia lia sana hapa JF nikiomba nisaidiwe nitakapo fika, lakini watu wanazidi kusisitiza "eti, mimi ni tapeli" Huku simu nayo imekaribia kuisha chaji, na treni ndiyo imeshafika Pugu.
Simu ikaisha chaji!
Na hapo niweshawafuata watu kadhaa PM hapa JF akiwemo manengelo na wengine wengi.
Wengine wananipigia simu, ila hawaongei, ambao walisema watanisaidia nikifika, wananiambia kwamba wako Safarini, kwahiyo hawataweza kunisaidia.
Mpaka hapo, nimebaki na elfu moja na mia nne tu.

Baada ya kukosa mtu wa kunipokea, nikaanza kuzurura hapa mjini. Nimezurura sana, na begi langu mgongoni huku nikitembea bize kama wenyeji wa mji wanavyo tembea. Naendelea hapo chini, maana hapa simu imefika mwisho wa kuandika, Kwahiyo naendelea hapo chini!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…