Wakuu leo ni siku maalumu, nataka niuanze mwaka kwa mambo mapya! Hapa nipo ndani ya treni nakuja Dar! Na muda mfupi treni ndiyo imeanza safari,
Sina sehemu ya kuaminika ya kufikia, kwahiyo kama utakuwa na kazi, Tafadhali nisaidie, Na elimu yangu ni darasa la Saba
Ni kama vile una zamia kwenda south Africa 🌍 au ughaibuni na haumjui yeyote....
Nashuhuda nyingi sana za watu kutoboa
KWENYE TUNDU LA HAIWEZEKANI...VITA YETU KUBWA NI NJAA... Karib mjini karibu Bongo DSM
Ukifika usiache kutupa mrejesho.....
Kutokana na ratiba zangu kua ngumu Kuna dogo alizamia dar......akapata waarabu wa kariakoo wakamtumikisha miezi mi5 bila kumlipa..
Alipo ulizia ujira wakamjibu SI ulikua una kula na kulala buree...
Hapa dar es salaam Kuna madalali wanawatafutia watu kazi za majumbani na ushamba boy, mambo ya kutunza garden 🏡🏡
Dalali akamtafuta kazi ya garden Kwa Maza mmoja taita wa kipare ambae mumewe yupo ubalozin nchi za nje....
Anasema yule mmama alikua kisirani na roho mbaya kinoma....hakuna kutoka hata nje ya geti....maana jamaa Ali state hana ndugu dar jamaa anasema alipigishwa kwata sana kama miezi sita...
Siku alipata msala Gani akaja nipigia simu kua amefukuzwa kazi so akawa analala stendi tegeta nje kituoni kama wiki mm still nikawa busy....
Akapata ishu ya kuchimba mashimo bagamoyo....project.....alinambia anatenda huko....still mm nilikua busy...akaja nambia ujira wote unaishia kwenye chakula....
Akanipigia simu akiniomba na kunisihi nimsaidie hifadhi au otherwise arudi nyumbani Kwao mkoa...
AM 4 REAL wakati naanza life nilipangaga nyumba sehemu Moja nzuri hata nilipo hama still Huwa nalipa Kodi Kule japo hakai mtu ndani Kuna Kila kitu....
Nikamwambia Kuna dogo muda Fulani mtakutana nae akupeleke sehemu ambayo utakua unakaa sawa....
Maisha mapya ya kaanza now yule dogo alishaga setlle ana nyumba mjini zaidi ya Moja...
Huwaga akikutana na mm huwaga ana ni treat kama king 👑 ni watu wachache sana unaweza kuwapa chance na wasikuangushee
Nimechoka kuandika.....
NB: MWOMBE SANA MUNGU AWE UPANDE WAKO NA UKUTANE NA WATU SAHIHI.