Nakuja Dar kusaka maisha! Treni ndio imeanza safari kutoka Kigoma kuja Dar, Mwenye kazi naomba tuwasiliane

Sawa mkuu!
 
picha linaanza ka muvi ya solomoni
ghafla vumbi linazidi wajanja wanavaa miwani
hii ndiyo dar, karibu ila usijisikie nyumbani
hapo ubungo usinunue simu utauziwa sabuni
panda daladala tukutane buguruni
kuna watu wanapiga utadhania majini
mtaani usiku utaona rangi zote za bikini
wanauza miili ili wanunue wali maini
usicheke bro kwa sababu mimi si mr. bean
chunga wallet yako hapa kuna wizi wa mfukoni
haukawii kushuka kwenye gari hauna phone
kuwa makini uvukapo huku gari hazipigi honi
daladala zina bajaji inakesha macho
ka huamini ngoja usiku ndo uamini we thomaso
wasio na kazi wanashindia stori za freemason
wajanja wamepanga sinza, kino na tabata
mchana anazibua vyoo usiku anakula bata
usikojoe ovyo bro mgambo watakukamata
hii ndo dar, mbona unadata kabla hata hujapata
starter?............nitaendelea verse ya pili ukifika mkuu


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe jamaa bwana!
 

Ha ha ha. Ni kipaji kuwasoma wanyonge, waliochanganyikiwa kidogo, wanaopenda uchawi, waliokata tamaa. Halafu kuwapiga pesa ndefu.
 

Usimtishe sana kijana wetu. labda kashafika Ubungo.
 

Kamanda!! Unaruka mkojo unakanyaga mavi 😱😱😱
 
Nimefika Uvinza wakuu!
Ushimen @Joseveret
Hazchem plate
Zero IQ manengelo
Kwa mwendo huo, tarajia mtafika Tabora saa kumi na moja - kumi na mbili alfajiri.
Hapo mtakaa mkisubiri treni ya kutoka Mwanza ifike ili muunganishe mabehewa kwaajili ya safari ya kwenda Dar.
Hivyo tarajia kuondoka Tabora mida ya saa mbili - tatu asubuhi
 


Yaani nimemiss hizo safari jaman..dah...tena km una kampani dah..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…