picha linaanza ka muvi ya solomoni
ghafla vumbi linazidi wajanja wanavaa miwani
hii ndiyo dar, karibu ila usijisikie nyumbani
hapo ubungo usinunue simu utauziwa sabuni
panda daladala tukutane buguruni
kuna watu wanapiga utadhania majini
mtaani usiku utaona rangi zote za bikini
wanauza miili ili wanunue wali maini
usicheke bro kwa sababu mimi si mr. bean
chunga wallet yako hapa kuna wizi wa mfukoni
haukawii kushuka kwenye gari hauna phone
kuwa makini uvukapo huku gari hazipigi honi
daladala zina bajaji inakesha macho
ka huamini ngoja usiku ndo uamini we thomaso
wasio na kazi wanashindia stori za freemason
wajanja wamepanga sinza, kino na tabata
mchana anazibua vyoo usiku anakula bata
usikojoe ovyo bro mgambo watakukamata
hii ndo dar, mbona unadata kabla hata hujapata
starter?............nitaendelea verse ya pili ukifika mkuu
Sent using
Jamii Forums mobile app