Nakuja Dar kusaka maisha! Treni ndio imeanza safari kutoka Kigoma kuja Dar, Mwenye kazi naomba tuwasiliane

Nakuja Dar kusaka maisha! Treni ndio imeanza safari kutoka Kigoma kuja Dar, Mwenye kazi naomba tuwasiliane

Wakuu ile safari yangu nadhani leo itafika mwisho, Kwahiyo nisaidieni wakuu, Mnisaidie japo kazi ili nipate hela ya kula.
Dakika kadhaa nyuma ndiyo tumeondoka hapa stesheni ya Morogoro, Asanteni!
Tupia picha, we ni demu au?!
 
Niliishia darasa la saba! Ila nilifaulu, matatizo kadhaa yalinifanya nishindwe kuingia kidato cha kwanza! Kwahiyo mkuu, nisaidie kazi kama ipo!
Haya ukifika dam na cheti chako nitafute pm. Utapata kuna kazi ipo buguruni kimboka
 
tafuta msaada kwingine. umejiridhisha kabisa kwamba wanaJF ndio chaguo lako la kwanza kukusaidia. tafuta wa kwenu huko au mtaa wanaopenda ndio uanzie hapo. la sivyo hatuchelewi kukuona ITV umepotea. jiji la vituko hilo sio Manyovu, Kasulu, Rungwe Mpya au Uvinza na ile salamu pendwa Akavubu.

wanaume kwa wanawake wenye elimu, busara, vianzio vya mitaji, majumba, biashara, viwanja na vichenji benk wanauhama mji wewe unaingiaje kichwa kichwa!

Wafurahie JF kwa kujenga hoja na kukupa ushauri murua kabisa kwa gharama ya bando zako tu lakini kuhusu kugusa pochi na huruma za aina yako utawasamehe. siwasemei wote; wapo wenye tofauti lakini nyakati tulizomo na mwezi huu sio rafiki kwa hitaji lako. watakachokusaidia kwa vile una uelewa wa internet wakupe twitter ya mh. Zito kwa vile naye ni mwanachama na au awe ameshasoma hii post.

kwa hapa nachelea kusema mafanikio yako yakiwa chini ya 25% utakuwa umejaaliwa bahati.

KWELI HUDUMU MILELE, HADAA NA ULAGHAI HUISHA! DAIMA TUUSEME UKWELI HATA KAMA MCHUNGU!
 
Back
Top Bottom