Nakukumbusha tena kaa mbali na mtu Kigeugeu

Nakukumbusha tena kaa mbali na mtu Kigeugeu

Mwanasayansi Kalivubha

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2024
Posts
344
Reaction score
926
Huyu mtu ni hatari sana atakuingiza kwenye matatizo kibao na kuna muda hutojua kama ni yeye kwa sababu mkiwa naye anaongea hivi ila mkiachana tu anaongea mengine.

Mtu kigeugeu mtakubaliana jambo fulani kwa pamoja ila likigeuka likawa na matokeo tofauti na matarajio tayari anakugeuka unaonekana wewe ndio mshukiwa namba moja.

Mtu kigeugeu hujiandaa kufanya hivyo hata kabla ya mambo kuharibika hivyo mnakubaliana ila tayari anaanza mipango ya kukugeuka endapo mambo yatakuwa ndivyo sivyo.

Mtu kigeugeu atakubambikizia makosa yake.

Ishi naye kwa akili nyingi kama hakuna namna ya kumkwepa ila kama ipo basi fanya hivyo.

#Mwanasayansi Saul kalivubha.
#Fikia Ndoto Zako
 
Kuna jamaa ofsini. Ukiandaa presentation au taarifa ya fedha ukiacha PC 🖥 yako wazi akapita anaibadili, mzee unaenda kupresent kitu kingine kabisa.

Siku moja wkt wakuandaa hotuba jamaa si akaichezesha. Masalaleeeeew
 
Back
Top Bottom