Kijana IVO amefungwa Kifungo cha maisha Gerezani Ukonga kwa kesi ya Kulawiti: Criminal case (cc); 165/2020
Kuzaliwa na Vifo vya Wazazi
Miaka 19 iliyopita katika kijiji cha Kifanya huko Mkoani Njombe kijana IVO alikuja duniani na kuiona dunia kwa mara ya kwanza, kwa bahati mbaya sana sana alimpoteza Mama yake kipenzi akiwa na umri tu mdogo wa miaka saba, hivyo alilelewa na Mama wa kambo kuanzia hapo. Akiw ana umri wa miaka 11 akampoteza Baba, hivyo akawa ni YATIMA. Maisha ya kuwa yatima ni magumu sana na yana changamoto kubwa sana.
Kutokana na kukosa usimamizi na malezi halisi ya wazazi kijana IVO alijikuta akiingia katika dunia bila muongoz sahihi wa wazazi wake na aliacha shule akiwa kidato cha pili tu katika shule ya UWEMBA Mkoani humo. Ni majuto, ni vidonda, ni maumivu, hakika dunia haina huruma.
Maisha ya shule
Baada ya kuacha shule mwaka 2017 (kwa sababu za kinidhamu) ndugu upande wa Mama mzazi wakaomba wasaidie kumlea na huku wakitoa ahadi za kumpeleka ufundi na ndo chanzo cha kutoka Njombe kwenda Dar kwa mamake mkubwa (yaani Dada wa Marehemu Mama).
Maisha ya JIJINI DAR
Maisha ya Dar ni mazuri na matamu, hakuna anayetamani kule kijijini kwenye shida na dhiki kusikia safari ya Dar kisha akatae, HAKUNA, na kama yupo atakaua na sababu binafsi sana. IVO alifikia nyumbani kwa Mama yake Mkubwa, kwa ahadi ya kupelekwa kujifunza ufundi wa magari, kazi ambayo Baba marehemu aliifanya enzi za uhai wake, kwa bahati mbaya Mama hakuwa kwenye nafasi kumpeleka kwenye hio fani kwa kipindi hicho na hivyo IVO akiwa kama mtoto wa familia alisaidia kwenye kazi ya kuuza mgahawa wa familia uliokua maeneo ya huko huko.
Pale nyumbani, IVO aliishi na ndugu wengine ikiwa na pamoja na Dada yake (Mtoto wa Mama yake mkubwa) ambaye kwa kipindi hicho alikua na mtoto mdogo aliyekadiriwa kuwa na miaka saba.
IVO na Kesi ya Kulawiti mtoto
Mwaka 2020 Mwezi wa Tano Mama Mkubwa huyu wa IVO alisafiri kwenda mikoa ya kusini kikazi, huku nyuma aliwaacha watoto hawa huku IVO na Dada yake wakiendelea na shughuli za mgahawa. Siku moja Dada mtu alirejea nyumbani na kumuomba IVO amsindikize kwenda kituo cha POLISI kwani aliibiwa simu yake (haijajulikana simu iliibwa lini), Ndugu hawa wawili waliongozana hadi kituo cha Polisi Na ghafla baada ya kufika hapo kijana huyu alikamatwa na kuwekwa mahabusu.
Siku iliyofuata, Askari alimchukua maelezo Kijana IVO kuhusu yeye kulawiti mtoto wa Dada yake hapo kwao nyumbani, hapa ndio kijana huyu, mshamba wa mji kutokea Njombe, asiye na malezi ya Baba wala Mama, kijana Yatima aliyekuja Dar kutafuta fursa, ghafla akaanza kuiona dunia ikimuelemea. Maelezo yalichukuliwa na akaachwa hapo.
IVO apelekwa Mahakamani
IVO anakiri kuwa, kuanzia siku hio tarehe za mwanzo za mwezi wa May, 2020 hakuwahi kupelekwa mahakamani hadi pale tarehe Moja June, 2020 alipofikishwa Mahakamani Kinondoni, kesi yake ikiendeshwa na Mheshimiwa Mshomba na kupewa namba Criminal case (cc); 165/2020.
Kwa mujibu wa kijana IVO, Mpelelezi wa kesi hii, wakati anampeleka Mahakamani alimrubuni kijana huyu kuwa, kesi hii ilikua ni nyepesi tu kwahio alichotakiwa kufanya ni KUKUBALI kosa na Mheshimiwa Hakimu angemuachia huru.
IVO ahukumiwa kifungo cha Maisha Jela
Walimwengu walipata kusema kuwa Dunia haina huruma, Kijana IVO baada ya kurubuniwa na mpelelezi kuwa akubali, alikubali ili kesi iishe na hivyo Mheshimiwa Hakimu Mshomba kulaza damu, akaamua kuwa HUO NDIO UWE MWISHO WA KIJANA IVO, kijana Yatima, Kijana aliyetokea Mkoani, kijana asiye na mbele wala nyuma.
Kijana IVO hakuwahi kupelekwa popote kusikilizwa wala kupimwa sperms wala mtoto hakuwahi kupelekwa kupimwa wala hakuna shahidi aliyethibitisha jambo hili. Je, hakimu aliridhika na UKIRI wa Kijana IVO pasipo kuangalia wala kufuatilia mwenendo wa mashtaka na aina ya mashtaka na umri wa kijana IVO?
Tangu kukamatwa, IVO aliwekwa mahabusu kwa mwezi mzima kabla ya kupandishwa Kizimbani na kuhukumiwa kifungo cha maisha.
KIJANA IVO NA MAISHA MAPYA GEREZANI UKONGA
Ni mchana wa jua kali, ndani ya karandiga, likiendeshwa rafu bila kujali usalama wa watu wengine barabarani, IVO akiwa bado yuko kwenye dunia ya pekee, akimkumbuka Mama ila hayupo, akiwaza laiti Baba yangu angekuepo, lakini hayupo pia, amefikishwa mahakamani na kuhukumiwa bila ndugu yoyote kuwepo, wangejuaje? Ingesaidia nini?
IVO anajikuta amekata tamaa ya kuishi ndoto ya kuwa Fundi Magari, anaikumbuka Njombe, anaielewa Dar isivyo na huruma. Nani wa kusimama na IVO?
Maisha ya nyumbani Njombe
Ni jioni moja yenye utulivu na baridi kali, wanapokea taarifa kuwa Kijana IVO hayupo nyumbani wala hayupo gereji bali yuko Gerezani Ukonga tena akitumikia kifungo cha maisha kwa kesi ya kulawiti. Sio taarifa njema hata kidogo maana ameshakaa karibia miezi sita gerezani bila kumuona wala kumjua ndugu yoyote kwa sura.
Kuokana na uwezo mdogo wa familia zetu, hatimae mwezi wa tano 2021 anafanikiwa kufika ndugu wa IVO gerezani Ukonga siku ya jumamosi.
Ana kwa Ana na IVO
Asikwambie mtu, zile nondo zinakatisha tamaa sana. Baada ya kukaa kwa muda pale mapokezi hatimae jina la Kijana IVO lilipatikana na hatua za kwenda kumuona zilifanyika. Waliachana wakiwa wadogo, wanakutana wakiwa wakubwa tena kwenye matatizo makubwa.
Hakuna kinachozungumzwa cha maana Zaidi ya kutizamana na kulia kwa muda mrefu, ni vilio na machozi kwa pande zote mbili. Ni kama ndoto, ndoto yenye kutisha, ndoto ambayo unatamani isiwe kweli. Ghafla wote wanastuliwa na sauti ya askari kuwa muda umekwisha. Ni ngumu kugeuka nyuma na kuondoka huku ukimuacha ndugu yako, ila sauti kali ya askari yule inasisitiza kuondoka, ni mwisho mchungu.
Ni vilio vya furaha na huzuni, Furaha ya kumuona ndugu tena na huzuni ya ndugu hawa wawili mmoja kuwa kwenye matatizo.
Mwisho na OMBI

- Wana ndugu wanaomba msaada ili ndugu yao aweze kukatiwa rufaa na kesi isikilizwe kwa upya
- Ndugu pia wanatafuta msaada wa kisheria ili kuweza kuendesha rufaa hii
- Tunaomba serikali itusaidie katika kuujua ukweli wa jambo hili
- Wanatanguliza shukrani kwa ndugu wote na marafiki watakoguswa na taarifa hii.
- Simulizi hii ni ya upande mmoja, hivyo ni haki ya mtu atakayekua na utayari wa kusaidia jambo hili kuweza kupata taarifa za upande wa pili.
- Simulizi hii hailengi wala haina nia kwa namna yoyote ile kufarakanisha familia na au wana ndugu, ni kuelezea uhalisia wa upande mmoja.
- Katika simulizi hii pia kuna maswali mengi ambayo majibu yatapatikana kwenye nakala ya hukumu husika, mfano, Kesi ilianzia wapi, mpelelezi alikua nani? Kwa nini Mtuhumiwa aliwekwa rumande kwa mwezi mzima bila kufikishwa mahakamani? Je, mtuhumiwa alipimwa sperms zake vs za yule mtoto aliyeathiriwa? Mashahidi walisemaje na nini ulikua ushahidi wao? Je, kwanini mtuhumiwa hakwenda kupimwa? Pengine na maswali mengine mengi.