Nakumbuka Mitihani yetu ya Darasa la Saba ilikuwa inaanza ivi

Nakumbuka Mitihani yetu ya Darasa la Saba ilikuwa inaanza ivi

*Nakumbuka mitihani ya Darasa la saba ilikuwa inaanza kama utani utani hivi*

19+87=
219-45=
12x34=
59÷7=

Halafu huko mbele sasa kuanzia swali la sita au la saba hivi...utajutaa!!

"Ndege inatoka Dar s
Forums JF Social Forums (Lounge) JF Chit-Chat
saa tatu asbh kwenda Chato. Na gari Toyota Land cruiser linatoka Chato saa nne asbh kwenda Dar.

Ikiwa spidi ya ndege ni 350km/saa na ya land cruiser ni km220/Saa, na umbali wa Chato-Dar ni KM 900, je, zitakutana saa ngapi?"

Ah, sasa mi ntajuaje???
Na hizi tochi zote barabarani na matuta na ishu ya kusimama kujisaidia...ntawezaje kujua watakutana saa ngapi.
[emoji57][emoji57][emoji57][emoji57]
Unajikuta umetoka kwenye pepa umejibu maswali manne tu ya mwanzo kati ya hamsini
hatari kweli nabaadae walikuja kubadili ikawa ni matple choise...unaangalia zako juu unachoma kwenye karatasi kalam iki gota kwenye B ndilo jibu
 
i see ww umemaliza juzi la saba hilo swali la mafumbo ya mdau lilikuwepo sana tulikuwa tunaziita hesabu za umbali=mwendokasi x muda
Nimemaliza kitambo sana, na nilishawahi kufundisha hesabu sekondari, ndio maana najua maswali yake yapoje
 
-MAARIFA
-LUGHA
-HESABU.

Kwa Dar-Es-Salaam ,Enzi Zetu Shule zilizokuwa Zinaongoza kwa Kufaulisha ilikuwa MUUNGANO-TEMEKE na RUTIHINDA zilikuwa noma watu walikuwa wanapiga 150 MUBASHARA.
 
-MAARIFA
-LUGHA
-HESABU.

Kwa Dar-Es-Salaam ,Enzi Zetu Shule zilizokuwa Zinaongoza kwa Kufaulisha ilikuwa MUUNGANO-TEMEKE na RUTIHINDA zilikuwa noma watu walikuwa wanapiga 150 MUBASHARA.
Kumbe umemaliza darasa la saba majuzijuzi,kipindi hicho Rutihinda haikuwepo,shule zilizokuwa noma kwa kufaulisha zilikuwa ni:- Madenge,Muungano zote Temeke, Ubungo NHC,Mlimami,Mapambano,mashujaa zote Kinondoni,kwa Ilala hawakuwa na shule tishio half hivyo vichwa tukawa tunakutana Azania na Tambaza,moto wake ulikuwa si wa kawaida...!!!
 
Haaaaaaa Nimemaliza la 7 mwaka 1989....Haaa hizo Shule zilikuwa Balaaa umenikumbusha mapambano,mlimani.
 
*Nakumbuka mitihani ya Darasa la saba ilikuwa inaanza kama utani utani hivi*

19+87=
219-45=
12x34=
59÷7=

Halafu huko mbele sasa kuanzia swali la sita au la saba hivi...utajutaa!!

"Ndege inatoka Dar saa tatu asbh kwenda Chato. Na gari Toyota Land cruiser linatoka Chato saa nne asbh kwenda Dar.

Ikiwa spidi ya ndege ni 350km/saa na ya land cruiser ni km220/Saa, na umbali wa Chato-Dar ni KM 900, je, zitakutana saa ngapi?"

Ah, sasa mi ntajuaje???
Na hizi tochi zote barabarani na matuta na ishu ya kusimama kujisaidia...ntawezaje kujua watakutana saa ngapi.
[emoji57][emoji57][emoji57][emoji57]
Unajikuta umetoka kwenye pepa umejibu maswali manne tu ya mwanzo kati ya hamsini
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]

Alieniacha hoi ni mwl wangu eti kuanzua la 1 mpaka la 25 hamna kukosaa
Hafu enzi hizo kama unalumbuka idadi ya mboko ni huruma ya mwl.
Ukikosa moja mboko moja

Mwenzangu nikakosa arobaini[emoji134] [emoji134] [emoji134] [emoji134]

Kilichonikuta nikaambiwa ntachapwa paredi
 
mbona unasema hizo hesabu za umbali=mwendokasi x muda hazipo?
nishajibu kitambo hili swali, nimeseama shule ya msingi zilikuwepo, ila hazikuwa compilcated, yalikuwa maswali plain tu, hiyo topic inakuja kujirudia form 3 ambapo ndio kuna maswali kama hayo
 
Hapo unafanya x ndio muda gari litakaotumia kukutana

gari litakuwa limesafiri kilomta 220x
ndege itauwa imesafisafiri kilomita 350(x+1), hiyo ni 1 sababu ya ndege iliwahi saa moja kabla ya gari

Kupata x ambayo ndio muda unatakiwa uzi equate hizo mbili, kwa kuwa jumla ya km ni 900, kilomita ilizosafiri gari lilipokutana na ndege itakuwa ni sawa na 900 utoe km ilizosafiri ndege

220x= 900-350(x+1)
Ukikokotoa utapata x ni 30/19 ya saa
ukitaka kuhakiki unatafuta kilomita ilizosafiri ndege baada ya 30/19 ya lisaa kisha unatafuta na km ilizosafiri gari baada ya 30/19 ya saa, hizo km za gari na ndege ukizijumlisha lazima zilete jibu la 900 kwa kuwa km zote zilikuwa covered.

Darasa la saba kulikuwa hakuna maswali magumu kama hayo, huo ni ukilaza wako unashindwa kutofautisha hata maswali ya la saba na sekondari
Kwa hiyo na ngari itaanzia air port[emoji86] [emoji86]
 
sijafanya hesabu za multiple choice na hata ningefanya bado maswali ya miaka ya nyuma ipo kwenye vitabu vya necta vilivyokuwa vinatoka, hivyo haijalishi mtu kujua maswali ya la saba miaka hata ya 70s achilia mbali hiyo 90s yako yalikuaje,

na narudia tena kama unaamini hilo swali ni la darasa la saba wewe ni kilaza wa hesabu, hilo swali najua solution yake na mtoto wa la saba hawezi kupewa swali kama hilo
Uache ulofa basi, hicho kijiswali kiko kwenye milinganyo ya mwendo kasi.

Na huamini hilo tafuta kitabu kimoja kimeandikwa hivi

"" jiandae vema kumsliza elimu ya msingi""
Au tafuta kitabu kinaitwaga Faulu mtihani wa darasa la saba

Au

Angalia kitabu
"" jipime katika hisabati""
Toleo la kwanza kabisaaaaaa,,, mtihani kama wa arobaini na tano kama dijasahau
Nadhani jirani yake ndio kuna swali moja hivi la umri
Tena wanauzungumzia umri wa tabu...

Kama sijui kama bado vitabu kitabu kimoja hivi kimeandikwa
"" msingi bora wa hesabu darsa la saba" nadhani ilikua hata kabla ya hisabati
 
wewe ni kilaza wa hesabu, kwa mtu anayejua solution ya hilo swali anajua kabisa hilo sio swali la shule ya msingi, ulikuwa huelewi hata maswali ya maelezo inaonekana
Hivi mtu anayefanya solution ya umri wa tabu anafanyeje??

Wacha kukalili. Na kwa taarifa yako hayo maswali sekondari yako kwenye fizikia buana
 
nimemuelewa ila hilo swali la fumbo sio la darasa la saba, ni la sekondari, nasema hivyo sababu najua solution yake na sio ya la saba
Wewe umekomaa na ka solution kakoo
Hujui hata maana ya hesabu embu tukalie kimya bhana[emoji35] [emoji35]
 
-MAARIFA
-LUGHA
-HESABU.

Kwa Dar-Es-Salaam ,Enzi Zetu Shule zilizokuwa Zinaongoza kwa Kufaulisha ilikuwa MUUNGANO-TEMEKE na RUTIHINDA zilikuwa noma watu walikuwa wanapiga 150 MUBASHARA.
Iyo Rutihinda Nilikuwa Naiogopa Sana

Mbaya zaid Walimu wetu walikuwa wanapenda kwenda kutushindanisha
 
Dah haya mambo yalikuwa mazito, sasa usiombe kukutana na swali la umri, yaani ukisolve vibaya unaweza jikuta mjukuu ana miaka mingi kuliko bibi!
Adeki nakumbuka nilipata mjukuu ana umri 20 zaidi ya babu[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]

Hapo kama ilivokua nilipiga jaramba kutafuta umri wa babu mpaka njaa[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Naomba niingilie huu ubishi mkuu chinchilla coat na wadau wengine, hili ni swali la topic gani kwa anayesema ni la darasa la saba, na kwa anayesema ni la form 3.
Hilo kwa darasa la saba au shule ya msingi ni milinfanyo.
Kwa shule ya sekondari iko kwenye fizikia topic ya motion in a streight line na kidato cha tatu kwa mbaali hua linagusiwa kwenye the earth as a sphere
 
Back
Top Bottom