Nakunywa maji lita 5 kwa siku

Brightman Jr

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2009
Posts
1,224
Reaction score
234
Wakuu na wataalamu nisaidieni hapo; je, kuna faida gani na hasara zipi za kunywa kiasi hicho cha maji kwa siku.? Nawasilisha.
 
Wakuu na wataalamu nisaidieni hapo; je, kuna faida gani na hasara zipi za kunywa kiasi hicho cha maji kwa siku.? Nawasilisha.


Muujiza ya matibabu kwa maji ya Uvuguvugu ya kunywa

Miracles from Drinking Hot Water


magonjwa yanatibiwa na maji ya Uvugvugu
- pumu= asthma-
shinikizo la damu= hbp
-
migraine / kichwa= migraine/ headache
-
ugonjwa wa sukari= diabetes
-
upungufu wa damu= anemia
-
maumivu nyuma= back pain
-
mawe katika figo= urinary calculus
-
maambukizo wa haja ndogo= urinary tract infection
- cholesterol= cholesterol-
baridi yabisi & ugonjwa wa mifupa= rheumatism & arthritis
- kiharusi =stroke -
udhaifu wa mwili =sexual and body weakness
-
kuchoka & uchovu = tiredness & fatigue
-
tonsili =tonsillitis
-
vijidudu vya tumbo = gastroenteritis (stomach virus)
-
mafua/homa =colds, flu & fever
- kukosa usingizi= insomnia (lack of sleep)
- kichome kwenye roho= heartburn
- kidonda tumboni =stomach ulcer-
kuvimbiwa (ugumu kupata haja kubwa) =constipation
-
kutetemeka mwili kutokana na umri= parkinsonism
- kupoteza nywele (upaa) =hair loss (baldness)-
magonjwa ya ngozi=skin diseases (psoriasis)
- kasoro ya ubongo =alzheimer (defects of the brain) -
maradhi ya moyo =heart disease
-
saratani= cancer
-
usafisha heidh ya kila mwezi ya wanawake= purifying women's monthly period

HAYA WAKUU KUNYWENI MAJI YA UVUGUVUGU KILA SIKU ASUBUHI MCHANA NA USIKU YANATIBU MARADHI MENGI SANA.

Chanzo.
https://www.jamiiforums.com/jf-doctor/365977-muujiza-ya-matibabu-kwa-maji-ya-moto-kunywa.html
 
Eti yakizidi ni tatizo as kuna aina ya madini inatumika kwa wingi na kuleta madhara mwilini. MziziMkavu naomba ushauri.
 
Last edited by a moderator:
Eti yakizidi ni tatizo as kuna aina ya madini inatumika kwa wingi na kuleta madhara mwilini. MziziMkavu naomba ushauri.
Yako Madini yanayoleta madhara kwa binadamu kwa mfano madini ya Zebaki, uranium na mengine mengi tu.

[h=2]Hatua zichukuliwe kuwanusuru Watanzania na madhara ya zebaki[/h]


Watanzania na madhara ya zebaki

ZIPO taarifa kwamba afya ya Watanzania wanaotegemea samaki wa Viwa Rukwa na mito yake, iko hatarini baada ya utafiti kuonyesha kuwa huenda samaki wa ziwa hilo wana kiwango kikubwa cha zebaki.

Kwa mujibu wa utafiti huo uliofanywa na shirika binafsi linalojishughulisha na utunzaji mazingira (AGENDA), zebaki hiyo imekuwa ikiingia katika mito inayokwenda hadi Ziwa Rukwa baada ya kutumiwa na wachimbaji wadogo wa dhahabu katika Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya.

Kwa vyovyote vile hii ni hatari ikizingatiwa katika sampuli 14 za nywele za wakazi wa maeneo hayo zilizofanyiwa utafiti, theluthi mbili ya sampuli hizo zilionekana kuwa na kiwango kikubwa cha zebaki.

Hatari hiyo inazidishwa na ukweli kuwa zebaki ni madini yanayoleta athari kubwa kwa mwanadamu ikiwa ni pamoja na kuharibu ubongo na figo.

Pamoja na hayo, nyingine ni kuathiri mtoto awapo tumboni kwa mama yake kwa kuharibiwa ubongo, akili kudumaa, upofu, matatizo ya moyo na kupoteza uwezo wa kuzungumza.

Ndiyo sababu ni muhimu serikali ichukue hatua madhubuti na za haraka zenye lengo la kuokoa maisha ya wananchi wanaotumia samaki wa Ziwa Rukwa na mito inayoingia katika ziwa hilo.

Hatua hizo pia ziwe ni pamoja na zinazolenga kuondoa matumizi ya zebaki kwa wachimbaji wadogo katika Wilaya ya Chunya na maeneo mengine nchini yanadhibitiwa na kuondolewa kabisa.

Tunayasema hayo tukitambua kwamba si wachimbaji wadogo wa dhahabu wilayani Chunya tu wanaotumia zebaki katika kutenganisha madini hayo, bali na katika maeneo mengine mbalimbali nchini ambako wananchi hao wanajishughulisha na uchimbaji wa madini hayo.

Hayo ni pamoja na maeneo mbalimbali ya migodi katika Mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Mara, Dodoma na mingine.

Kwa nyakati tofauti viongozi serikali wamekuwa wakizungumzia umuhimu wa kuwawezesha wachimbaji wadogo kutumia njia zisizohatarisha aisha yao na ya wananchi wengine katika shughuli yao hiyo.

Pamoja na mambo mengine, uwezeshaji huo pia utakuwa na lengo la kuhakikisha wanaachana na njia za zamani katika uchimbaji, kama hiyo ya kutumia zebaki.

Hivyo basi, wakati umefika jitihada hizo zizidishwe kuinua kiwango na ubora wa uchumbaji kwa wachimbaji wadogo kuondoa hatari inayowakabili na watanzania wote kwa ujumla.

Bila kufanya hivyo, taifa hili lijiandae kwa maafa makubwa katika miaka ijayo kwa vile karibu maziwa yote na mito nchini itakuwa imekwisha kuenea zebaki. Ieleweke, zebaki ni hatari kwa mwanadamu.

 
Watu walisoma sayansi, biology lakini haiwasaidii. Unakumbuka kitu kinaitwa osmosis. Sasa ukinywa maji mengi kitu kama hiki kinatokea as result utapata cell swelling because of over hydration. Na matokeo yake ni kuwa utapata headache, heart failure, renal failure etc. In normal situation human being anatakiwa kunywa maji 3L per day. Kwa mtu alikuwa debilitated yaani yupo serious hajitambui tunampa iv fluid 3L lakini kwa wewe mzima maji mengi unapata vitu vingi kwa mfano, kwenye ugali, mboga matunda, michuzi, juice, pombe, soda na maji yenyewe. Sasa kwa siku kwa mtu wa kawaida unatakiwa kunywa maji tupu si chini ya 1.5L, ikifika lita mbili siyo mbaya. Kikubwa kwamba ukinywa maji mengi sana unapata brain oedema na matokeo yake utapata kichwa kuuma na wakati mwingine degedege.
Kunywa maji fuata utaratibu huu.
Asubuhi ukiamka kunywa glass moja, kabla ya kuoga kunywa glass moja, kabla ya kula msosi wowote kunywa glass1, kabla ya kulala kunywa glass 1. Ukinywa hivi its enough sana. Merry Christmas and Happy new year. Karibu Songea kwa matibabu safi.
 
[h=1]Madini adui yanayoathiri afya[/h]


Unaweza kufikiri ni hadithi, lakini ukweli ni kwamba watoto wengi wanaozaliwa kijijini Mtakuja Wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, wengi wao wamepinda miguu, kuharibika ubongo na wengine kupata meno yenye rangi ya kahawia.
Tatizo hili limekuwepo kijijini hapo kwa muda mrefu sasa na kukiathiri kijiji hiki kilichopo kilometa 25 kutoka Bomangíombe, Makao Makuu ya Wilaya ya Hai.
Ukubwa wa tatizo
Ni kwa watoto kuzaliwa na vichwa vikubwa, matatizo ya ubongo na wengine ambao miguu yao imepinda.
Sababu kubwa inaelezwa kuwa ni kunywa maji ya visima yenye kiasi kikubwa cha madini aina ya Fluoride.
Mzee Selestine Shayo (67) ambaye ameishi kijiji hapo tangu mwaka 1964, anasema wamekuwa wakinywa maji hayo bila kujali kiwango cha madini hayo.
Anaeleza kuwa maji hayo kimsingi hayafai hata kwa matumizi ya mifugo.
Asia Ramadhan (31) ni mama wa watoto watano, lakini mmoja kati yao, Rajabu Hassan (14) ameathirika, yeye alianza kupinda miguu alipokuwa darasa la tatu mwaka 2009.
ìMwanzo mwanangu alilalamika kuwa mifupa ya miguu inapasuka, ndipo tukampeleka Hospitali ya Mawenzi na baadaye wazungu waliokuja hapa wakatupa dawa, ndipo akapata nafuu kidogo,î anasema.
Anaongeza kuwa baada ya kufanyiwa vipimo na madaktari wakamweleza kuwa mtoto wake amepata matatizo hayo kutokana na maji wanayokunywa kijijini hapo ambayo yana madini mengi aina ya Fluoride.
Mama huyo anamshukuru Mungu kwa kuwa mtoto wake amefaulu mtihani wa darasa la saba mwaka huu katika Shule ya Msingi Mtakuja na kupangiwa Shule ya Sekondari Kia.
ìKutoka hapa hadi Kia ni kilometa sita, ukiongeza zile za kurudi ambazo pia ni sita, mtoto wangu hatoweza kujiunga na masomo ya sekondariÖMifupa ya miguu haitaweza kutembea umbali wote huo,î anasema.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Makao Mapya, Pili Hamisi (56) ni bibi anayemlea mjukuu wake aitwaye Juma Hamza (8) ambaye ni mlemavu wa viungo na ubongo kutokana na matumizi ya maji hayo.
ìBaada ya kuzaliwa, kwa miezi tisa hakukaa wala kuonyesha dalili ya kutambaa, nikampeleka KCMC (Hospitali ya Rufaa), pia Mawenzi ambako madaktari wakaniambia kuwa akifikisha umri wa miaka mitano ataweza kutembea,î anasema.


Anaongeza: "Kweli alipofika umri huo akatembea japo kwa shida, viungo vimelegea na mpaka sasa hajaweza kuongea na wala hawezi kula chakula mwenyewe… yote tunamwachia Mungu."

Mwenyekiti huyo anaeleza kuwa eneo hilo lina karibu watoto 20 ambao wote wamepinda miguu na madaktari walimweleza kuwa kiini cha tatizo hilo ni maji wanayokunywa yana kiwango kikubwa cha Fluoride.

"Wapo waliozaliwa wazima, lakini baada ya miaka michache wakapata tatizo la kupinda miguu na wengine wanakufa. Hata juzi juzi tulizika hapa watoto wawili… kweli inauma," anasema Pili.

Hali katika Shule ya Msingi Mtakuja inashtua kwani watoto wasiopungua 20 wamepinda miguu.

Mwalimu Method Haule anapiga kengele na kuagiza watoto watoke nje ambako kwa hesabu ya haraka, wasiopungua 20 wana matege ya waziwazi.

"Hapa nina watoto kama 20 wamepinda miguu, lakini tatizo ni maji…haya maji ya visima yana Fluoride nyingi sana… naona kuja kwako (mwandishi) utakuwa ukombozi kwetu," anasema.

Wenye vichwa vikubwa hufungiwa ndani hadi kufa

Wenyeji wa kijiji hiki ambao ni wafugaji wa Kimasai na wakulima wa makabila mchanganyiko, wanadokeza kwamba wapo watoto wenye ulemavu ambao wanafichwa.

"Wenzetu (Wamasai) wakipata mtoto mwenye kichwa kikubwa ama aliyepinda miguu, wao husema ni mokii (laana) wanawafungia ndani hawapati huduma mpaka wengine wanakufa," anaeleza Leslie Makundi.

Mkazi mwingine wa kijiji hicho, Christopher Shao, maarufu Kimeta, anasema inahitajika kazi ya ziada kutoa elimu kwa wananchi wa kijiji hicho ili wasiwafungie watoto wao ndani wawapeleke shule.

"Kumficha mtoto si suluhisho kwa sababu hii sio laana kama wanavyofikiri… inatakiwa waonekane ili na Serikali nayo ijue tuna tatizo na inapaswa kuchukua hatua kuokoa wananchi wake," anasema.
Mariana Lyimo ni mhudumu katika zahanati ya Kijiji cha Mtakuja, anasema tatizo la maji kijijini hapo ni kubwa na madhara yake ni makubwa kiafya kwa watoto wanaozaliwa.

"Kuna wakati hapa (zahanati) tuliletewa dawa ya Water Guard (ya kutibu maji) tukaiweka kwenye madumu mengi nakuambia ilikuwa balaa maji yalibadilika rangi yakawa ya njano," anasema.

Abraham Leiyo (18) na Simon Lazaro (28) ni vijana wa Kimasai ambao ni miongoni mwa wengi ambao walipata masaibu ya kupinda miguu miaka michache baada ya kuzaliwa.

Leiyo ambaye alipata ufadhili wa kufanyiwa upasuaji katika Hospitali ya Seliani iliyoko Arusha anasema alianza kupinda miguu alipofikisha umri wa miaka mitatu. "Walikuja madaktari wengi hapa kijijini kwa nyakati tofauti wakatuorodhesha, lakini sikupata matibabu hadi nilipopata ufadhili nikapasuliwa kurekebisha mifupa…natembea vizuri sasa," anasema.



Kauli za wataalamu, wanasayansi

Mtaalamu wa utafiti wa maji aliyewahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi Moshi (Muwsa), Anthony Kasonta anasema ipo mikoa minne nchini yenye kiwango kikubwa cha Fluoride.

"Mikoa yenye matatizo makubwa ya Fluoride ni Kilimanjaro, Arusha, Shinyanga, Mwanza na Mara na unajua kiwango kilichokubalika kwa matumizi ya binadamu kinatakiwa kisizidi nane," anasema.

Hata hivyo, Kasonta anasema katika maeneo mengi ya Hai hasa Mtakuja, kiwango cha madini ya Fluoride katika maji ya visima ni kati ya 9.2 hadi 39 ambacho ni cha juu mno.

Profesa Waitoky Nkya ni mwanasayansi mtafiti aliyewahi kufanya kazi katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC na ile ya Mbeya anasema madini hayo ya Fluoride yana madhara makubwa kwa binadamu.

"Fluoride ina tatizo kwenye mifupa, uti wa mgongo, meno kuwa ya kahawia na hata yanaweza kuleta brain damage (kuathiri mfumo wa ubongo) ni madini yenye madhara kwa binadamu hasa watoto.

Profesa Watoky anasema kwa kawaida mtoto anahitaji madini ya Calcium ili kujenga mifupa lakini wanapokunywa maji yenye Fluoride inakwenda kuathiri mfumo mzima wa kujenga mifupa," anasema. Anasema, matokeo yake watoto wanaweza kuzaliwa wakiwa na matatizo ya ubongo, kupinda miguu ama kuwa na matege na meno kuwa na rangi kama inavyotokea Mtakuja.
Suluhisho la tatizo

Mkurugenzi msaidizi wa Huduma za Ubora wa Maji katika Wizara ya Maji, Philipo Chandy anasema utafiti umeonyesha ipo mikoa ikiwamo ya Kaskazini yenye kiwango cha juu cha Flouride.

"Sisi katika serikali tumeshabaini vijiji vyenye tatizo hili na kuna mikakati ya aina mbili kwanza kuna maeneo yatapata maji ya miradi mikubwa lakini tumebuni teknolojia rahisi ya kuondoa Flouride," anasema.

Anasema wizara ina kituo eneo la Ngurdoto ambacho kimegundua teknolojia ya kutumia mifupa ya ng'ombe katika kuondoa kiwango cha madini ya Fluoride katika maji ya kunywa na kupikia.

Katika kituo hicho, mifupa ya ng'ombe huchomwa kwa joto la digrii 500 halafu mifupa hiyo inasagwa na kupata unga unga ambao ndiyo unaotumika kuchuja maji yenye madini ya Fluoride.

"Hivi sasa tuko mbioni kusambaza teknolojia hii na tumeshampata mkandarasi na tutakuwa na mitambo mikubwa na mitambo ya kaya… Ni teknolojia rahisi na salama," anasisitiza Chandy.

Chandy anasema Serikali imeagiza mtambo mkubwa ambao utatumika kuzalisha mitambo midogo midogo kwa ajili ya kaya ili wananchi waondokane kupata madhara ya madini hayo.

Mpango mahususi kwa Mtakuja

Mkuu wilaya ya Hai, Novatus Makunga anakiri kwamba tatizo la watoto katika Kijiji cha Mtakuja na maeneo jirani kupinda miguu au kuzaliwa na vichwa vikubwa kwa sababu ya maji ni la muda mrefu.

"Ni kweli hicho kijiji maji yake yana kiwango kikubwa cha madini ya Fluoride na ni malalamiko ya muda mrefu na Serikali imesikia kilio cha wananchi na Serikali ni sikivu, " anasema.

"Nataka niwahakikishie wananchi wa Mtakuja kwamba ikifika Juni 30 mwakani hilo tatizo la kupinda miguu au kuzaa watoto wenye vichwa vikubwa litakuwa ni historia kwao," anaongeza.

Anasema katika awamu ya pili ya mradi mkubwa wa maji wa Losaa-Kia, vijiji vinne kikiwamo mtakuja kitanufaika na mradi huo mkubwa utakaogharimu Sh 2.3 bilioni. "Mchakato wa usanifu wa huo mradi umeshakamilika sasa hivi halmashauri iko katika mchakato wa kutangaza zabuni na tayari tumeshapokea Sh600 milioni kutoka Serikali kuu," anasema DC Makunga.
Anasema chini ya mradi huo, maji yatachukuliwa moja kwa moja kutoka kwenye chanzo na ukubwa wa boma la mradi wa maji wa Losaa-Kia utapanuliwa ili ufike Mtakuja na vijiji jirani.cc.@Mamndenyi
Source: Mwananchi



 
Asante kwa kutuelimisha. Merry xmas too!
 
MziziMkavu kaeleza faida tu hajasema kiasi stahili kutumika. Ngoja tumsubiri tena.
Kwa Mtu Mzima au Mgonjwa wa Maradhi yoyote inatakikana awe anakunywa maji Uvuguvugu unapo amka Asubuhi kabla ya

kupiga mswaki unywe Glasi 2 za Maji ya Uvuguvugu na baada ya kupiga Mswaki Unywe glasi 1 na kabla ya kunywa chai unywe

Glasi moja ya maji Uvuguvugu kila siku ufanye hivyo kwa wakati wa asubuhi.


Na Wakati wa mchana Dakika 30 au dakika 45 kabla ya kula chakula cha mchana unywe maji ya Uvuguvugu Glasi 1.

Na Wakati wa chakula cha Usiku unatakiwa unywe Maji ya Uvuguvugu Glasi 2 kabla ya kula chakula cha usiku.

na unywe Maji Ya Uvuguvugu Glasi 1 kabla ya kwenda kulala usiku.
 

Nashukuru sana kwa ushauri mzuri.
 
Wakuu na wataalamu nisaidieni hapo; je, kuna faida gani na hasara zipi za kunywa kiasi hicho cha maji kwa siku.? Nawasilisha.

Madhara yake ni kwamba utakuwa huwezi kuugua kirahisi au utakjuwa hauugui kabisa na pia chances kwamba utaishi miaka 100+ ni kubwa. Mimi siyo daktari lakini naweza kukuhakikishia kuwa hayo ndiyo madhara ya kunywa maji mengi.
 
Madhara yake ni kwamba utakuwa huwezi kuugua kirahisi au utakjuwa hauugui kabisa na pia chances kwamba utaishi miaka 100+ ni kubwa. Mimi siyo daktari lakini naweza kukuhakikishia kuwa hayo ndiyo madhara ya kunywa maji mengi.
.
Aisee...! Niwekee rejea hata moja tu.
 
Nina sixty kg mkuu ninywe kiasi gani kwa uzito huo.?

Kanuni ya kimakisio kwa mahitaji ya maji ni; kunywa nusu ya uzito wako katika aunsi (ounces) ugawe mara mfululizo utakaoufuata kwa siku nzima. Kiasi kidogo chini au juu ya hiki, kinakubalika. Aunsi 1 = miligramu 31.25.

Kanuni ya kimakisio kwa mahitaji ya chumvi ni, Robo tatu gramu za chumvi kwa kila nusu lita ya maji, nusu kijiko cha chakula kwa kila nusu galoni ya maji au kijiko kimoja cha chakula kwa kila galoni moja la maji.

Pengine umeshageuza kichwa na kujisemea, "Wewe ni kichaa…..hicho ni kiasi kingi sana cha maji".

Ukweli ni kuwa, ni rahisi kunywa hivyo hasa tukitumia sentensi, glasi 8 za maji zikigawanywa mara nane kwa siku (glasi 1 = ml 250 au robo lita).

Mfano, kwa mtu mwenye uzito wa kilogramu 75:

Badili kilogramu kwenda aunsi kwa kuzidisha mara 2.2. Hivyo, 75×2.2 = aunsi 165.
Tafuta nusu ya aunsi kwa kugawa aunsi na 2. Hivyo, aunsi 165/2 = aunsi 82.5.
Gawanya mara mfululizo utakaoamua kuufuata kwa siku nzima, mfano mara 8 kwa siku. Kwa hiyo aunsi 82.5/8 = aunsi 10.3.

Badili aunsi kuwa miligramu za maji. Aunsi 1 = miligramu 31.25. Kwa hiyo aunsi 10.3×31.25 = miligramu 322.
Kwa hiyo itampasa mtu huyo mwenye uzito kilo 75, kunywa ml 322 za maji mara nane kwa siku.

Namna anavyopaswa kufuata hiyo ratiba mara 8 kwa siku:

1) Akiamka tu (mfano saa 12 kamili asubuhi), cha kwanza atakunywa maji ml 322. ataendelea na shughuli zake za asubuhi

2) Nusu saa kabla ya chakula cha asubuhi (yaani saa 12:30 asubuhi), atakunywa maji ml 322. atasubiri nusu saa ipite ndipo atapata chakula chake cha asubuhi (itakuwa saa 1 kamili asubuhi).

3) Kisha kula chakula cha asubuhi, atahesabu masaa 2 na nusu ndipo atakunywa tena maji ml 322 (itakuwa saa 3 na nusu asubuhi).

4) Atahesabu masaa 2 tena ndipo atakunywa tena ml 322 nusu saa kabla ya chakula cha mchana (itakuwa saa 6 mchana) kwa hiyo nusu saa baadaye atakula chakula cha mchana (yaani saa 6 na nusu mchana).

5) Atahesabu yapite masaa 2 na nusu baada ya chakula cha mchana ndipo atakunywa tena maji ml 322 (itakuwa saa 9 kamili alasiri).

6) Atahesabu masaa 2 na nusu yapite ndipo atakunywa maji ml 322 nusu saa kabla ya chakula cha jioni (itakuwa saa 11 na nusu jioni). Nusu saa baadaye atakula chakula cha jioni (itakuwa saa 12 kamili jioni).

7) Kisha kula chakula cha jioni, atahesabu masaa 2 na nusu tena ndipo atakunywa tena maji ml 322 (itakuwa saa 2 na nusu usiku).

Muda wowote atakapokwenda kulala kuanzia saa 4 usiku atakunywa tena maji ml 322 kumalizia mara 8 zake kwa siku.

Huyo alikuwa na kilo 75, sasa na wewe andika uzito wako na utumie fomula hiyo hapo juu ujuwe ni kiasi gani cha maji unahitaji kwa siku na kisha ufuate mara hizo 8 kama zilivyopendekezwa hapo juu. Kwa staili hii ndipo maji huwa ni zaidi ya dawa.

Kila mmoja wetu sasa anaweza kutumia uzito wake kwa kutumia fomula hii na kujua ni kiasi gani cha maji anahitaji kwa siku.

Kumbuka, Kunywa maji nusu ya uzito wako katika aunsi ni kiasi cha chini kabisa, lakini mahala pazuri pa kuanzia, ikiwa ni mtu unayejishughurisha zaidi na mazoezi au unaishi katika mazingira ya joto zaidi, utahitaji zaidi ya hapo.

Sasa, hutakubali kuwa kunywa maji kwa protokolo hii ni kazi rahisi?. Endelea nayo hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…