Nakusudia kuitisha maadamano makubwa nchi nzima ili kupinga mgao wa umeme ambao ni wa kutengenezwa ili kuumiza wananchi!!

Nakusudia kuitisha maadamano makubwa nchi nzima ili kupinga mgao wa umeme ambao ni wa kutengenezwa ili kuumiza wananchi!!

Sahihi kabisa....

Suluhisho lilitafutwa kwa kipindi hicho ila iko mitambo mikubwa bado nayo ni chakavu....

Baada ya miezi 6....
 
Jamani naomba mniunge mkono biashara yangu inakufa tra wanataka Kodi yao mwenye frem anataka Kodi yake nayaona maisha yangu yanakufa hivihivi.

Kilichonikatisha tamaa ni kuona serikali imerelax kabisa haina hata wasiwasi. Wanakuja na majibu rahisi mno, eti tusubiri miezi 6!!!

Naomba watanzania kwa umoja wetu tuungane bila kujali vyama vyetu maadamu unaumizwa na suala la kukatikakatika Kwa umeme, tuiambie serikali kwa njia ya maandamano makubwa yasiyo na kikomo mpaka iwashe umeme.

Haiwezekani watu tuliowaajiri watutatulie KERO zetu watupuuze namna hii.

Tuungane kusema noooo!!
Tunataka umeme au ondokeni ofisini.
Siungi mkono ukatikaji wa umeme..
Ila maandamano sio mazuri yatatumiwa vibaya na wale wote wasio kua na nia njema na taifa LETU kutupiga gepu.....
 
Nyie mtaanza asubui mpk jioni...
Wengine tutaanza usiku!
Usiku...
Usiku wa manane
 
Unaweza kuwa na points ila acha kuwa brainwashed kuwa mgao ni wa kutengeneza

Shirikisha akili yako ukiambiwa kitu. Hakuna mtu anaweza tengeneza mgao wa umeme nchi nzima.
Hili ttz la mgao lilikuwepo enzi za Magufuli?
 
Nchi ya kisenge hii, hayo maandamano hayatakamilika sisi wafu ni wafu, hatusikii maumivu kabisa, linalotokea si ni hewala tu,inasikitisha.
 
Walipokuwa wanafanya service ikawa inawalazimu kuzima baadhi ya mitambo ili kuifanyia service wananchi tukalalamika sababu ilipelekea umeme kupungua baada ya uzimwaji wa hizo mashine, tukapata kiongozi mmoja anaecheza na jukwaa akaamuru hakuna kufanya service ili umeme usikatike na ikawa hivyo.

Sasa mitambo bila service nadhani hata wewe unajua kinachoenda kutokea. Imeharibika zaidi na inataka service kubwa zaidi bahati mbaya kiongozi wa sasa haamini kwenye kucheza na majukwaa kaamua kuruhusu service kunusuru mitambo ni lazima kuwe na upungufu wa umeme.

Tatizo la kimsingi ni kuwa tunazalisha umeme mdogo kuliko matumizi yetu na bahati mbaya yanaongezeka kila siku. Ingalikuwa tuna vyanzo vingi vya kuzalisha umeme basi hata kuzimwa kwa mtambo mmoja au 2 ili ifanyiwe service kusingekuwa na impact kubwa Sana kwenye upatikanaji wa umeme.

Kwa Hali ilivyo sasa hata umlete Malaika au Nani sijui awe MD wa Tanesco tutaendelea kupata mgao. Subiri masika Ije mabwawa yajae kuwe na umeme mwingi maisha yaendelee
HUNA AKILI TIMAMU
 
Unaweza kujiuliza wazee wa zamani waliwezaje kuanza harakati za kudai Uhuru hadi wakafanikiwa?

Courage walipata wapi?

Uthubutu walipata wapi?

Ikumbukwe haikuwa rahisi tena kwa Mamlaka za Mzungu?!

Lakini waliweza [emoji123]

Wasomi wakati ule walikuwa wachache wa kuhesabika.

Leo hii wasomi wengi ingawa wengine fake.

Exposure Kama zote.

Technolojia iko juu ,

Lakini ndio imekuwa kinyume kabisa ! [emoji848][emoji848]

Tatizo ni nini?
 
Wanaume wakula chips chai rojo na mahindi ya kuchoma kwa chumvi hawawezi kuwa na uthubutu wa mambo mazito [emoji123]
 
Back
Top Bottom