Nalaani Mbunge Condester Michael kutolewa ndani ya Bunge kisa Mavazi, ameonewa na kudhalilishwa kwa makusudi

Achague tu kama anataka kuvaa atakavyo akaungane na watanzania wengine walioko baa wakisaka tonge.
vinginevyo bungeni siyo sehemu ya kwenda kusaka wachumba.
 
Huyu mzee Hussein Nassor Amar aliyemchongea huyu Dada ni mpuuuzi. Kwanza alikua anaangalia nini hadi kaona hilo. Pili nguo ya kawaida kabisa hiyo huyu mzee ana matatizo aseme kama katoswa sio kusingizia mavazi ya kubana.
 
Mwomba mwongozo kaona hiyo ndiyo hoja ya uwakilishi wa wananchi wa Momba?

Hili ndilo ametumwa na wapiga kura wake?
Hapo kawatetea wanyonge?

Alikosa namna bora ya kulimaliza/kumrekebisha nje ya kamera ili kutumia muda huu adhimu kwa manufaa mapana ya taifa.
 
Babu mihemko atakuwa, yaleee ya Makonda kutuhumu watu ushoga badala ya kufanya kazi za Jiji
 
Akina mama ni watu wanaopenda mitindo, sasa hawa wazee wajifunze hulka za kina mama au ndo ile kutaka kuleta maadili ya kidini kuvaa hijab mjengoni.
 
Chizi. Huyo mzee Ni Nani?
 
Huyo mzee babu kajilipua, kama bwai bwai tu[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Huyu babu useless kabisa , suruali ni vazi la staha kabisa kwa mwanamke , huyu babu kala maharage ya wapi sijui , nashauri wanawake wa jimbo lake wote wasimpe kura 2025 kamdhalilisha dada wa watu
 
U
Ni mzee,ana mtazamo wa 1950 huko
Unajua hawa wazee wa zamani ukiunganisha na 'mifumo dume' ni kaaazi kwelikweli... nakumbuka enzi zile hata Waziri mkuu mwendazake Rashid Kawawa,aliwahi agiza mgambo kutembea na nikasikia na kufanya operation ya kuwasaka na kuwachukulia hatua wale wanawake wote waliovaa nguo fupi mitaani..... ilikuwa patashika wakati ule wa siku za siasa ya Ujamaa...... Anyway kazi iendelee.
 
Maneno ya nyerere yanaanza kuonekana bungeni. ( Zambi ya ubaguzi .) Walianza kubagua wagombea kwa kuangalia chama chao tu. Sasa mungu anaanza kuwaonyeshea matunda ya umimi. R.I.p nyerere.
 
Tuwekee kwanza dressing code ya bungeni..
 
Labda supika alitupa ndoana ikateleza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…