WanaJF,
Pamoja na kuwa sitaki kuingilia mjadala katika hatua hii, naomba kuthibitisha kuwa:
I) Katibu Mkuu wa Chadema, kwa mujibu wa Katiba na Kanuni ya Chadema, ndiyo mhimili mkuu na mwenye jukumu la kutunza na kuhakikisha Katiba ya Chama inatunzwa.
2) Nataka kuwahakikishia wanachadema wote, kuwa nilikuwepo nimekuwa ndani ya Chadema kuanzia 1998 ambapo nilikuwa Makamu Mwenyekiti Bara, na baadaye 2003 Kaimu Katibu Mkuu, na hatimaye Katibu Mkuu. Hivyo nimeshiriki kikamilifu kuandaa Katiba ya 2004 na pia Katiba ya 2006 baada ya Rebranding ya Chama. Nataka niwahakikishie wanachadema, hakuna toleo lolote la Katiba ndani ya Chadema imeweka " muda wa Uongozi kuwa vipindi viwili tu", kuanzia Katiba aliyoiasisi Mzee Mtei na kupitishwa na Mkutano Mkuu, wala si ya 2004 au ya 2006. Kama kuna mtu anasema ilikuwepo na imeondolewa kinyemela, basi aonyeshe kifungu hicho kwenye Katiba yeyote ile, au miniti za kikao chochote kile.
3. Mimi Dr Slaa, ndiye niliyewasilisha Miniti za Mkutano Mkuu wa 2006 kwa Msajili ikiambatana na Katiba iliyopitishwa na Mkutano Mkuu. Tulichobishana Mimi na Msajili, na kwa maandishi, ni kuwa Msajili alit aka nimwasilishie nakala ya Katiba kwa Kiingereza. Nilimkatalia kwa msingi kuwa Katiba yetu ilipitishwa na Mkutano Mkuu kwa kiswahili na Mkutano Mkuu na hivyo siwezi Mimi kumpelekea kwa Kiingereza. Msajili alidai kuwa ni hitaji la kisheria. Nilimjibu kuwa sheria hiyo inapaswa kufanyiwa marekebisho. Hata hivyo, baadaye tulikubaliana kuwa nitengeneze " literal translation" lakini kwa mahitaji ya kisheria itatumika Katiba ya Kiswahili ambayo ndiyo iliyopitishwa na Mkutano Mkuu. Hivyo, ninathibitisha kuwa hakuna kipengele chochote kilichoingizwa kinyemela.
Wanachadema, wapenzi, na wananchi kwa ujumla, huo ndio ukweli. Kama mtu anadhani kuna utata aende kwa Msajili akague Katiba ya 1992, 2004 na 2006, nadhani utaratibu wa Msajili itaruhusu ukaguzi huo. Ndio njia pekee ya kuacha kabuni na kuwa watabiri kwa misingi ya waganga wa kienyeji. Tufanye kaki kisayansi, na tusiwatie hofu wananchi bila sababu.
Kama mtu Ana ajenda yake ya siri, huyo hatuwezi kumsaidia! Wananchi, tuna mambo ya muhimu zaidi kuliko hizi propaganda, tunahitaji kutumia muda wetu kwa mambo hayo, mathalan madai ya Katiba Mpya, kupigania maslahi ya Taifa na Watanzania hasa walala hoi ambao kila siku wanazidi kupigika, kupambana na manyanyaso Kama yaliyotokea Serengeti na Babati ambao wananchi wameteswa viajabu katika nchi inayojitangaza kuwa na utawala wa sheria nk.