Huyo mleta mada mwenyewe anawateka akili. Bila shaka ni chawa kama alivyo Etwege na the like.
Msigwa amejibu vizuri sana, halafu huyu analeta taarifa za uwongo.
Mwana habari makini huuliza swali likiwa limejengwa katika msingi. Ukomo wa uongozi kwa kiongozi yeyote unaelezwa kwenye katiba. Kama unauliza tu kutokea hewani unaonekana ni mwanahabari kanjanja.
Huyo mwanahabari wa Clouds angekuwa na weledi, angemwuliza Msigwa kama ana mpango wa kugombea nafasi ya Umwenyekiti kwenye uchaguzi ujao (kwa sababu katiba ya CHADEMA inamruhusu mwanachama yeyote mwenye sifa kugombea nafasi hiyo). Au angeweza kumwuliza Mbowe, kama ana mpango wa kugombea tena (kwa sababu katiba ya CHADEMA haina kipengere kinachomzuia mwenyekiti wa sasa kugombea tena, akitaka).
Lakini kutokana na ujinga, mwulizaji swali ameuliza swali lisilo sahihi kwa mtu asiye sahihi. Msigwa siyo Mbowe, anamwuliza swali linalomhusu Mbowe.