Nalaani suala la Sizya wa Clouds kuuliza ukomo wa Uenyekiti wa Mbowe

MSAGA SUMU

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2015
Posts
6,661
Reaction score
21,656
Huyu mtangazaji wa Clouds anatumiwa na CCM kwa maslahi ya nani? Yuko laivu mida hii halafu anamuuliza mchungaji Msigwa "the forbidden question "

Jamaa amemuuliza Msigwa eti ni lini Mbowe ataachia nafasi ya Uenyekiti? Kwa kifupi Msigwa alishindwa kabisa kulijibu swali hili zaidi ya kuruka ruka.

Mimi Kama Chadema nalaani Sana swali hili, na sitaki liulizwe tena na mtu mwingine.
 
Kwanini Msigwa ashindwe kujibu swali rahisi kama hilo?

Mbowe alishasema ataachia madaraka this year, sioni ugumu wa hilo swali, na hata muuliza swali anaonekana anatembea na maswali ya kukariri kwenye kazi yake, ndio maana Mkapa aliwaita kanjanja.
 
Demokrasia unayoipigania ni ipi sasa kama swali dogo tu kama hilo unafura na unalaani
Hawa ni chawa wanaoishi kupitia mfuko wa Mbowe. Kwahiyo wanahofu ikiwa Mbowe ataachia chama leo au kesho ni nani atakaewalisha?

Wapo wengi tu na hili wala halishangazi.
 
Mtangazaji kabla ya kuuliza angalau aingie mtandaoni na kujiridhisha na katiba ya CHADEMA. Swali linakuwa la kichawa chawa kunguni kunguni kama hataki kurejea miongozo!
 
Hicho chama alikianzisha baba mkwe wa Mbowe, hatutakiachia kirahisi, Bora tukivunje kuliko kukiachia. Tutakivuruga kama NCCR au CUF, zidisheni kelele ndio mtajua hamjui, pale Kuna Hela zetu, jasho letu, na damu yetu, it is our family project
 
Usilaaani bali mwombee adui yako aishi siku nyingi ili unapofanikiwa ajionee kwa macho yake mawili.
 
Huyo mleta mada mwenyewe anawateka akili. Bila shaka ni chawa kama alivyo Etwege na the like.

Msigwa amejibu vizuri sana, halafu huyu analeta taarifa za uwongo.

Mwana habari makini huuliza swali likiwa limejengwa katika msingi. Ukomo wa uongozi kwa kiongozi yeyote unaelezwa kwenye katiba. Kama unauliza tu kutokea hewani unaonekana ni mwanahabari kanjanja.

Huyo mwanahabari wa Clouds angekuwa na weledi, angemwuliza Msigwa kama ana mpango wa kugombea nafasi ya Umwenyekiti kwenye uchaguzi ujao (kwa sababu katiba ya CHADEMA inamruhusu mwanachama yeyote mwenye sifa kugombea nafasi hiyo). Au angeweza kumwuliza Mbowe, kama ana mpango wa kugombea tena (kwa sababu katiba ya CHADEMA haina kipengere kinachomzuia mwenyekiti wa sasa kugombea tena, akitaka).

Lakini kutokana na ujinga, mwulizaji swali ameuliza swali lisilo sahihi kwa mtu asiye sahihi. Msigwa siyo Mbowe, anamwuliza swali linalomhusu Mbowe.
 
Mbowe yuko pale kikatiba..Wanachadema ndio waliomchagua kuwaongoza Hadi hapo tutakaposema basi baba pumzika.

Ni kwanini CCM wanaumia sana kumuona mbowe mwenyekiti? Na kwa taarifa yenu akipumzika tunawaletea chuma zaidi. Kwa akili zenu kwa sababu mmeshindwa kumnunua mnataka awekwe mtakayemmudu? Chadema mmegonga mwamba aisee..

Nanyi CCM ni lini mtafanya uchaguzi wa haki kumpata mwenyekiti? Maana kusema kweli hamjawahi kufanya uchaguzi kwenye hiyo nafasi zaidi ya maigizo pale Dodoma.
 
Wanataka wamuue wapumue
 
Sawa kabisa tumekusikia kuhusu waandishi na media kuuliza the forbidden questions, ila pia ukae ukijua the forbidden fruit is the sweetest!.

Nakumbuka ukizungumzia ukomo wa uongozi Chadema ni kama unatangaza vita!, angalia nilichojibiwa na Dr. Slaa nilipoulizia hili https://www.jamiiforums.com/threads...kithibitishwa-chadema-inaweza-kufutwa.543947/
P
 
Sizya ana haki ya kuhoji " freedom of speech" lakini pia msigwa ana wajibu wa kujibu kama kiongozi.

sasa mimi kama mimi sijaona kama Sizya katumiwa na Ccm ni swala la kuacha ushabiki na kutazama ukweli tu
 
Mtangazaji mjinga hajuwi mtu amechaguliwa kwa katiba na si kujipa cheo?Afanye yanayomhusu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…