Nalalamikiwa, nimfanyie nini mpenzi wangu zaidi ya haya?

Nalalamikiwa, nimfanyie nini mpenzi wangu zaidi ya haya?

Evelyn Salt

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2012
Posts
70,916
Reaction score
141,437
Mbwa mzee kujifunza mbinu mpya hili nalo tatizo tena tatizo kubwa.

Huwa naona real men The Boss akiwa among wanasema mwanaume anahitaji mambo matatu: food, sex and space.

Katika hayo mambo kwakweli am doing the best inawezekana kabisa nina mapungufu yangu ila am doing the best kwakweli, food, napika japo sio bonge moja la mpishi kama farkhina but I cook tena delicious ones, sex hii si kuwa tu ni wajibu ila ni hobby yangu kitu ikiwa hobby kifuatacho itv ni known kabisa, space hapa kidogo pananishinda japo najitahidi ila sio kwa fungulia doggy, anaechungwa ni mbuzi kwa binadamu tunafanya kukaba tu japo kukaba kwenyewe ni kulinda bahari ila hivo hivo tu almradi kuna kibao "Punguza mwendo kazi inaendelea mbele" tunapunguziana speed natoa space kwa kiasi Chake may be majukumu yakinizidi itakua zaidi ya hapo.

Apart from hivo vitatu nafanya na mengineyo mengi napika mwenyewe simuachii dada wa kazi, mezani naweka mwenyewe kumake sure kila kitu kipo sawa, nguo nasaidiwa kufua ila boxa nafua mwenyewe, nanyoosha mwenyewe, asubuhi naanda maji ya moto napeleka bafuni (bafu halina heater) muda huo nshaweka nguo za kazini standby na viatu nimebrush kabisa mara chache naandaa Chai sio kila siku kwasababu ni mvivu kula BADILI TABIA bila shaka unanishangaa sana make haya mambo hautajagi ha ha ha nishangae tu ukinishangaa nami na kushangaa.

Swala la heshima na kujali nikijifanyia assessment najiona nina 99%,i do respect him much, much kwakweli nikijilinganisha na ndugu, jamaa na rafiki am the best, naweza kuwavisit katikati ya maongezi mara wachambane na waume zao mara wawafokee kitu ambacho mi huwa nashangaa unawezaje kumchamba mmeo au kumfokea mbele za watu mmh sijawahi na sitakaa nithubutu nikikereka nangoja tukiwa wawili nikiona nachelewa kutoa dukuduku naandika meseji.

Kuna shost angu alishawahi kunitembelea akaishia kunishangaa inakuaje nanyoosha nguo za baby dady yeye wanaishi wote ila hajawahi kumfulia wala kumnyooshea nikamshangaa pia na kuzidi kujiona am the best mie ni "mwanamke" hizi huduma nazionaga kwa wamana watu wazima ndo wanawalea waume zao ila mie kwa age yangu tu hii najiona nipo kama mama lowasa ha ha .

Point yangu what else should I do? Pamoja na kujiona mwanamke, najiona kama mama Lowassa ila bado nalalamikiwa jamani wanaume zaidi ya haya kunakuna yapi tena?au ni human nature tu kwamba hatunaga kuridhika? Au kunanii?
 
jitahidi kumfanyia vitu vingine tofauti ambavyo hujamzoesha kumfanyia
 
For me your doing your best. Swala ninaloliona hapa ni kuwa human needs never end. mtu kama alikua anakunywa chai ya rangi na kiporo siku ukimpa chai ya maziwa na mkate atafurah ila atafika mahali atadai huweki siagi.
 
For me your doing your best. Swala ninaloliona hapa ni kuwa human needs never end. mtu kama alikua anakunywa chai ya rangi na kiporo siku ukimpa chai ya maziwa na mkate atafurah ila atafika mahali atadai huweki siagi.

Ha ha ha mmh kumbe huenda hakuna shida ila tu nature yetu binadamu kuridhika kwetu ni msamiati
 
Mpaka hapo umejitahidi sanaaa makofi kwako dada..........lakini binadamu unaweza kujitahidi lakini still akaona bado,lakini kama tulivyo binadamu hatukosi mapungufu na inabidi tusameheyane lakini mpaka hapo umejitahidi sanaaa....
 
Daah gelofriend wangu ni bonge la wife material jamani. Ngoja kwanza gelofriend, unaweza ukataja baadhi ya mambo unayolalamikiwa?

Teh gelofriend bila shaka hata ye ukimuuliza anaweza kua hajui may be nikupe kamfano kadunchu jana mchana mida ya kula nimemnawisha mikono nikampakulia akaanza kula mara kidume cha mbegu kinazunguka pale (our son) nikamchukua kumlisha daddy kamaliza kula mie namlisha mtoto akaanza kunawa mwenyewe eeh nkashangaa analalamika kuwa anajinawisha mwenyewe simhudumii au nlitakiwa nimuache kidume cha mbegu nimnawishe? Maisha ni magumu mweh.... Kuna vitu vidunchu ila vinaumizaga kichwa unaweza hata usilale unakiwaza tu japo kidogo
 
Mpeti peti tuu...men tunapenda kubembelezwa kama watoto...kuna raha yake
 
Mpaka hapo umejitahidi sanaaa makofi kwako dada..........lakini binadamu unaweza kujitahidi lakini still akaona bado,lakini kama tulivyo binadamu hatukosi mapungufu na inabidi tusameheyane lakini mpaka hapo umejitahidi sanaaa....

Duh sasa kama hapa am doing nothing natakiwa kuishi vipi labda???
 
For me your doing your best. Swala ninaloliona hapa ni kuwa human needs never end. mtu kama alikua anakunywa chai ya rangi na kiporo siku ukimpa chai ya maziwa na mkate atafurah ila atafika mahali atadai huweki siagi.
ha ha hahaaaaaaa
 
hadi hapo wewe binamu yangu ni wife material....endelea lawama haziishii siwajua wengine sisi tuna element za ubaba saleh...
 
Analalamika nin? Hajawah sema ni kitu gan hayupo satisfied?
Pamoja na kufanya yote pia wanapenda sana kubembelezwa na kupetiwa.
Though sometimes hawa viumbe bana hawatabiriki, utafanya vyote na bado hataona effort yako na hapo ndipo wanaponichosha jaman
 
Teh gelofriend bila shaka hata ye ukimuuliza anaweza kua hajui may be nikupe kamfano kadunchu jana mchana mida ya kula nimemnawisha mikono nikampakulia akaanza kula mara kidume cha mbegu kinazunguka pale (our son) nikamchukua kumlisha daddy kamaliza kula mie namlisha mtoto akaanza kunawa mwenyewe eeh nkashangaa analalamika kuwa anajinawisha mwenyewe simhudumii au nlitakiwa nimuache kidume cha mbegu nimnawishe? Maisha ni magumu mweh

Gelofriend unanishangaza ujue afu unaniinspire, kwa age yako ujue unafanya mambo amazing sana. Kumnawisha mume mikono mwee, hata hao mama zetu ni wachache wanafanya hivyo. Nahisi umemdekeza sana shem darlin, kiasi kwamba ukisahau tu kumfanyia ka kitu anaona kama humjali vile. Anataka attention yako 100% na ndicho ambacho umemzoesha miaka yote hii. Ingawa sasa hivi ka junior kapo, lazima kuna attention ihamie kwake. Mfanye asijihisi kuwa anacompete attention yako na junior. Utanisamehe kama ntakukwaza but nahisi shem anahisi labda umehamishia mapenzi kwa junior, otherwise asingecomplain kuwa hujamnawisha while anaona unamlisha juju.

Gelofriend unajua kupalilia ndoa wallahi loooooooh
 
evelynchumvi unafanya wanayofanya mama zetu jambo ambalo ni nadra kwa ndoa za vijana wa sasa labda tu kutoridhika kibinadamu pole yako cha muhimu ni uvumilivu
 
For me your doing your best. Swala ninaloliona hapa ni kuwa human needs never end. mtu kama alikua anakunywa chai ya rangi na kiporo siku ukimpa chai ya maziwa na mkate atafurah ila atafika mahali atadai huweki siagi.

Hahhaha uwiiiii
 
Back
Top Bottom