Nalalamikiwa, nimfanyie nini mpenzi wangu zaidi ya haya?

Nalalamikiwa, nimfanyie nini mpenzi wangu zaidi ya haya?

unaweza ukawa unafanya vingi sana lakini kuna vidogo ambavyo hugusi na ndo vinaugusa mtima wake

USHAURI:ZUNGUMZA NA MWENZIO kuhusu nini umfanyie

Si bora angekua anasema sasa kwamba do this do this ye walaaa analalamika tu hunihudumii Uuuh sijui nkapige ramli nijue
 
Gelofriend unanishangaza ujue afu unaniinspire, kwa age yako ujue unafanya mambo amazing sana. Kumnawisha mume mikono mwee, hata hao mama zetu ni wachache wanafanya hivyo. Nahisi umemdekeza sana shem darlin, kiasi kwamba ukisahau tu kumfanyia ka kitu anaona kama humjali vile. Anataka attention yako 100% na ndicho ambacho umemzoesha miaka yote hii. Ingawa sasa hivi ka junior kapo, lazima kuna attention ihamie kwake. Mfanye asijihisi kuwa anacompete attention yako na junior. Utanisamehe kama ntakukwaza but nahisi shem anahisi labda umehamishia mapenzi kwa junior, otherwise asingecomplain kuwa hujamnawisha while anaona unamlisha juju.

Gelofriend unajua kupalilia ndoa wallahi loooooooh
Yani huwezi amini wala mtoto hajahamisha upendo kwakweli mi najiona ni yule yule, nipo kama zamani
 
evelynchumvi unafanya wanayofanya mama zetu jambo ambalo ni nadra kwa ndoa za vijana wa sasa labda tu kutoridhika kibinadamu pole yako cha muhimu ni uvumilivu

Mmmh huu uvumilivu huu mmmh
 
Kuna wanaume wanapenda kufanyiwa zaidi ya watoto. Mkishakuwa na mtoto lazima mume nae ajiongeze coz tayari mke ana jukumu la kulea mtoto (kwa % kubwa). The best thing ni kuongea nae ili kujua wapi anakwazika.
Pamoja na kuwa na mtoto huduma zangu kwa baba ake zipo pale pale kinachonikera ndo hicho nnachokifanya hakionekani wala
 
Yani huwezi amini wala mtoto hajahamisha upendo kwakweli mi najiona ni yule yule, nipo kama zamani
Sasa analalamika nini tena jamani. Na huko kulalamika ni tangu kwenye uchumba au kaanza lini? Ni bora mtu aseme tatizo ni A, B, C utajua ujirekebishe vipi. Hakuna kitu kinaumiza kama mtu unajitahidi kufanya kila unachoweza ili mwenzio afurahi, but yeye haridhiki wala kuappreciate. Ni kazi sana kumridhisha binadamu asiye na moyo wa kuridhika. Gelofriend labda tumuombee
 
Pamoja na yote Evelyn Salt, shemeji anapaswa afunguke.....nini ambacho amemiss. Anapokulalamikia tu bila kuwa wazi hamjitendei haki. Wewe sio mfalme njozi ujue palipopungua.

Pia na yeye ana wajibu wa kukusaidia malezi.
Wanaume wakumbuke hata wao sio wakamilifu ila wake zao wanayakubali yake mapungufu. Na haswa kama una mtoto mdogo jamani shemeji aelewe na kuvumilia.
 
Last edited by a moderator:
Pamoja na kuwa na mtoto huduma zangu kwa baba ake zipo pale pale kinachonikera ndo hicho nnachokifanya hakionekani wala

Shemeji ajifunze ku- appreciate juhudi zako aisee... kama uliyoyaandije ndiyo hali halisi unajituma sana. Hebu zungumzeni mvunje ukimya
 
Mwanaume Mwenye Uhitaji na Uthamini wa Hisia katika kupenda Haangalii kipi unakifanya kwake hata kama wewe utaona ndio utendaji wako wa mwisho.. Mwanaume anahitaji Zaidi ya Chukula, mapenzi na Kufuliwa. Heshima tu haiwezi kukufanya uwe mke bora Ikiwa kuna Vidogovidogo ambayo humfanyii au Huvifanyii.. Cha kufanya ni kuwa Huru kwake kwa kuwa tayari ni Mtu wako.. Muulize kipi unachokosea kwake ukiona Hana Jibu jaribu kumbadilishia mazingira ya Kimchezo kwa kutoka nje ya nyumba kwenda kwenye hoteli au lodg na kama siku ukipata nafasi na utulivu hata kama ni bafuni au jikoni unaweza kumaliza nae kwa kuwa kila kitendo kigeni utakachomfanyia kitapunguza lile gubu lako.. mwanaume ni Zaidi ya chakula, heshima na kufuliwa Ubunifu ni wajibu wako dada
 
Evelyn Salt unasema unalalamikiwa lakini hujaeleza ni nini hasa unacholalamikiwa. Pengine ungesema unalalamikiwa nini maybe ningejua namna ya kukusaidia.
 
Last edited by a moderator:
Wala hakuna risk. Wakipeana space, watajua kama wanastahili kuwa pamoja, ama na watu wengine. They could all be right, but not right for each other.
Paulo jamani, space Watu wapo kwenye ndoa? Mie bf tu aniambie mambo ya space kwa kweli bora anisahau tu.

Hawa watu wanahitajiana sana, pamoja na malalamiko yote haya, gelofriend still anamuhitaji mumewe ujue, vivyo hivyo na shemeji. Ndo maana ES anajitahidi kutafuta mzizi wa tatizo lilipo ili wasolve waendelee kuenjoy paradiso yao. Kupeana space ingekuwa sawa kama wangekuwa wamechokana labda. Ili mtu ukajipange upya urudi kuwa kama the girl he fell In love with miaka hiyoo. ES is still the Es he fell in love with miaka hiyo, ndo maana haelewi tatizo ni nini. Hata wakipeana hiyo space ( sishauri kabisa) still watarudiana tu afu hayo malalamiko yatakuwepo tu vile vile

Labda kikubwa zaidi, waongee tu kwa nukta. Shem aelezee anataka awe treated vipi labda. Inawezekana shem hana tu ile roho ya kuridhika. Sasa shughuli itabaki kwa ES kuamua if anaweza akavumilia tu hiyo weakness ya mwenzie au atajua mwenyewe abebe vipi hilo jaribu lake. Ndo mumewe huyo na Inawezekana pungufu lake ni hilo tu, kwengine kote yupo mwaaaaah
 
kumtoa out, kumsindikiza asubui anapokwenda kazini kumfanyia suprise unampikia chakula akipendacho unampelekea kazini just like that and much more

Namsindikizaje kazini wakati namie ni mfanya kazi? Mi sio mama wa nyumbani....
Hapo kwenye chakula akipendacho wala hanaga labda suprise ya bia ndo itamfurahisha food sio priority kwake
 
Anapokuwa analalamika anakuwa serious au yupo kawaida.Yawezekana analalamika kiutani but hamaanishi ili kukufanya usijisahau sana hasa katika hiki kipindi ambacho mna mtoto.Nnachomaanisha usibase kwa mtoto kiasi yeye umsahau.Hongera mana unajitahidi sana aisee

Wala mtoto hajabadili kitu kila mtu anapata anachostahili kabisa tena kwa mapenzi yote yupo serious sio joke
 
Gelofr hizi nyingine hapa nafanya kuassume tu so usikwazike mwaya
1.Kauli zako je especially ukiwa na hasira? Inawezekana ukawa huwezi kumfokea mbele za watu lakini huku ndani humkwepeshi ( maana gelofriend una tumajibu amazing) " kiboro dinda wee" nk

Afu hapo kwenye space, maana sijasahau kama huwa unakaba hadi notifications teh. Huyo ni mumeo learn to trust him unless kuna Vitu anakuwa anafanya ambavyo huvielewi elewi. Hakuna privacy kati yenu lakini usimkabe hadi ikawa kero, Mpe kauhuru kidogo. Honestly hata mimi sipendi mtu ambaye ananikagua 24/7, nahisi kama siaminiki vile.

Umehisi shem ana tumawasiliano na mtu mwingine huko. Please thibitisha kwanza afu deal kwanza na shem alone (nakuaminia kwa katimbwili amazing), asipoelewa basi ndo msake huyo binti umpe "grand warning". Lakini umekuta tu text ushaanza kumchamba mdada, utakuja kumistake hata na ndugu zake. Inaaibisha muda mwingine
Ha ha ha gelofriend umenifanya nicheke hapo Kweli kukaba lol, hata nikiwa na hasira aisee najitahidi kucontrol ulimi huwa simjibu vibaya sijui kaniloga teh zaidi zaidi naishia kunyamaza na kulia
 
Ha ha ha gelofriend umenifanya nicheke hapo Kweli kukaba lol, hata nikiwa na hasira aisee najitahidi kucontrol ulimi huwa simjibu vibaya sijui kaniloga teh zaidi zaidi naishia kunyamaza na kulia
Hahaha maana niliwazapo na hapo teh. Hivi kumbe team kulia lia tupo wengi mwee
 
Back
Top Bottom