Nimesoma nikarudia nikasoma. Sasaaa... dah! ndoa naipenda lakini iko kama itanipita jameni. Una mtoto mdogo, unapata muda wa kupika (sasa sijui ni kila siku?) na chakula unapeleka mezani wewe, unamnawisha mume, mtoto nae anakungoja umlishe, umesema unapasi, unapeleka maji bafuni, unamuandalia nguo, viatu....
Nimetafakariii nikajiangalia ili mimi niweze kuwahi kazini kwa kujihudumia mwenyewe naamka saa 11. Nikihamia nje kidogo ya jiji kuamka itakuwa saa 10. Sasa nikianza kumhudumia na mtoto mkubwa hadi kusafisha viatu si ndio nitaamka saa 9? Kazi za mwajiri ufanye kama mtumwa, urudi home ukiwahi sana saa 12 uvae apron uingie jikoni....kuna viwatu vya kukaguliwa au kusaidiwa homework... sijui nini.... ukimaliza hapo useme ukaoge ujitupe kitandani mwenzio yeye ana nguvu zote wewe mgongo unalia kama vijiti vikavu..
Kama sitapata mume anayeweza kujitegemea kwa mambo na sina hela za kununua mashine za nyumbani (kama heater, mashine za kufulia, sinki la kunawia dining...) itabidi nichague kuwa hausiwaifu tu na sijui kama niko tayari maana nilishagundua siko kwenye kundi la superwomen.
Unajua ni rahisi sana kusema mume anahitaji kufanyiwa kama mtoto lakini mnasahau kuwa watoto wana rewards za kutia moyo. Kwanza unajua hajiwezi kwa hiyo unajiskia raha kumsaidia mtu asiyejiweza. Unaweka na bidii ili kumwelekeza aweze kujitegemea; ukimhudumia hana matusi wala dharau. Wakati mwingine hawaridhiki na unachowapa, wanweza kukulilia hadi ukatamani kuhama nyumba lakini unawavumilia kwa kuwa hawajui chochote kuhusu hela wala mipango. Wanatulilia tu kama sisi tunavyomlilia Mungu. Unaweza kumnunulia nguo ya laki halafu we moyoni unajiskia raha kweli ulivyogharamia gauni halafu unakuta amelivaa anachezea mchanga ila ukimnunulia pipi au chama anashukuru mpaka anakubusu!! Halafu mapenzi yao hayana masharti. Mnakosana, baada ya dk chache anakufata kujaribu kurudisha uhusiano. Vimbwanga vyote atakavyofanya unajua anafanya kwa sababu mtoto. Haya, mtu mzima analinganishwaje na mtoto? Na mtu mzima wa kike yeye ni mtu mzima tu toka utotoni hadi uzeeni?