Nalalamikiwa, nimfanyie nini mpenzi wangu zaidi ya haya?

Sijakuelewa kiukweli, he is 30s I am 20s hebu rudia tena sasa nikuelewe

naamini wewe ni progressive woman, halafu kijana mwenye uelewa, kwanini umuoshe mwanaume mikono...sidhani kama kizazi hiki mnafanya hivyo. mie nimeona wanaofanya hivyo ni wazee mbao kwasasa wapo 70+
 
Heee we vepe kununiana kuna raha mwisho wa mnuno ni nini kama sio kugegedana?

aisee Nimekushindwa hakika.. Kumbe inawezekana jamaa anakuchokoza makusudi ili mwisho wa mnuno apate mgegedano uliotukuka maana staili ya mnuno huwa inamshindo katika mpatano. Nimewaza tu
 
Nimesoma nikarudia nikasoma. Sasaaa... dah! ndoa naipenda lakini iko kama itanipita jameni. Una mtoto mdogo, unapata muda wa kupika (sasa sijui ni kila siku?) na chakula unapeleka mezani wewe, unamnawisha mume, mtoto nae anakungoja umlishe, umesema unapasi, unapeleka maji bafuni, unamuandalia nguo, viatu....

Nimetafakariii nikajiangalia ili mimi niweze kuwahi kazini kwa kujihudumia mwenyewe naamka saa 11. Nikihamia nje kidogo ya jiji kuamka itakuwa saa 10. Sasa nikianza kumhudumia na mtoto mkubwa hadi kusafisha viatu si ndio nitaamka saa 9? Kazi za mwajiri ufanye kama mtumwa, urudi home ukiwahi sana saa 12 uvae apron uingie jikoni....kuna viwatu vya kukaguliwa au kusaidiwa homework... sijui nini.... ukimaliza hapo useme ukaoge ujitupe kitandani mwenzio yeye ana nguvu zote wewe mgongo unalia kama vijiti vikavu..

Kama sitapata mume anayeweza kujitegemea kwa mambo na sina hela za kununua mashine za nyumbani (kama heater, mashine za kufulia, sinki la kunawia dining...) itabidi nichague kuwa hausiwaifu tu na sijui kama niko tayari maana nilishagundua siko kwenye kundi la superwomen.

Unajua ni rahisi sana kusema mume anahitaji kufanyiwa kama mtoto lakini mnasahau kuwa watoto wana rewards za kutia moyo. Kwanza unajua hajiwezi kwa hiyo unajiskia raha kumsaidia mtu asiyejiweza. Unaweka na bidii ili kumwelekeza aweze kujitegemea; ukimhudumia hana matusi wala dharau. Wakati mwingine hawaridhiki na unachowapa, wanweza kukulilia hadi ukatamani kuhama nyumba lakini unawavumilia kwa kuwa hawajui chochote kuhusu hela wala mipango. Wanatulilia tu kama sisi tunavyomlilia Mungu. Unaweza kumnunulia nguo ya laki halafu we moyoni unajiskia raha kweli ulivyogharamia gauni halafu unakuta amelivaa anachezea mchanga ila ukimnunulia pipi au chama anashukuru mpaka anakubusu!! Halafu mapenzi yao hayana masharti. Mnakosana, baada ya dk chache anakufata kujaribu kurudisha uhusiano. Vimbwanga vyote atakavyofanya unajua anafanya kwa sababu mtoto. Haya, mtu mzima analinganishwaje na mtoto? Na mtu mzima wa kike yeye ni mtu mzima tu toka utotoni hadi uzeeni?

Mimi naomba wanawake wanaoweza kufanya kama huyu Evelyn Salt wajitokeze niwape zawadi......Huyo mumewe kiboko,hadi kunawishwa mikono??!!!
 
Last edited by a moderator:

Take it easy life is not fair anyway. You should know that by now!
 
Kaka angu hapa kama vile nmeanza kupata picha halisi sasa, katika kulalamika nikimuuliza hana sababu ya msingi, pia ni first born.... Kuna vitu umeongea hapa vina ka ukweli fulani Oooh so natakiwa tu kuona ndivo alivo ehuuuuuu atleast hata nmejua pa kuanzia ubarikiwe bro angu
Nilikuwa nasubiri jibu la huyo ndugu. am ur young bro. unavowalaumu wanaume au mme wako the same wapo wanaume nao wanalalamika kama alivyo mume wako. issue ya kutoridhika,ugomvi au ulalamishi mara nyingi huwa ni tabia ya mtu na niki refer chat yako na Heaven Sent hapo juu kwamba ulikuwa unalia kama wahindi probably huyo bro hajaanza leo na shida ya tabia even when ur wrong and u disturb others mara nyingi wewe unajiona upo sahihi na unastahili kuwa hivyo kumbe sio. kujua tatizo ni nusu ya ushindi katika kulikabili. nimewahi ku experience hii kwa msichana tuliachana. sasa wewe tafuta busara na hekima zaidi bila kuathiri ndoa yako ungekuwa hujaolewa ningesema quit that uhusiano
 
Last edited by a moderator:
Relax, take a back seat and enjoy the view. kama unachosema ni sahihi hayo mambo ya kawaida kabisa. Hata wewe kuna vitu unalalamika ni ubinadamu tu, vitu vingine vidogo vidogo kama hivi haviwezi kukosekana vinginevyo labda useme ulitegemea "a perfect relationship"!. By the way ngoja nikuchekeshe kuna mdada yeye akimuandaa mume asubuhi jamaa anazingua ile mbaya utasikia hiyo nguo sitaki nipe ile au hata kuchagua mwenyewe wakati mwingine, sasa siku akiachwa achague pia anasema, "mke wangu wewe ndiyo mamaa hebu nichagulie viwalo bwana" yaani alimradi ni ubinadamu tu.

Ha ha ha ha eti wewe ndio mama lol
Sasa kama yeye ndo mama mbona haridhiki, binadamu hatujui kuridhika
 
Mbwa mzee kujifunza mbinu mpya hili nalo tatizo tena tatizo kubwa.

Huwa naona real men The Boss akiwa among wanasema mwanaume anahitaji mambo matatu: food, sex and space.

Katika hayo mambo kwakweli am doing the best inawezekana kabisa nina mapungufu yangu ila am doing the best kwakweli, food, napika japo sio bonge moja la mpishi kama farkhina but I cook tena delicious ones, sex hii si kuwa tu ni wajibu ila ni hobby yangu kitu ikiwa hobby kifuatacho itv ni known kabisa, space hapa kidogo pananishinda japo najitahidi ila sio kwa fungulia doggy, anaechungwa ni mbuzi kwa binadamu tunafanya kukaba tu japo kukaba kwenyewe ni kulinda bahari ila hivo hivo tu almradi kuna kibao "Punguza mwendo kazi inaendelea mbele" tunapunguziana speed natoa space kwa kiasi Chake may be majukumu yakinizidi itakua zaidi ya hapo.

Apart from hivo vitatu nafanya na mengineyo mengi napika mwenyewe simuachii dada wa kazi, mezani naweka mwenyewe kumake sure kila kitu kipo sawa, nguo nasaidiwa kufua ila boxa nafua mwenyewe, nanyoosha mwenyewe, asubuhi naanda maji ya moto napeleka bafuni (bafu halina heater) muda huo nshaweka nguo za kazini standby na viatu nimebrush kabisa mara chache naandaa Chai sio kila siku kwasababu ni mvivu kula BADILI TABIA bila shaka unanishangaa sana make haya mambo hautajagi ha ha ha nishangae tu ukinishangaa nami na kushangaa.

Swala la heshima na kujali nikijifanyia assessment najiona nina 99%,i do respect him much, much kwakweli nikijilinganisha na ndugu, jamaa na rafiki am the best, naweza kuwavisit katikati ya maongezi mara wachambane na waume zao mara wawafokee kitu ambacho mi huwa nashangaa unawezaje kumchamba mmeo au kumfokea mbele za watu mmh sijawahi na sitakaa nithubutu nikikereka nangoja tukiwa wawili nikiona nachelewa kutoa dukuduku naandika meseji.

Kuna shost angu alishawahi kunitembelea akaishia kunishangaa inakuaje nanyoosha nguo za baby dady yeye wanaishi wote ila hajawahi kumfulia wala kumnyooshea nikamshangaa pia na kuzidi kujiona am the best mie ni "mwanamke" hizi huduma nazionaga kwa wamana watu wazima ndo wanawalea waume zao ila mie kwa age yangu tu hii najiona nipo kama mama lowasa ha ha .

Point yangu what else should I do? Pamoja na kujiona mwanamke, najiona kama mama Lowassa ila bado nalalamikiwa jamani wanaume zaidi ya haya kunakuna yapi tena?au ni human nature tu kwamba hatunaga kuridhika? Au kunanii?

Kweli binadamu tumetofautiana sana ...mimi siku ikitokea nimefanyiwa haya makeke huwa nashangaa kabisa manake sijazoea kabisa na nimeshakubali yaishe.... tumeishi hivyo miaka 12+ now!
 
Dada Evelyn unaweza ukaandika lalamiko lake hasa ili tupate kujua hayo matatu upo safii sana ila unahitaji mawili zaidi (1) muwe mnatoka kwenda sehemu kama beach na kuongea yanayo kukwaza moyoni juu ya mumeo (2) unahitaji uwe mwenye kuleta matani pia jaribu kuhave fun na mwezio kwani furaha huletwa na wawili wakijuwana, kuchekeshana na kuvumiliana.
 
Kweli binadamu tumetofautiana sana ...mimi siku ikitokea nimefanyiwa haya makeke huwa nashangaa kabisa manake sijazoea kabisa na nimeshakubali yaishe.... tumeishi hivyo miaka 12+ now!

Ha ha ha eeh haya bana
 
naamini wewe ni progressive woman, halafu kijana mwenye uelewa, kwanini umuoshe mwanaume mikono...sidhani kama kizazi hiki mnafanya hivyo. mie nimeona wanaofanya hivyo ni wazee mbao kwasasa wapo 70+

namnawishisha mikono muda wote wa kula kama nipo around....wajibu
 
mke wangu mwenyewe anafanya hivyo ila siku nyingine nakuwaga na mihasira tu, na hujui yametoka wapi hasa hasa mifuko ikitoboka, network inakuwa ina-search kwa kasi ya ajabu ili kuziba mifuko, msamehe bure ndo hivyo tena pengine mihasara ya kazini anaingia nayo hadi ndani ya nyumba badala ya kuiacha mlangoni
 
Kama we unafanyiwa hivo ni halali yako kuona kawaida
Sasa Eve wewe kama ni mtanzania wa kawaida unataka kuniambia mke kumnawisha mume ni ishu nayo?!! Acheni utani bana hayo mambo ya kawaida sana kwenye jamii za kitanzania labda kama mnaongelea jamii ya hapo kwa jaluo mtaa wa pili.
 
Unampa too much attention ndio maana haishi kulalama. Do your part with all your heart basi vingine mwachie yeye ahangaike navyo. Kuna watu wana gubu wewe na ukiendekeza atataka hadi umtafunie na kumlisha kila siku. Biandamu hatuko perfect na kama yeye anaona mapungufu au wewe ni jukumu lake kama mpenzio/mumeo/mkeo kukwambia darling hapa naona kuna kitu kinapelea from there you can talk ila mtu wa gubu mara hiki alalame mara hiki anune mhh huyo abebeki. Siku kausha tu maana ameshaona weakness yako ni kuogopa akilalamika . MAisha haya utaishi kwa kuguess kuwa sijui nifanye nini kipya asilalamike? utaweza? Mapenzi ni pamoja na uwazi na kuongea sio kumtegeshea mwenzio akosee ndio utoe malalamiko hayo hayatakuwa mapenzi bali utumwa.
 
Back
Top Bottom