Nalalamikiwa, nimfanyie nini mpenzi wangu zaidi ya haya?

Nalalamikiwa, nimfanyie nini mpenzi wangu zaidi ya haya?

Ongeza surprise...na ubunifu... Kwenye 6x6 uko uwe porn star kabisaaa...leo mpake nutella, kesho mpake asali ...Lainisha kauli..., mpe attention, bembelezaaaa.. Endelea kuwa Mama Lowassa, mume atakuganda kama wino wa NEC. 

Nutella na asali.....interesting....
 
Teh gelofriend bila shaka hata ye ukimuuliza anaweza kua hajui may be nikupe kamfano kadunchu jana mchana mida ya kula nimemnawisha mikono nikampakulia akaanza kula mara kidume cha mbegu kinazunguka pale (our son) nikamchukua kumlisha daddy kamaliza kula mie namlisha mtoto akaanza kunawa mwenyewe eeh nkashangaa analalamika kuwa anajinawisha mwenyewe simhudumii au nlitakiwa nimuache kidume cha mbegu nimnawishe? Maisha ni magumu mweh.... Kuna vitu vidunchu ila vinaumizaga kichwa unaweza hata usilale unakiwaza tu japo kidogo
Relax, take a back seat and enjoy the view. kama unachosema ni sahihi hayo mambo ya kawaida kabisa. Hata wewe kuna vitu unalalamika ni ubinadamu tu, vitu vingine vidogo vidogo kama hivi haviwezi kukosekana vinginevyo labda useme ulitegemea "a perfect relationship"!. By the way ngoja nikuchekeshe kuna mdada yeye akimuandaa mume asubuhi jamaa anazingua ile mbaya utasikia hiyo nguo sitaki nipe ile au hata kuchagua mwenyewe wakati mwingine, sasa siku akiachwa achague pia anasema, "mke wangu wewe ndiyo mamaa hebu nichagulie viwalo bwana" yaani alimradi ni ubinadamu tu.
 
Ha ha ha mme na mtoto wangu wote ni wa muhimu sana kwangu ila mmh mme ana special treatment zake, anapata mapenzi ya mke mwanangu nae anapata mapenzi ya mama....kuoga tunaoga wote karibu kila siku hata kama tumechuniana bafuni tunaenda wote hivo hivo kimya kimya

Ni kwa nini mchuniane? hilo linalofanya mchuniane huenda likawa sehemu ya malalamiko yake,rekebisha kama linarekebishika wakati ukiendelea kutafiti kiini cha malalamiko yake.Kuhusu simu jitahidi kuiepuka wakati uko na mumeo,hata kama utaona kuwa yeye yuko nayo busy, Jizoeshe kumshukuru kwa kila anachofanya kizuri na uombe msamaha pale unapokosea,asante mume wangu,nisamehe mume wangu yaweke kwenye matumizi ya maneno yako ya kila siku. Usioneshe hasira zako waziwazi mbele yake pindi akikuudhi,na usiongelee jambo au kuandika msg ukiwa na hasira,mwanaume hapendi kukaripiwa,subiri hasira zishuke kwanza. Nakuombea ulivuke hili salama,Nami nimepitia kipindi kama hiki ila mwisho wa siku niligundua tatizo nikasolve.
 
Tubarikiwe sote sist, nimefurahi kama umepata japo ujumbe wa kuutuliza moyo wako... Usibadilishe hayo uyatendayo kwani lawama zitazaa ugomvi. Keep it up nadhani unakumbuka ushauri wangu kwa Mr
Nakumbuka, ahsante pia
 
Basi atakuwa ni dictator.....maana hawezi kuwa yupo busy na simu yake halafu wewe kuwa busy ionekane ni kosa! Eti anapiga stori na washkaji, stori zenyewe ni zile ambazo haupo na uelewa nazo halafu unaamua kujifariji kwa kutumia katelephone halafu anakubana...kweli huyu analojambo! But kila jambo lina mlango...maana kaa ukijua kuwa shida sio shida ila njia utakayoitumia kutatua shinda ndio shida yenyewe.
Kwakweli kwenye swala la simu naona udikteta wa wazi wazi
 
Sikutegemea Kma Hili Lingekua Tatizo Kwako, Then Umejuaje Kma Kwel Upo Vizur Mambo Uliyoyataja?? Alafu Naona Kma Sumtime Huwa Unajisahau Kwa Kuona Kuwa Unamfanyia Mambo Mengi Tofaut Na Wanawake Wengne...So Ni Kma Kuna Muda Unalegeza. Mfano Mimi Hivyo Vitu Nilikua Nafanyiwa Nikiwa Chuo Kwa Upande Wako Unaona Unamfanyia Mambo Makubwa Sanaa Wakat Upande Mwingne Ni Ya Kawaida Sanaaa Kwa Wapenzj Wanaopendana Real...Stor Yako Inaonyesha Kma Saikolojia Yako Inakudanganya That Unafanya Mambo Makubwa But Bado Haridhiki!! Kuna Muda Huwa Unajisahau Kwa Advantage Ya Hayo Unayomfanyia Ukiyaona Ni Ya Kipekee. Unachotakiwa Ni Kubuni Vingine Vizur Zaidiiii. Na Wale Usiseme Wengne Hawafny Hiv Mimi Nafanya!! Na Inaonekana Umemzoesha So Unapositisha Kimojawapo Anahisi Kma Umebadilika. Ongeza Manjonjo Bwana Aujafika Mwisho Ndio Kwanza[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] !!

It's not about psychology, nlichoongea ni mambo ya kawaida majukumu ya mwanamke ndani ya nyumba..... OK hayo ulifanyiwa chuo ulipo graduate unafanyiwa yapi?
 
Mie nadhani sio rahisi kumridhisha mtu yeyote yule, let alone a man. huwezi jua what is enough kwa mtu huyo mpaka uje useme hadharani kwamba umempa vya kutosha. hivi ukija kumsikia anawaambia watu pembeni kwamba hujui kupika, au una mapungufu kitandani...utasemaje...Mie nadhani hakikisha jipe first priority kwanza...just be you fanya mambo ndani ya uwezo wako...sex kwa wanaume ni psych...kufanya different styles au kila kona hizo ni adventures tu na men tunapenda games. lakini sio guarantee ya sex satisfaction...madada wengine mpaka anafikia kusema nimempa hadi kinyume lakini simuelewi huyu kaka...nafikiri just be you, fanya kazi kwa bidii kuwa successful woman, ujenge heshima yako , mheshimu, msikilize....
Pia jambo kubwa wewe una handle vipi mikwaruzano ndani ya nyumba, you should handle them calmly.... nina imagine mama Hillary Clinton ali handle vipi aliposikia mumewe anatembea na monica lewinsky....
 
Sijasoma maoni yote ya wadau so naweza kuwa narudia waliyoshauri wengine...

kuna kitu kimoja ambacho nakiona ni muhimu sana wanawake wakijue..
'do not change yourself to please him'

usibadilishe 'personality' yako saaana just tu kumfurahisha mume..

atashindwa 'kukusoma'.......na mtashindwa kujenga bond na compatibility inayotakiwa

Sasa labda kama unayoyafanya yoote 'yamekubadili' personality...
alijua ana mwanamke 'chui' ndani..na wewe umeanza ku act kama 'swala'
hizo complains zinakuja sababu ya 'kukosekana' kwa 'the real you'

Sometimes huwa unakuwa na mtu na still unam miss.......
watu hupenda 'the good and bad side' za mtu...

Wala sijachange kitu chochote naishi maisha ya Kweli kabisa, tena tulivokua tumekutana naona ndo I was faking kujifanya siongei, najifanya sister Maria....tulivozoeana nikaanza kuishi maisha halisi with true colors kupika, kufua n.k nilianza tangu anaishi geto, good thing ananijua in and out kama vile kaniumba yeye lol
 
It's not about psychology, nlichoongea ni mambo ya kawaida majukumu ya mwanamke ndani ya nyumba..... OK hayo ulifanyiwa chuo ulipo graduate unafanyiwa yapi?
Ni Mambo Ya Kawaida Sawa, Ila Ww Unaona Umemaliza Kila Kitu Kiasi Kwamba Unasema Unamfanyia Kila Kitu Lakin Bado Haridhiki!! Mean Umemaliza Kila Linalostahil Yy Kufanyiwa Lakin Haridhiki!!!
 
Sidhani kama ni kweli hii stori, kwa level ya uelewa wako na character. Ungekua mshamba ningekubali au kabila fulani hivi sawa na mumeo. au kaka huyo ni mshamba fulani hivi una mkaanga na kumlia timing. BTW sijatumia neno ushamba kama kukutukana.
Hata age difference.....huyo kaka labda yeye 75 wewe below 35 bado sidhani kama unafanya hivyo....labda wewe uwe mkubwa sana kwa mwanaume like 50+ huyo kaka below 30.....otherwise nimeyameona haya kwa mama yangu mkubwa...yeye na mumewe 71 kwa 75 respectively.
Sijakuelewa kiukweli, he is 30s I am 20s hebu rudia tena sasa nikuelewe
 
Ongeza surprise...na ubunifu... Kwenye 6x6 uko uwe porn star kabisaaa...leo mpake nutella, kesho mpake asali 😂😂...Lainisha kauli..., mpe attention, bembelezaaaa.. Endelea kuwa Mama Lowassa, mume atakuganda kama wino wa NEC. 👏👏

Mmmh jamani huko kwenye sita kwa sita nshasema ni hobby.... Anyway haya bana
 
Evelyn Salt mpendwa umenisupriz..Sikujua kama unajua kupetipeti hivi...
Huyo mume umeshamlemaza kwa mahaba..Cha msingi jaribu kufanyia kazi malalamiko yake kama yako ndani ya uwezo wako

Na ukiona kitu anacholalamika hakina msingi wowote usimzarau wala kukaa kimya..Jaribu kumuelewesha kwa upole..Hope yale maneno yako ya hapa jamvini huyatumii huko ndoani
Ha ha ha maneno yapi
 
Last edited by a moderator:
Ubandidu huleta u sexy fulani
unafanya mtu anakuwa addicted na real you ambayo haipati kwa mwingine
na ile hofu ya kukupoteza inajitokeza...but ukiwa mama theresa unakuwa so predictable..
mtu anajiuliza why huyu ana act hivi?au kuna dhambi anaifanya?au yuko desperate kuwa na mimi?
au ni kimeo hiki kinajilazimisha kwangu? but ukiwa real you....ile sexiness inamvuta kila mtu...
'ndo mnaajaziana kila kwenye mapungufu' kila mtu anaziba ya mwenzie....

Nawaz tu......labda bibie anampenda sana mwanaume ........kwa hiyo anajitahidi kufanya kila awezalo kuonyesha upendo wake!!!!!!!
 
Nawaz tu......labda bibie anampenda sana mwanaume ........kwa hiyo anajitahidi kufanya kila awezalo kuonyesha upendo wake!!!!!!!

Inawezekana...tukipenda huwa tunabadilika...
love is blind but the neighbors can see
 
Ha ha ha gelofriend bado tu kutoa michicha ndani ya friji tuingie sie
Hahahha ingieni tu afu junior aje awafungie na funguo. Ila kila kitu kina mwisho wake gelofriend, vumilia tu huku ukiendelea kumuombea. Ndo mumeo, ndo udhaifu wake huo na Inawezekana huo ndo mzigo wake unaotakiwa kumbebea. Ila wewe mtoto ni mbayaaaa jamani hahahhaa
 
Nimesoma nikarudia nikasoma. Sasaaa... dah! ndoa naipenda lakini iko kama itanipita jameni. Una mtoto mdogo, unapata muda wa kupika (sasa sijui ni kila siku?) na chakula unapeleka mezani wewe, unamnawisha mume, mtoto nae anakungoja umlishe, umesema unapasi, unapeleka maji bafuni, unamuandalia nguo, viatu....

Nimetafakariii nikajiangalia ili mimi niweze kuwahi kazini kwa kujihudumia mwenyewe naamka saa 11. Nikihamia nje kidogo ya jiji kuamka itakuwa saa 10. Sasa nikianza kumhudumia na mtoto mkubwa hadi kusafisha viatu si ndio nitaamka saa 9? Kazi za mwajiri ufanye kama mtumwa, urudi home ukiwahi sana saa 12 uvae apron uingie jikoni....kuna viwatu vya kukaguliwa au kusaidiwa homework... sijui nini.... ukimaliza hapo useme ukaoge ujitupe kitandani mwenzio yeye ana nguvu zote wewe mgongo unalia kama vijiti vikavu..

Kama sitapata mume anayeweza kujitegemea kwa mambo na sina hela za kununua mashine za nyumbani (kama heater, mashine za kufulia, sinki la kunawia dining...) itabidi nichague kuwa hausiwaifu tu na sijui kama niko tayari maana nilishagundua siko kwenye kundi la superwomen.

Unajua ni rahisi sana kusema mume anahitaji kufanyiwa kama mtoto lakini mnasahau kuwa watoto wana rewards za kutia moyo. Kwanza unajua hajiwezi kwa hiyo unajiskia raha kumsaidia mtu asiyejiweza. Unaweka na bidii ili kumwelekeza aweze kujitegemea; ukimhudumia hana matusi wala dharau. Wakati mwingine hawaridhiki na unachowapa, wanweza kukulilia hadi ukatamani kuhama nyumba lakini unawavumilia kwa kuwa hawajui chochote kuhusu hela wala mipango. Wanatulilia tu kama sisi tunavyomlilia Mungu. Unaweza kumnunulia nguo ya laki halafu we moyoni unajiskia raha kweli ulivyogharamia gauni halafu unakuta amelivaa anachezea mchanga ila ukimnunulia pipi au chama anashukuru mpaka anakubusu!! Halafu mapenzi yao hayana masharti. Mnakosana, baada ya dk chache anakufata kujaribu kurudisha uhusiano. Vimbwanga vyote atakavyofanya unajua anafanya kwa sababu mtoto. Haya, mtu mzima analinganishwaje na mtoto? Na mtu mzima wa kike yeye ni mtu mzima tu toka utotoni hadi uzeeni?
 
Back
Top Bottom