Evelyn Salt
JF-Expert Member
- Jan 5, 2012
- 70,916
- 141,437
- Thread starter
-
- #341
Sasa dada kauli kama hii ndo inanichanganya. Sasa kama unajua ni majukumu na wajibu wako unalalamika nini? Umesahau kawaida hujenga sheria na hakuna excuse ya kuvunja sheria? Just be you. We shukuru tu kuwa hata unapika, unaweka mezani na kinaliwa. Wapo wenzio humu wameenda mpaka shule za mapishi lakini waume hawakamatiki. Vyakula vinawekwa mezani, mume anaingia home saa 7 usiku au harudi kabisa na siku akiwahi anakitoa kasoro halafu anaenda kulala. Jifunze kuhesabu baraka, hayo mengine potezea. Malaika utampata wapi?
That's my gelofriend.....Tatizo naloliona si kwamba anamlazimisha kumshukuru, tatizo ni kwamba kwa nini analalamika wakati mtu anajitahidi kutimiza majukumu yake yote na zaidi? It's better hata kama angekuwa hasemi Ahsante ila tu asilalamike. Analalamikia kitu gani? Ndo swali hapo
Teh labda huduma ya cheka bombastic. Ila yana mwisho wake gelofriend, Mungu ni mwemaThat's my gelofriend.....
Addition kidunchu ni sawa kuambiwa pale nnapokuwa sijawajibika ipasavyo but niambiwe sasa "kuwa sijafanya hiki nilitakiwa nifanye na hiki, au nimefanya hiki ila sivo ilitakiwa kiwe hivi" that's very okay na ndio nataka ila sio tu kupewa neno kavu "hunihudumii" huduma ipi sasa jamani mpesa au luku ha ha ha ncheke kama mazuri
Teh labda huduma ya cheka bombastic. Ila yana mwisho wake gelofriend, Mungu ni mwema
Mwe mwe mwe mweeeeeh!! Basi mie itabidi nipelekwe the heg kabisaaaaaa!
Teh Kisa?
Mwe mwe mwe mweeeeeh!! Basi mie itabidi nipelekwe the heg kabisaaaaaa!
bora wewew the hague,kuna wanaotakiwa kunyongwa kabisa teh teh
Yaani sijafikia hata robo ya ufanyayo, sasa kama wafanya yote hayo na bado ukalalamikiwa mie si ndio basi tena!
Kwanini usifanye? Mbona ni majukumu yako mwanamke
Jukumu langu ni kuzaa tu, na ktk hilo niko vizuri.
mada imepita muda lakini ndo nimepata leo muda wa kurudi. Swali lako limenikumbusha kitu nilichojifunza kwenye mahusiano yangu na mtoto. Katika kuwa mama kuna wakati nilikuwa nikiona kitu kizuri kwangu nakinunua wakati mwingine kwa gharama kubwa nampeleka mtoto nikitarajia naye atakiona ni kizuri na atafurahi sana. Mara nyingi alikuwa hafurahi kiasi cha kuweza kutuliza kiherehere cha moyo wangu. Anasema asante, anaipeleka chumbani anaendelea na mambo yake. Basi napata huzuni au nanung'unika kwamba hajali jinsi nilivyojinyima ili kumpatia kile kitu. Unamnunulia nguo bei kubwa unakuta yeye anapenda kuivaa anapoenda kucheza, na ile uliyomnunulia elfu 3 kwa ajili ya kuchezea yeye ndo anaipenda sana na anataka aivae karibia kwenye kila tukio analolithamini.
Mtoto huyo huyo ninayenung'unika kuwa hathamini mahangaiko yangu nikimnunulia pipi, popcorn, rangi za kuchorea au kumpeleka matembezi anafurahi sana na anashukuru sana . Kuna wakati nikajiuliza hivi huyu ana kichaa au? With time nikajifunza kuna mambo tunawafanyia wapendwa wetu kwa ajili yetu, na kuna tunayowafanyia kwa ajili yao. Kumnunulia nguo laki 1 badala ya elfu 20 ni mapenzi yangu na kiherehere changu binafsi - nataka apendeze, najiskia fahari mimi mwenyewe kuona bidii yangu kwenye mwili wake lakini hawajibiki kuninyenyekea na kunishukuru saaana. Ile "tenda wema uende zako" inaingia hapa. Nitende wema kwa ajili ya wema. Nikitaka kumfurahisha, nasema leo nataka nimfurahishe mtoto basi nachagua nimfanyie nini katika yale mambo ambayo with time nimegundua yanamfurahisha, mfano, kumpikia chakula anachopenda sana, kumnunulia tu pipi au choklet anayopenda au kumpeleka kwenye maeneo ya mitoko ya watoto anayoyapenda. Kama hii kanuni inafanya kazi kwa mtoto basi hata kwa watu wazima inafanya kazi hivyo hivyo kwani mtoto ndo picha halisi ya binadamu.
Teh gelofriend bila shaka hata ye ukimuuliza anaweza kua hajui may be nikupe kamfano kadunchu jana mchana mida ya kula nimemnawisha mikono nikampakulia akaanza kula mara kidume cha mbegu kinazunguka pale (our son) nikamchukua kumlisha daddy kamaliza kula mie namlisha mtoto akaanza kunawa mwenyewe eeh nkashangaa analalamika kuwa anajinawisha mwenyewe simhudumii au nlitakiwa nimuache kidume cha mbegu nimnawishe? Maisha ni magumu mweh.... Kuna vitu vidunchu ila vinaumizaga kichwa unaweza hata usilale unakiwaza tu japo kidogo
Gelofriend unanishangaza ujue afu unaniinspire, kwa age yako ujue unafanya mambo amazing sana. Kumnawisha mume mikono mwee, hata hao mama zetu ni wachache wanafanya hivyo. Nahisi umemdekeza sana shem darlin, kiasi kwamba ukisahau tu kumfanyia ka kitu anaona kama humjali vile. Anataka attention yako 100% na ndicho ambacho umemzoesha miaka yote hii. Ingawa sasa hivi ka junior kapo, lazima kuna attention ihamie kwake. Mfanye asijihisi kuwa anacompete attention yako na junior. Utanisamehe kama ntakukwaza but nahisi shem anahisi labda umehamishia mapenzi kwa junior, otherwise asingecomplain kuwa hujamnawisha while anaona unamlisha juju.
Gelofriend unajua kupalilia ndoa wallahi loooooooh
Kumbe ni hayo?
Sidhani kama ataacha kulalamika kwani anafanyiwa zaidi ya mfalme. Kwani mahari alitoa ng'ombe wangapi?
in short that's too much na atakulalamikia milele!
Babu jamani mmmh
Umeset viwango ambavyo vitakutesa maisha yako yote.