mada imepita muda lakini ndo nimepata leo muda wa kurudi. Swali lako limenikumbusha kitu nilichojifunza kwenye mahusiano yangu na mtoto. Katika kuwa mama kuna wakati nilikuwa nikiona kitu kizuri kwangu nakinunua wakati mwingine kwa gharama kubwa nampeleka mtoto nikitarajia naye atakiona ni kizuri na atafurahi sana. Mara nyingi alikuwa hafurahi kiasi cha kuweza kutuliza kiherehere cha moyo wangu. Anasema asante, anaipeleka chumbani anaendelea na mambo yake. Basi napata huzuni au nanung'unika kwamba hajali jinsi nilivyojinyima ili kumpatia kile kitu. Unamnunulia nguo bei kubwa unakuta yeye anapenda kuivaa anapoenda kucheza, na ile uliyomnunulia elfu 3 kwa ajili ya kuchezea yeye ndo anaipenda sana na anataka aivae karibia kwenye kila tukio analolithamini.
Mtoto huyo huyo ninayenung'unika kuwa hathamini mahangaiko yangu nikimnunulia pipi, popcorn, rangi za kuchorea au kumpeleka matembezi anafurahi sana na anashukuru sana . Kuna wakati nikajiuliza hivi huyu ana kichaa au? With time nikajifunza kuna mambo tunawafanyia wapendwa wetu kwa ajili yetu, na kuna tunayowafanyia kwa ajili yao. Kumnunulia nguo laki 1 badala ya elfu 20 ni mapenzi yangu na kiherehere changu binafsi - nataka apendeze, najiskia fahari mimi mwenyewe kuona bidii yangu kwenye mwili wake lakini hawajibiki kuninyenyekea na kunishukuru saaana. Ile "tenda wema uende zako" inaingia hapa. Nitende wema kwa ajili ya wema. Nikitaka kumfurahisha, nasema leo nataka nimfurahishe mtoto basi nachagua nimfanyie nini katika yale mambo ambayo with time nimegundua yanamfurahisha, mfano, kumpikia chakula anachopenda sana, kumnunulia tu pipi au choklet anayopenda au kumpeleka kwenye maeneo ya mitoko ya watoto anayoyapenda. Kama hii kanuni inafanya kazi kwa mtoto basi hata kwa watu wazima inafanya kazi hivyo hivyo kwani mtoto ndo picha halisi ya binadamu.