Nalima mchicha mara ya tatu unakataa

king kunta j

Senior Member
Joined
Jul 21, 2021
Posts
124
Reaction score
85
Wanajukwaa sielewi najitaidi mara ya tatu kila nikilima unakataa mwenye utaalamu anisaidie
 
Unakataa vipi kiongozi..unakataa kuota.unadumaa.au unakomaa haraka..fafanua wadau wakusaidie
 
udongo sio piga tuta changanya huo udongo na mbolea ya ng'ombe piga maji
 
Wanajukwaa sielewi najitaidi mara ya tatu kila nikilima unakataa mwenye utaalamu anisaidie
sasa kwa haya maelezo unategemea msaada gani? Hebu eleza kama mtu unayehitaji msaada.
 
sasa kwa haya maelezo unategemea msaada gani? Hebu eleza kama mtu unayehitaji msaada.
Ni kwamba mara 3 nimelima mchicha mara ya kwanza ulidumaa na nilipojaribu mara ya nyingine ikakomaa mapema
 
Ni kwamba mara 3 nimelima mchicha mara ya kwanza ulidumaa na nilipojaribu mara ya nyingine ikakomaa mapema
bado siwezi kukusaidia kwa maelezo haya. Lakini jaribu kununua mbegu kutoka kwenye duka lolote la kilimo. Tengeneza matutu yako vizuri kisha panda mbegu zako vizuri na funikia kwa nyasi kavu matuta yako. Baada ya hapo hakikisha una mwagilia maji kila siku ya Mungu asubuhi kabla ya jua kuchomoza na jioni pia. Endelea kumwagilizia hadi utakapoanza kuvuna. Unaweza kutumia mbolea ya dukani NPK UREA Kwa ajil ya kukuzia mchicha wako wiki moja baada ya mchicha wako kuota.Angalizo mchicha ukiota tu toa nyasi zote kwenye matuta ulizofunikia hapo mwanzo.
 
Lima shamba lako Lima tifutifu weka samadi ya ngombe au kuku tandaza tifuatifua tena mwagia maji shamba lote acha kwa siku saba then panda mchicha utakuja niambia
 
Sijui kwanini umesema maelezo yangu hayatoshi ila mimi nimekuelewa na nitafanyia kazi na nilikuwa naogopa sana matumizi ya mbolea ya dukani..barikiwa sana
 
Wanajukwaa sielewi najitaidi mara ya tatu kila nikilima unakataa mwenye utaalamu anisaidie
Jitafakari vyema kama je unatumia akili zako vizuri?
Mchicha unakushinda mahindi je?
Umeshjndwa hata kuingia Google jamani kweli?

Kumbuka mafanikio yanaanza na juhudi zako mwenyewe binafsi
 
Jitafakari vyema kama je unatumia akili zako vizuri?
Mchicha unakushinda mahindi je?
Umeshjndwa hata kuingia Google jamani kweli?

Kumbuka mafanikio yanaanza na juhudi zako mwenyewe binafsi
Nalima mahindi si chini ya eka 20 kila msimu kwa mwaka wa 5...hiki ni kitu kipya kwangu alafu google sio kwamba kuna info za kutosha nimekuja jukwaani najua kuna wataalamu au watu wenye uzoefu...unazipimaje akili zangu kirahisi ivyo sababu ya kutokujua kitu fulani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…