Angekuwa na akili hata ile ya chini kabisa, angeudhiwa sana na ushetani wa kuteka watu na kuuawa, lakini kwa sababu halina akili, kutekwa na kuuawa watu wanaomkosoa Rais, kwake ni sherehe, ila kukosolewa Rais kwa maneno makali, anaona ni janga.
Kwa ushetani unaoendelea nchini wa kuteka na kuua wakosoaji na wapinzani, na chaguzi hizi za hovyo, Rais kukaripiwa, kukemewa, kukosolewa na hata kudharauliwa, ni halali yake.
Jukumu la kwanza na la msingi la Serikali yoyote Duniani ni usalama wa wananchi. Sasa nchi ambayo watu wanatekwa na kuuawa, tena bila hatia, na ushenzi huo ukawa unafanywa na vyombo vya dola, hiyo nchi unaweza kusema mna kiongozi anayewajibika? Kama kiongozi hawajibiki, kuna haja gani ya kuheshimiwa?
Wenye akili wote na wanaoelewa maana ya uongozi, hawana haja ya kumheshimu. Asubirie tu mapambio toka kwa machawa punguani. Wenye akili watampongeza siku atakapofanya vizuri, lakini watamkosoa atakapokosea, watamdharau atakapoonesha kiburi au kuubariki uovu kama alivyofabya kwa wauaji wa Kibao.