Nalivua jina la "Zanzibar finest" kwa Feisal Salum nakumpa rasmi kijana kazi kazi "Ibrahimu Bacca"

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
10,587
Reaction score
13,425
Sasa Rasmi nimeamua kumvua Feisal Salum jina la ZANZIBAR FINEST na kumpatia jina hili kijana mdogo anayepiga kazi kubwa mno na kuibeba Zanzibar kwenye mabega yake na siyo mwingine Bali ni Ibrahimu Bacca.

Naam huyu ni beki kitasa Tena kitasa mno beki asiyekua na sifa atakapo fanikiwa kuwini mipira miwili Kama Yule beki mkongo aki win mipira miwili ya mshambuliaji kutoka upinzani hukata Hadi viuno.

Kuanzia Sasa Nampa jina la "ZANZIBAR FINEST " beki kitasa beki sharibu beki anayefuata maelekezo kutoka kwa kocha wake Prof Nabi huyu ni beki anayecheza na mipira ya juu mpaka mipira chini, beki linaloteleza mpaka pakavu.

Hilo ndilo beki lililookoa michomo ya marumo gallants pale Kaka zake wanapopitwa na mawinga hili beki lilisawazisha makosa .

Ibrahimu Bacca ni "ZANZIBAR FINEST"
 
Unamvua, kwani wewe ndiye uliyemvisha?

Mashabiki wa Yanga wana uhayawani. Yote aliyofanya Feisal yanapaswa kufutwa kwa mechi tano za Bacca?

Pathetic!.
 
Jamaa anapiga miguu yote, wa kushoto wa kulia anafanya tackling za maana hachezi rafu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…