Uchaguzi 2020 Namba 06: Aliyewahi kuwa Meya wa Jiji la Dar, Isaya Mwita amechukua fomu kuomba ridhaa kuwania Urais kupitia CHADEMA

Uchaguzi 2020 Namba 06: Aliyewahi kuwa Meya wa Jiji la Dar, Isaya Mwita amechukua fomu kuomba ridhaa kuwania Urais kupitia CHADEMA

Aliyewahi kuwa Mstahiki Meya wa Jiji la Dar, Isaya Mwita amekuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa kuwania nafasi ya Urais Tanzania kupitia CHADEMA

Isaya anayekuwa mgombea wa 6 kuchukua fomu hiyo Kaulimbiu yake ni "Mageuzi ya mfumo wa elimu, upanuaji na uongezaji wa ajira kwa vijana na mchakato wa Katiba Mpya"

Isaya Mwita amesema haya

Mipango mibaya ya Chama kilichopo madarakani ndio maana vijana wengi nchini hawana ajira, kilimo ndio sekta pekee inayoweza kuajiri Watanzania wengi, nikichaguliwa nitalisimamia kuhakikisha vijana wanaomaliza vyuo vikuu wanapata ajira.

Taifa letu lina changamoto kimataifa na hata ndani, kazi yangu kubwa ni kwenda kuhakikisha nchi ina mahusiano mazuri na wadau wa Maendeleo ndani na nje.

Katiba mpya ndio jambo la kwanza nitakaloanza nalo endapo Chama changu kitaniamini na kunipitisha na hatimaye kuwa Rais wa Tanzania, Katiba itaheshimiwa na kila mtu
Mpaka muda huu, Chadema haijapata hata mmoja mwenye sifa ya kupeperusha bendera kuomba ridhaa ya kuwania nafasi ya Uraisi,

Wote walioomba wanafurahisha genge tu, Ila wote hawafai, sio kwamba hawafai tu katika nafasi hiyo Ila hawafai pia hata kwenda kuchukua hizo fomu za uraisi mahali popote kwenye Chama makini!!

Ukweli mchungu
 
Lisu huko aliko atatamani kuangua kilio alikuwa aki ji overstate kuwa yeye ndio yeye hakuna mwingine hiyo nafasi ona sasa watu kibao wanainuka.Meseji sent kwake
CCM tulieni sindano za Lissu ziingie, tafadhali.
 
Mwita mjanja sana. Huyu wameshamtuhumu kuwa ni msaliti na si mmoja wa wanounda ngome au upande wa mwenyekiti.
Mwita anajua fika kuwa hawezi kupita ila hii ndio njia ya kutokea ili aachane na cdm kwa usalama na kutogombea nafasi yoyote wala kwenda ccm. Ongera na kila la kheri kwake.
 
Tangu TAKUKURU watinge UFIPA zinatolewa bure!

Ushauri. Ni vyema sasa ubadili hiyo avatar. Imeshamaliza kazi ya kutufikishia kinyaa cha kisiasa. Aidha, mlengwa wake “keshajirekebisha” muda kitambo sasa. Si vyema, kibinadamu, “aibu” aliyokusudiwa iendelee kukumbushwa. Ameshadhalilishwa vya kutosha.
 
Kwani hawa viongozi wa CDM nafasi ya Urais wa Jamhuri wameionaje. Kama kutoka Sinza madukani kwenda Club Ambiance au?

Waache kuivunjia heshma hii ofisi ya 60m heads + it's blessed natural resources.
Kama Magufuli ameweza na mnampamba kila siku basi hata Dr Shika agombee tu.
 
Back
Top Bottom