Zanzibar 2020 Namba 30: Mussa Aboud Jumbe, Mtoto wa Rais wa zamani wa Zanzibar, Aboud Jumbe amechukua fomu ya CCM kuwania Urais wa Zanzibar

Zanzibar 2020 Namba 30: Mussa Aboud Jumbe, Mtoto wa Rais wa zamani wa Zanzibar, Aboud Jumbe amechukua fomu ya CCM kuwania Urais wa Zanzibar

Historia ya Mzee Sheikh Aboud Mwinyi Jumbe katika siasa za Zanzibar na Tanzania


By dmkali wa JF - click / bofya hapa : Mambo kumi usiyoyajua kuhusu marehemu Aboud Jumbe
1. Rais wa Awamu ya Pili wa Zanzibar, Alhaj Sheikh Aboud Jumbe MIAKA 32 iliyopita, Januari 1984, Halmashauri Kuu (NEC) ya Chama cha Mapinduzi (CCM), iliyoketi mjini Dodoma kwa dharura, ilimvua (ilimpindua?) nafasi zote za uongozi, Nyadhifa alizovuliwa kiongozi huyo na kubakia kuwa raia wa kawaida ni pamoja na urais wa Zanzibar, uenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, umakamu wa Rais wa Tanzania na umakamu Mwenyekiti wa CCM Taifa.

2. Marehemu mzee Jumbe alikuwa mrithi wa Rais wa kwanza wa Zanzibar, Sheikh Abeid Amani Karume, aliyeuawa katika jaribio la mapinduzi ya kijeshi lililoshindwa, Aprili 7, 1972. Kabla ya hapo, Jumbe alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, akishughulikia mambo ya Muungano.

3. Jaribio la mapinduzi lililoshindwa liliandaliwa na wanasiasa makini wa Kizanzibari kwa kuhusisha baadhi ya wanajeshi wa Jeshi la Zanzibar, ambalo hadi akiuawa, Karume alikuwa bado Amiri Jeshi Mkuu wake; kwa kushirikisha pia wanajeshi kadhaa wa Kizanzibari waliokuwa kwenye Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWT) kwa upande wa Bara.

4. Mwalimu Nyerere hakutaka mauaji ya Rais Karume yatafsiriwe au yahusishwe na jaribio la mapinduzi, bali alitaka yatafsiriwe kama mauaji ya kisiasa tu. Akasema, hatua yoyote ya kumteua Kanali Seif Bakari ambaye ni mwanajeshi, kuchukua nafasi ya Karume aliyeuawa na mwanajeshi pia, kungetafsiriwa kama Mapinduzi ya Kijeshi. Hapo, Wazanzibari wakanywea, wakatazamana kwa ishara bila kupata jibu kwa hoja ya Mwalimu Nyerere. Hawakuwa na namna isipokuwa kufuta pendekezo la uteuzi wa Kanali Seif Bakari kumrithi Karume.

5. Ndipo ikawadia zamu ya Mwalimu Nyerere kushawishi na kushauri nani ateuliwe. Akasema, pamoja na kuuawa kwa Karume, ambaye alikuwa mwasisi mwenza wa Muungano wa Tanzania, Muungano huo lazima uendelezwe bila kuyumba; na mtu pekee aliyefaa, kwa maoni ya Nyerere, alikuwa ni Aboud Jumbe Mwinyi, kwa sababu kuu tatu:-

(a). ni msomi na mwanasiasa mkongwe mwenye kuzielewa vyema siasa na migongano ya jamii ya Kizanzibari.

(b). ni mtu ambaye hakuwa na majungu wala makundi yenye kuhasimiana.

(c). wadhifa wake wa Waziri wa nchi, Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais (Mambo ya Muungano) kwa muda mrefu, ilikuwa ni sifa ya ziada iliyompa uzoefu, na uwezo wa kuendeleza na kudumisha Muungano.
Hoja ya Mwalimu ikapita; Jumbe akapaa, akawa Rais wa Zanzibar wa awamu ya pili.

5. Oktoba 1976, maridhiano yalifikiwa ya kuunda Chama kipya, Chama cha Mapinduzi' (CCM), kilichozinduliwa Februari 5, 1977, tarehe na mwezi sawa na ilipozaliwa ASP miaka 20 nyuma, mwaka 1957.
Licha ya Wazanzibari kushinikiza tarehe na mwezi wa kuzaliwa chama chao, yaani Februari 5, walishinikiza pia na kufanikiwa kubakiza neno;Mapinduzi' yaliyoleta uhuru wao Januari 12, 1964, liwe sehemu ya jina la chama kipya. Kwa maana ya Chama cha Mapinduzi bila kuwa na tafsiri yake kwa lugha ya Kiingereza.

6. Hofu ilitanda miongoni mwa Wazanzibari pale Mwalimu alipopendekeza mabadiliko zaidi ya Katiba kutaka kuunda Serikali moja badala ya Serikali mbili, wakihofia nchi yao kumezwa na Tanganyika. Hali hii ilimweka pabaya Jumbe Visiwani juu ya uswahiba wake na Nyerere, wakimwita ;msaliti' wa Mapinduzi ya Zanzibar na Wazanzibari.
kuona hivyo, Jumbe alianza kugeuka nyuma kwa kuchanganyikiwa; akawa njia panda. Wakati hilo halijapoa, jingine kubwa zaidi lilikuwa njiani likija. Mwaka 1983, Edward Moringe Sokoine, aliyekuwa Waziri wa Ulinzi wa Muungano, aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu. Sokoine alikuwa na mvuto wa watu, shupavu na mwadilifu kiasi kwamba katika kipindi kifupi tu alijidhihirisha kuwa chaguo la watu na mrithi halali wa Mwalimu, ambaye naye alimkubali kwa ishara na kwa vitendo.

7. Kwa kuridhika na Sokoine, taratibu Mwalimu alianza kumbeza Jumbe kwa sababu nyingi, lakini Wacha nitaje mbili tu.

(a), alimwona kama kiongozi mpweke asiye na sapoti na aliyepoteza mvuto Visiwani, pia kama dikteta mkimya asiyeshaurika na watu wa chini yake.

(b); Mwalimu aliudhika kwa Jumbe kugeuka mhafidhina wa kidini na mpambanaji wa Kiislamu katika Taifa lisilo na dini. Kwa hili, Jumbe alizuru nchi nzima akitoa hotuba kwenye misikiti, na Serikali ikalazimika kutoa Waraka mkali wa Rais, kuwakumbusha na kuwataka viongozi wa kitaifa kutojipambanua au kuendekeza mambo ya kidini. Jumbe alipuuza Waraka huo; kwake ndio kukawa kumekucha.

Habari za Mwalimu kupoteza imani na upendeleo kwa Jumbe hatimaye zilimfikia kiongozi huyo, zikamuuma sana na kumvunja moyo. Hapo uhasama ukazuka kati yake na Mwalimu kwa njia ya kukomoana. Kwa hasira na kukata tamaa, Jumbe akaanza maandalizi ya kuumbua Muungano, kwa minyukano na Mwalimu.

8. Kuanzisha minyukano hiyo, ilikuwa ni lazima kwanza Jumbe arejeshe imani yake iliyopotea kwa Wazanzibari, kutokana na hatua yake ya kuhamia Mji mwema, Kigamboni na kwa kuwatelekeza Wazanzibari. Baada ya kuridhika kwamba mambo ameyaweka sawa, aliomba mawazo ya Makatibu Wakuu wa Wizara zote na Watendaji Wakuu wengine wa Serikali, ni aina gani ya Muungano unaotakiwa.
Wote, isipokuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali wa Zanzibar, Damian Lubuva, walikataa muundo wa sasa wa Serikali mbili au wa Serikali moja uliokuwa umeanza kupigiwa upatu na Mwalimu na baadhi ya wanasiasa. Jumbe na watendaji wake hao ndani ya Serikali ya Zanzibar wakapendekeza muundo wa Shirikisho lenye Serikali tatu. Serikali ya Tanganyika, Serikali ya Zanzibar na Serikali ya Muungano kwa mambo kumi na moja tu yaliyoainishwa katika Mkataba wa awali wa Muungano.

9. Mtizamo huo ndio aliouweka wazi Jumbe baadaye katika kitabu chake kiitwacho;The Partnership,' yaani ;Ubia kati ya Tanganyika na Zanzibar,' kilichosambazwa mwaka 1984. Kuthibitisha hilo, ananukuu ibara ya tano ya Mkataba wa Muungano inayosema kwamba kufuatia kuundwa kwa Serikali ya Muungano, "Sheria za Tanganyika zilizopo na zile za Zanzibar, zitaendelea kuwa na nguvu katika nchi hizo." (The Partnership, uk. 22).

10. Kuanzia hapo, madai ya Wazanzibari kutaka mabadiliko ya Katiba, huku wengine wakitaka warejeshewe Visiwa vyao (Zanzibar), kupitia mihadhara, magazeti na redio, yalipamba moto ambapo wanajeshi wa Kizanzibari nao walikuwa na malalamiko yao.

Hadi Mungu kamchukua, Mzee jumbe alikuwa ni kiongozi mpambanaji asiyeyumbishwa na kutishwa. Mzee Jumbe amekuwa mgonjwa kwa sikuu kadhaa kabla ya kifo chake,Pamoja na hayo, Mzee Jumbe amekuwa mnyonge kutokana na familia yake kukumbwa na dhoruba la maradhi kwa kipindi kilefu, Akiwemo mkewe, na mwanae ambao nao taarifa zinaonyesha kusumbuliwa na maradhi.

...hii ndio historia fupi ya mzee wetu mpendwa aliye tutoka; Mungu aipokee na kuilaza mahali pema peponi

More info :
WHAT HAPPENED IN ZANZIBAR IN 1984?
The ‘Daily News’ in an article headed ‘Focus “84”‘ has thrown some light on what is described as a ‘serious political crisis’ which occurred at the beginning of 1984 and the efforts of the Party to resolve it.

The article states that the crisis was serious –
because it both endangered the continued existence and survival of the nation as well as the threatened integrity of the political system. For underlying what came t o be described as ‘cleansing the polluted political atmosphere in Zanzibar’ were serious issues of a basic and fundamental nature with important political implications. Basic and fundamental because they were related to national integrity , particularly whether the Union should continue to exist and in the same form and manner as the people had known them since its creation on April 26th. 1964.

The relevance and significance of this development does not merely lie in the fact of its having been amicably resolved. In other words it does not simply lie in the country having successfully averted a potentially dangerous crisis.

It also lies in the fact of those issues and the entire crisis being resolved by the Party. The fact of the Party rather than any other contemporary organ handling this situation is significant because it at tests and underscores its centrality and supremacy in the polity.

This point becomes particularly apparent when the following facts are taken into consideration. First, the emerging crisis was first discussed in the Central Committee of the National Executive Committee of the Party. Second, the whole is sue was brow before the National Executive Committee of the Party and subsequently discussed frankly and exhaustively in one of its most important sessions.

Third, the discussion and debate culminated in the resignation from the offices of Vice-Chairman of the Party, Vice-President of the United Republic of Tanzania, Chairman of the Revolutionary Council of Zanzibar and President of the Revolutionary Government of Zanzibar of Ndugu Aboud Jumbe.

Fourth, it was the National Executive Committee which not only accepted his resignation, but also nominated Ndugu Ali Hassan Mwinyi as Interim Vice-President of the United Republic of Tanzania, Interim Chairman of the Revolutionary Council and Interim President of the Revolutionary Government.

Apart from demonstrating the fact of the supremacy of the Party, the additional significance of this development lies in its being the first time a leader of national importance relinquished his office voluntarily through resignation.

When it is realised the person concerned held the number two office in the Union Government and the number one office in the Revolutionary Government, the significance of the change becomes apparent.

Equally significant is the fact of this change having resulted in the immediate elections in Zanzibar for the offices of the Chairman of the Revolutionary Council and President of the Revolutionary Government. Although it was not the first time those offices were filled through elections, they were nevertheless the first elections to fill an office left vacant by a previous incumbent.
 
Huku bara fomu ni moja tu iliyochapwa kama kitambulisho cha NIDA, CCM woyee demokrasia imeshika hatamu
 
Raza asema Zanzibar 2020 mpambano ni CCM Mpya vs ACT wazalendo
Kutuatia wingi wa wanaCCM kutia nia Zanzibar, watu watoa tafsiri ya jambo hili



Source: KTV TZ online
 

Source : Channel N TZ
RAZA ATEMA CHECHE,AMTAJA MAALIM SEIF PT 2
Watu wachache wenye masanduku na kujidai ni Kingmaker yaani wenye ushawishi wa nani kuwa kiongozi....Zanzibarv pekee Afrika Mashariki na Kati ndiyo kuna upinzani wa kweli na kihistoria ndiyo maana matokeo ya chaguzi zake tofauti yake ni upana wa kijiti tu...

Source : Visiwani TV
 
Hiki kinachotokea Zanzibar ndo kinakuja kutokea majimbon
 
Mussa Aboud Jumbe, Mtoto wa Rais wa zamani wa Zanzibar, Aboud Jumbe amechukua fomu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwania Urais wa Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020. Jumbe amekuwa mgombea wa 30 katika mbio hizo za Urais.

Bado mtoto wa Idrisa Wakil Ngómbe,safi sana watoto wa wakubwa.
 

Mussa Aboud Jumbe ni mmoja wa watoto 14 wa Rais wa pili wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar Sheikh Aboud Mwinyi Jumbe. Sheikh Jumbe anakumbukwa kwa kupigania maslahi mapana zaidi ya Zanzibar ktk Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.

Rais Amani Amani Abeid Karume anasema moja ya alama kubwa alizozipigania Sheikh Aboud Jumbe rais wa Pili ni Baraza la Wawakilishi linaloamua mambo mengi kwa maslahi ya wazanzibari na historia ya taifa hilo la Zanzibar.

Mussa Aboud Jumbe ni mdau mkubwa wa kupigania masuala ya bahari na rasilimali zake. Amehudumu kama Mkurugezi wa Idara ya Samaki wa Serikali ya SMZ katika Wizara ya muhimu ya Maji, Ardhi / Makazi, Nishati, Mazingira na labda atakuwa na maono kama ya baba yake marehemu Sheikh Jumbe.


MUSWADA WA SHERIA YA KUSIMAMIA NA KUENDELEZA UVUVI WA BAHARI KUU WA MWAKA 2020 (THE DEEP SEA FISHERIES MANAGEMENT AND DEVELOPMENT ACT, 2020)

(Kanuni ya 86(6) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, toleo la mwaka 2016)

  1. UTANGULIZI
  2. Mheshimiwa Spika,kwa mujibu wa Kanuni ya 86(6) naomba kuwasilisha maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuhusu Muswada wa Sheria ya Kusimamia na Kuendeleza Uvuvi wa Bahari Kuu ya Mwaka 2020..


  1. Muswada wa Sheria ya Kusimamia na Kuendeleza Uvuvi wa Bahari Kuu ya Mwaka 2020 pamoja na kuweka masharti bora ya usimamizi, udhibiti na uhifadhi wa rasilimali za uvuvi katika Ukanda Maalum wa Uchumi wa Bahari (EEZ). Kutungwa kwa Sheria hii kutaimarisha utekelezaji wa matakwa ya Sheria na Mikataba ya Kikanda na Kimataifa katika kudhibiti na kuhifadhi rasilimali za uvuvi. Aidha, Muswada huu unakusudia kuifuta Sheria ya Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi wa Bahari Kuu, Sura ya 388.
  2. Mheshimiwa Spika, kwa ujumla maudhui ya muswada yako vizuri. Hii ni kutokana na Muswada huu kuzingatia mambo muhimu ambayo Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imekuwa ikiyapendekeza kwa kipindi chote toka mwaka 2005 hadi sasa. Kitendo cha kuzingatia ushauri huo, kinaifanya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni iamini kwamba sasa eneo hili la uvuvi wa bahari kuu; kama litasimamiwa vizuri; linaweza kuifikia ndoto ya mageuzi makubwa ya kiuchumi katika eneo hilo kwa kuwa na mchango mkubwa wa fedha za kigeni na chanzo cha ajira kwa watanzania wengi.
  3. Mheshimiwa Spika, pamoja na nia njema ya muswada huu na licha ya muswada huu kuzingatia mambo mengi muhimu ambayo Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imekuwa ikiishauri Serikali; yapo baadhi ya maeneo ambayo yanatakiwa kufanyiwa marekebisho ili kuifanya sheria inayopendekezwa kuwa bora zaidi. Maeneo hayo ni kama ifuatavyo:-
  4. Tafsiri ya Maana ya Maneno yaliyotumika kwenye Muswada
  5. Mheshimiwa Spika, kifungu cha (3) cha muswada kinachohusiana na tafsiri ya maneno yanayotumika katika muswada, kuna baadhi ya maneno yameshindwa kupatiwa tafsiri na badala yake inatolewa kwenye majukumu ya Mkurugenzi, mfano ni maneno “fishery inspector na fishery observer” hawa ni watu wawili tofauti; lakini majukumu yao hayajaainishwa bayana ili kuwatofautisha jambo ambalo linaweza kuleta mkanganyiko wakati wa utekelezaji wa sheria inayopendekezwa. Kambi Rasmi ya Upinzani inaona ni muhimu sana katika kifungu hiki cha tafsiri kutoa maana inayoeleweka kwa wale wataokuwa wanatumia sheria hii ili kuondoa mkanganyiko usio kuwa na ulazima.
  6. Eneo la Makao Makuu ya Mamlaka
  7. Mheshimiwa Spika, kifungu cha 5(3) cha muswada kinachohusu makao makuu ya mamlaka kuwa yatakuwa ni Zanzibar, au mamlaka inaweza kufungua ofisi yake katika eneo lolote la Tanzania Bara, au nje ya Tanzania Zanzibar– (3) The headquarters of the Authority shall be in Tanzania Zanzibar, ———- or outside Tanzania Zanzibar)
  8. Mheshimiwa Spika, ili kuwa na uelewa uliokusudiwa ni vyema haya maneno “outside Tanzania Zanzibar” yakafutwa kwa kuwa yakiendelea kuwepo maana yake mamlaka inaweza kuwa na ofisi Mombasa, Comoro, Ushelisheli nk. kwani ni nje ya Tanzania Zanzibar pia.
  • Kazi za Mamlaka inayoanzishwa na Muswada
  1. Mheshimiwa Spika, kifungu cha 6(3)(iii) cha muswada kinahusu kazi za mamlaka hii inayoundawa. Kifungu hicho kinachosema kwamba; “concluding agreements for fisheries access by non-citizens and non-nationals, including foreign fishing vessels”. Hapa ndipo kumekuwa na tatizo kubwa sana kwa kuwaachia watu ambao tumewapa mamlaka kwa kuwaamini lakini ukweli wanatuangusha sana. Kambi Rasmi ya Upinzani inapendekeza kwamba mamlaka iongozwe na Sheria za Mamlaka ya Nchi ya Usimamizi wa Mali na Rasilimali asili (The Natural Wealth and Resources (Permanent Sovereignty) Act) na Sheria ya Mapitio na Maelewano Mapya ya Masuala yenye Utata kuhusu Mali na Rasilimali Asili (the Natural Wealth and Resources (Review and Re-Negotiation of Unconscionable Terms) Act 2017 (“Contract Review Act”)”; ili kuziba mianya ya rushwa na utashi binafsi katika kuingia mikataba yenye maslahi ya kiuchumi kwa Taifa.


  1. Mkanganyiko juu ya Matumizi ya Sheria iliyofutwa
  2. Mheshimiwa Spika, kifungu cha 102(2) (b) kinasomeka kwamba; “all licences, permits, authorizations and other instruments or documents granted or issued under the repealed Act, shall, so long as they on the date of commencement of this Act continue in full force and effect until they expire, cease to have effect or are replaced;”


  1. Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani ina wasiwasi na maudhui ya kifungu hicho kwa kuwa inaweza tokea tasnia moja ikawa inatumia sheria mbili tofauti kama ambavyo inatokea kwenye tasnia ya madini kwa baadhi ya makampuni kutumia sheria ya zamani na mengine kutumia sheria mpya kutokana na mikataba na leseni na vibali vilivyokuwa vimetolewa kabla ya matumizi ya sheria mpya. Jambo la kuangangalia ni kwamba uwekezaji katika uvuvi wa bahari kuu ni chombo cha mtu anayefanya biashara hiyo tu kuwa kina viwango vinavyohitajika kwa mujibu wa sheria tu na sio jambo lingine. Hivyo ni tofauti sana na uwekezaji kwenye rasilimali zingine kama mafuta, gesi na madini mengine.
  2. Uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu
  3. Mheshimiwa Spika, kifungu cha 15 kinachohusu uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka, na kifungu kidogo cha (3) kinasema kuwa; ili kudumisha Muungano, Mkurugenzi Mkuu na Naibu Mkurugenzi Mkuu mmoja wapo lazima awe ametoka upande wa pili wa Muungano. Kifungu kinasomeka kama ifuatavyo namba kunukuu “(3) For the purpose of ensuring equal representation of both sides of the Union, the Director General and Deputy Director General shall, at any given time, be appointed one from Mainland Tanzania and the other from Tanzania Zanzibar, and subsequent appointments for each position shall alternate between the two sides of the Union”
Source :: Chama Cha Demokrasia na Maendeleo
 
Mussa Aboud Jumbe ni mdau mkubwa wa kupigania masuala ya bahari na rasilimali zake. Amehudumu kama Mkurugezi wa Idara ya Samaki wa Serikali ya SMZ katika Wizara ya muhimu ya Maji, Ardhi / Makazi, Nishati, Mazingira na labda atakuwa na maono kama ya baba yake marehemu Sheikh Jumbe.
MBUNGE SAADA ATOA ANGALIZO UTUNGAJI WA KANUNI ZA SHERIA YA UVUVI WA BAHARI KUU

20 May 2020
Mbunge wa Welezo, Saada Mkuya akizungumza bungeni alipokuwa akichangia mjadala wa kupitisha muswada wa sharia ya kusimamia na kuendeleza uvuvi wa bahari kuu wa mwaka 2020, jijini Dodoma leo.
Source : mwananchi digital
 
28 Oct 2017
Utafiti wa mafuta na gesi asilia Bahari Kuu , kitalu cha Pemba - Zanzibar
Bi. Salama Aboud Talib waziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wa Maji, Ardhi, Mazingira na Nishati wa SMZ kuhusu kuja kwa meli ya kutafuta mafuta na gesi asilia
 
26 Nov 2018
Zoezi la Mtetemo Kusaka Maliasili Bahari Kuu
Meli ya STANFORD BATELEUR inayotumia teknolojia ya kisasa ya ROV ya kutafuta nishati ya mafuta na gesi asilia, kuanza zoezi la kutafuta viashiria vya nishati hizo kwa njia ya MTETEMO.
 
Miaka 55 ya muungano na Changamoto 15 za muungano.



source : fatuma matulanga
 
Kisima cha kwanza cha utafutaji wa Mafuta na Gesi asilia Zanzibar

24 Oct 2018
Makala ya utafutaji wa mafuta na Gesi asilia kwa Unguja na Pemba.

 
Utiaji Sain Mkataba wa Mafuta na Gesi asilia.
  • 25 Oct 2018

  • 298
  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na mgeni wake Mtawala wa Ras Al Khaimah Shaikh Saud bin Saqr Al Qasimi wakati alipofanya ziara ya kuitembela Zanzibar mara alipofika katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar kushuhudia utiaji wa saini mkataba wa mgawanyo wa uzalishaji wa mafuta na Gesi asilia(PSA) baina ya Serikali ya Mapinduzi na Rakgas
  • Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Rakgas L.L.C ya Ras Al Khaimah Bw.Kamal Mohamed Ataya(kulia) Waziri wa ardhi, Maji,Nishati na Makazi Mhe.Salama Aboud Talib (katikati) Mkurugenzi Katika Kampuni ya Maendeleo ya Mafuta Zanzibar (ZPDC)Nd,Mwanamkaa Abdulrahman Mohamed wakitia saini mkataba wa mgawanyo wa uzalishaji wa mafuta na Gesi asilia(PSA) baina ya Serikali ya Mapinduzi na Rakgas sherehe iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar
Source :
 
http://www.ikuluzanzibar.go.tz/en/m...jengo-la-wizara-ya-ardhinyumbamaji-na-nishati


Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Zanzibar

Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Zanzibar

UZINDUZI WA JENGO LA WIZARA YA ARDHI,NYUMBA,MAJI NA NISHATI.
  • 26 Jun 2020
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifungua pazia kuashiria ufunguzi wa jengo jipya la Wizara ya Ardhi,Nyumba,Maji na Nishati katika hafla iliyofanyika katika jengo hilo leo Maisara Mjini Zanzibar.Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifungua pazia kuashiria ufunguzi wa jengo jipya la Wizara ya Ardhi,Nyumba,Maji na Nishati katika hafla iliyofanyika katika jengo hilo leo Maisara Mjini Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, ameeleza kuwa ujenzi wa majengo bora ya Serikali ni azma iliyoanza mara tu baada ya Mapinduzi matukufu ya Januari 1964.

Akinukuu maelezo ya Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Marehemu Mzee Abeid Amani Karume, Rais Dk. Shein alisema kuwa nchi inaendelea kwa kujengwa majengo na ndio maana Awamu ya Saba nayo inatekeleza hatua hiyo.

Rais Dk. Shein aliyasema hayo leo katika hafla ya ufunguzi wa jengo la Wizara ya Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati pamoja na Taasisi zake ikiwemo Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati (ZURA), huko Maisara, Jijini Zanzibar.

Katika hotuba yake, Rais Dk. Shein alisema kuwa Awamu zote za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zilifuata mkondo huo ambapo kila Awamu ilijenga majengo bora na ya kisasa mjini na vijijini.

Alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ina historia kubwa katika ujenzi wa majengo yakiwemo yale iliyoyajenga wenyewe kwa kupitia wataalamu na wajenzi wazalendo yakiwemo majumba ya Michenzani, Kilimani, Mpapa, Kikwajuni, Mkoani, Wete na Chake Chake kwa kupitia Idara maalum ya ujenzi iliyokuwa chini ya SMZ.

Alisema kuwa ujenzi wa kutegemea wataalamu wa nje unaviza elimu na utaalamu wa wajenzi wazalendo na kueleza nia ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya kuanzisha Kampuni ya Ujenzi yake wenyewe ambayo tayari imeshaanza kazi.

Aliongeza kuwa Kampuni hiyo ishaundwa kwa lengo la kujenga majengo bora na ya kisasa ambayo itawashirikisha wataalamu na mafundi kutoka Idara za Vikosi vya SMZ na pale itakapoonekana haja ya kukaribishwa Kampuni za nje zitakaribishwa.

Rais Dk. Shein alisema kuwa Kampuni hiyo itajengewa uwezo na kwa kuanzia itaanza kujenga majengo ya hospitali ya Binguni, iliyopo Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja ambapo ujenzi wake unatarajiwa kuanza hivi karibuni.

Alieleza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inakwenda na wakati licha ya kuwepo watu ambao hawapendi pale inapofanya mambo mazuri huku akirejea kauli yake ya kukemea vikali wale walioharibu miundomnibu ya taa za barabarani kwa kuzivunja kwa makusudi huko kisiwani Pemba.

Alisisitiza kuwa waliofanya hivyo wana matatizo ya akili kwani si rahisi kwa mtu mwenye akili zake timamu akaharibu kwa makusudi taa za barabarani ambazo zinawasaidia wananchi wote.

Sambamba na hayo Rais Dk. Shein alisema kuwa mwelekeo wa matokeo ya utafutaji wa Mafuta na Gesi Asilia unakwenda vizuri na taarifa maalum itatolewa baada ya Kampuni ya Mafuta na Gesi Asilia Zanzibar (ZPDC) na RAK Gas ya Ras Al Khaimah kumaliza kazi waliyopewa.

Aidha, alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ina uwezo mkubwa na ikiamua kufanya mambo yake wenyewe inafanya tena bila ya kuwezeshwa kama ilivyofanya kwa ujenzi wa jengo hilo ambapo fedha zote ni za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Rais Dk. Shein alitoa pongezi zake kwa viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kufanya kazi kwa pamoja na hatimae kupata mafanikio hayo huku akitumia fursa hiyo kumpongeza Waziri wa Wizara hiyo pamoja na uongozi wote wa Wizara.

Pia, Rais Dk. Shein alitumia fursa hiyo kuipongeza Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati (ZURA) na kueleza jinsi inavyofanya kazi vizuri ikiwa ni pamoja na kuonesha matokeo ya Mamlaka hiyo katika ujenzi wa bandari ya Mangapwani pamoja na nyumba 31 kwa ajili ya wananchi waliopisha ujenzi huo ambao watapewa bure.

Rais Dk. Shein pia, aliipongeza Kampuni ya ujenzi ya Hainan Internationa Limited.

Nae Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati Salama Aboud Talib alimshukuru na kumpongeza Rais Dk. Shein kwa niaba ya wafanyakazi na uongozi wa Wizara hiyo kwa kujenga jengo hilo sambamba na miongozo aliyokuwa akiitoa.

Alieleza kuwa licha ya baadhi ya changamoto zilizotokea lakini mafanikio makubwa yamepatikana ikiwa ni pamoja na kumaliza ujenzi wa jengo hilo kwa wakati huku akieleza sehemu za jengo hilo ukiwemo ukumbi mkubwa na wa kisasa walioupa jina la “Dk. Shein Conference Hall”.

Mapema, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati Ali Khalil Mirza alisema kuwa gharama zote za ujenzi wa jengo hilo zimetolewa na SMZ ambazo ni Tsh. Bilioni 19.9.

Aliongeza kuwa ghorofa 7 za juu ya ardhi za jengo hilo zitatumika kwa shughuli za kiofisi kwa watendaji wa Wizara ya Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati pamoja na Taasisi zake zikiwemo Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati (ZURA), Mamlaka ya Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia (ZPRA), Kampuni ya Maendeleo ya Mafuta na Gesi Asilia Zanzibar (ZPDC) na Idara ya Nishati na Madini.

Alieleza kuwa ghorofa iliyoko kwenye usawa wa ardhi imepangwa kutumika kwa shughuli za kibenki na tayari uongozi wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) inakamilisha taratibu za kuweza kuanza kutoa huduma.

Pamoja na hayo, alieleza kuwa ghorofa iliyopo chini ya ardhi ni kwa ajili ya kuegesha vyombo vya usafiri vya wafanyakazi watakao tumia jengo hilo ambapo zinakadiriwa kuwa maegesho 40.
Katibu Mkuu huyo alitoa pongezi na shukurani kwa Rais Dk. Shein kwa juhudi zake alizozichukua za kuhakikisha kuwa kabla ya kumaliza kipindi chake cha uongozi Wizara hiyo inahamia katika jengo lake jipya kama ilivyo kwa Wizara nyengine za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 
Back
Top Bottom