Tetesi: Namba mbili CHADEMA anakaribia kujiunga na CCM, huyo aliyeenda ametangulizwa tu na Kila kitu kipo tayari. Ni sUala la muda tu

Ninakubaliana nawe sehemu kubwa ya andiko lako.
Slaa; kama mfano wa kukatisha tamaa? Hapana. Hata yeye zilikuwepo dalili toka alipojitokeza kisiasa, kuwepo na vimelea vya kuyumba; kutokuwa na 'moto' unaotogota tumboni na akilini mwake juu ya anayo yasimamia na kuyaamini kwa moyo thabiti.

Mtu wa mwisho, atakaye niondoa hapa nilipo, na kuungana na wewe, kwa sasa anayefahamika ni Tundu Lissu.
Kwa sababu yoyote ile huyu atakaposhawishiwa na kusahau kabisa maslahi mapana juu ya nchi hii na kujiunga na uovu ndani ya CCM..., nitakuwa nawe, bega kwa bega kuhusu hawa wanaojitambulisha kuwa wana siasa.

Lakini. Pamoja na hayo yote; imani yangu ni kwamba CCM katika muundo huu wa sasa, haiendi popote. Wanajitengenezea kaburi lao wenyewe.
 
Lissu anaweza kubaki Chadema mpaka uzeeni, lakini tunaweza vipi kumsaidia kuyafikia malengo yake aliyojiwekea kisiasa?

Kama tunashindwa kumsaidia, kuna ubaya gani Lissu akiamua kurudi CCM akapewe marupurupu yake anayolilia kila siku ya kumuuguza akiwa kalazwa Ubelgiji?

Binafsi kama akiamua kwenda CCM, sitamlaumu, tunajua sana kuwanyooshea vidole hawa watu zaidi ya tunavyojinyooshea sisi wenyewe, tunajiona tuna mamlaka ya kuwahukumu.
 
Hili si 'povu', ila ni kukuonyesha tu 'ujinga' (kwa sasa nitauita hivyo, baadae utakuwa upumbavu)...,
Ushauri namba moja (1), unajua kuwa hawezi kuanzisha chama wakati huu; kama hujui, huo ndio 'ujinga'.

Ushauri namba mbili (2), ndio 'upumbavu huo, tena unao elekea kwenye uhayawani.

Sasa chagua mwenyewe sifa inayo kufaa.
 
Akili za wapi hizi so waanzishe vyama vipya badala ya kukimbilia CCM
 
Ukisikia umbea wa kijinga ndiyo huo, unashindwa nini kutaja jina?

Wewe ni mbea bwege.
 
Lissu hawezi kwenda CCM, hilo kwanza tuliondoe njiani.

Lissu ndani ya CHADEMA isiyo yumbishwa na Mwenyekiti na kundi lake, ni 'lethal' kabisa juu ya uhai wa CCM ya 'Chura Kiziwi'.
Usiwabeze waTanzania; hapana, waTanganyika. Hawa wakati huu wapo btayari kabisa kuizika CCM (hii ya Chura).
Labda izaliwe CCM nyingine kati ya sasa hadi uchaguzi 2025; jambo linalo wezekana sana.
Sasa kama unazungumzia hiyo CCM tofauti na hii ya sasa inayoweza kumshawishi Lissu kuungana nayo, hilo ni jambo tofauti kabisa.

Mkuu 'denoo', hivi kwa nini tunawakatia tamaa sana hawa waTanzania(tanganyika)?
 
Lissu alikataa 1bn ya mwendazake ujue!, ramli au majini ya kzmkaz hayamwezi
 
Serikali ya CCM. Jeuri ya kufuta mfumo wa vyama vingi haina badala yake inahangaika kuua vyama vya upinzani kwa kutumia hela za walipa kodi wasiojielewa kununua makada wa upinzani kwa gharama kubwa. Sijui matarajio ni yepi? Nchi inazidi kufilisika kufurahisha magenge ya mafisadi wa dola.

Wanajaribu kila namna ya vitisho, maangamizi, manyanyaso, propaganda, kumwaga fedha za umma lakini jinamizi “CHADEMA” lipo tu linawakodolea macho. Sijui mwisho utakuwaje? It’s certainly a no win situation. Upinzani hauwezi kufa. Haijawahi kutokea popote tangu kuumbwa kwa dunia. Tuombe tu tusijefikia kuwa a failed state kwa ujinga unaoendelea.
 
Hakuna jipya hapo,alihama Dr.Slaa lakini chama bado kipo imara.
 
Lissu anaweza kubaki Chadema mpaka uzeeni, lakini tunaweza vipi kjmsaidia kuyafikia malengo yake aliyojiwekea? kama tunashindwa, kuna ubaya gani Lissu akiamua kurudi CCM akapewe marupurupu yake anayolilia kila siku ya kumuuguza akiwa Ubelgiji?

Binafsi kama akiamua kwenda CCM, sitamlaumu, tunajua sana kuwanyooshea vidole hawa watu zaidi ya tunavyojinyooshea sisi wenyewe, tunajiona tuna mamlaka ya kuwahukumu
Nimeshaona mengi sana yasiyo na idadi yanayonifanya niwakatie tamaa, tunatendwa vibaya mpaka
tumefika hatua ya kusahau mabaya tuliyotendwa siku za nyuma, sasa tunatendwa mabaya mengine mapya bado tupo kimya tu.

Chukulia mfano, nimegundua yale madudu tunayoambiwa na kuyaona kila siku kwenye ripoti ya CAG kwetu siku hizi sio ajabu tena, tumeshazoea kutafunwa na tumewaacha waendelee kututafuna, tumelala tu.

Sasa wamehamia kwenye kuuza/kutoa sadaka rasilimali zetu, walianza na bandari tumenyamaza, kabla ya hapo walitoka Loliondo, leo tunasikia wametoa sehemu ya bahari, madini ya kimkakati, wamewapa waarabu hekari za misitu zaidi ya laki nane kila siku Lissu anayapigia kelele haya, lakini bado tupo kimya tu...!

Niambie, ni kipi kingine kitakachotuamsha sisi? au mpaka waje kutuuza sisi wenyewe ndio tutaamka?!

Ajabu leo imefika stage mpaka baadhi niliowaona humu ndani wanajielewa, nao wamegeukia upande wa mafisadi, wanampiga vita anayekemea na kufichua ufisadi, simply because sio wa chama chao.

Hawa wanataka kodi zetu zikitafunwa mpaka aseme Lissu ndio wamuelewe, nje ya hapo, kwanza wanakutazama sura wewe ni nani, umetoka wapi!!

Wakati hata Lissu mwenyewe anaungana na mtu kama Mpina kukemea uhuni wa watawala bungeni, sisi huku chini tunahukumiana kwanza, huyu aliwahi kufanya nini kabla? kwao ni kama vile kuna malaika wapo sehemu ndio tunaowahitaji kwenye siasa zetu!.

- Hili taifa bado sana kujikomboa kifikra, achilia mbali kisiasa, na nyanja nyingine, tuna wasomi wengi wasiojua chochote, ndio maana miaka yote tume stack kwenye uchafu wa CCM.

Na ndio maana nasema, kama itatokea mpinzani yeyote akaamua kuondoka na aondoke, sitamlaumu, wameshatuamsha sana mpaka wamechoka, now ni kama wamegundua wanapoteza muda wao kuziamsha maiti.
 
Na ndio maana nasema, kama itatokea mpinzani yeyote akaamua kuondoka na aondoke, sitamlaumu, wameshatuamsha sana mpaka wamechoka, now ni kama wamegundua wanapoteza muda wao kuziamsha maiti.
Nimekusoma vizuri mkuu 'denoo JG', tena siyo mara moja. Nimekuelewa. Sikubaliani na hayo uliyo andika,; na ninaamini hata wewe yanakupa mhangaiko sana hayo kuyakubali.

WaTanzania kamwe hawawezi kuikatia tamaa nchi yao, eti kwa sababu kuna washenzi hawa washenzi wanaoiharibu nchi yao wakati huu. Hatuwezi kuwakatia tamaa na kuwaua moyo wachache wetu wanaotafuta njia za kuondoa takataka hizi. Ni wajibu wetu kuwatia moyo, hata wakati inapoonekana kazi yao inakuwa ngumu.

Licha ya yote uliyo andika hapo, sina shaka yoyote kuhusu upande uliopo wewe katika maswala haya.. Sitetereki hata siku moja, kwani najua Tanzania itashinda tu.
 
Unatakiwa kwenda Kwa fundi madishi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…