Ninakubaliana nawe sehemu kubwa ya andiko lako.
Slaa; kama mfano wa kukatisha tamaa? Hapana. Hata yeye zilikuwepo dalili toka alipojitokeza kisiasa, kuwepo na vimelea vya kuyumba; kutokuwa na 'moto' unaotogota tumboni na akilini mwake juu ya anayo yasimamia na kuyaamini kwa moyo thabiti.
Mtu wa mwisho, atakaye niondoa hapa nilipo, na kuungana na wewe, kwa sasa anayefahamika ni Tundu Lissu.
Kwa sababu yoyote ile huyu atakaposhawishiwa na kusahau kabisa maslahi mapana juu ya nchi hii na kujiunga na uovu ndani ya CCM..., nitakuwa nawe, bega kwa bega kuhusu hawa wanaojitambulisha kuwa wana siasa.
Lakini. Pamoja na hayo yote; imani yangu ni kwamba CCM katika muundo huu wa sasa, haiendi popote. Wanajitengenezea kaburi lao wenyewe.
Lissu anaweza kubaki Chadema mpaka uzeeni, lakini tunaweza vipi kjmsaidia kuyafikia malengo yake aliyojiwekea? kama tunashindwa, kuna ubaya gani Lissu akiamua kurudi CCM akapewe marupurupu yake anayolilia kila siku ya kumuuguza akiwa Ubelgiji?
Binafsi kama akiamua kwenda CCM, sitamlaumu, tunajua sana kuwanyooshea vidole hawa watu zaidi ya tunavyojinyooshea sisi wenyewe, tunajiona tuna mamlaka ya kuwahukumu
Lissu hawezi kwenda CCM, hilo kwanza tuliondoe njiani.
Lissu ndani ya CHADEMA isiyo yumbishwa na Mwenyekiti na kundi lake, ni 'lethal' kabisa juu ya uhai wa CCM ya 'Chura Kiziwi'.
Usiwabeze waTanzania; hapana, waTanganyika. Hawa wakati huu wapo btayari kabisa kuizika CCM (hii ya Chura).
Labda izaliwe CCM nyingine kati ya sasa hadi uchaguzi 2025; jambo linalo wezekana sana.
Sasa kama unazungumzia hiyo CCM tofauti na hii ya sasa inayoweza kumshawishi Lissu kuungana nayo, hilo ni jambo tofauti kabisa.
Mkuu 'denoo', hivi kwa nini tunawakatia tamaa sana hawa waTanzania(tanganyika)?
Nimeshaona mengi sana yasiyo na idadi yanayonifanya niwakatie tamaa, tunatendwa vibaya mpaka
tumefika hatua ya kusahau mabaya tuliyotendwa siku za nyuma, sasa tunatendwa mabaya mengine mapya bado tupo kimya tu.
Chukulia mfano, nimegundua yale madudu tunayoambiwa na kuyaona kila siku kwenye ripoti ya CAG kwetu siku hizi sio ajabu tena, tumeshazoea kutafunwa na tumewaacha waendelee kututafuna, tumelala tu.
Sasa wamehamia kwenye kuuza/kutoa sadaka rasilimali zetu, walianza na bandari tumenyamaza, kabla ya hapo walitoka Loliondo, leo tunasikia wametoa sehemu ya bahari, madini ya kimkakati, wamewapa waarabu hekari za misitu zaidi ya laki nane kila siku Lissu anayapigia kelele haya, lakini bado tupo kimya tu...!
Niambie, ni kipi kingine kitakachotuamsha sisi? au mpaka waje kutuuza sisi wenyewe ndio tutaamka?!
Ajabu leo imefika stage mpaka baadhi niliowaona humu ndani wanajielewa, nao wamegeukia upande wa mafisadi, wanampiga vita anayekemea na kufichua ufisadi, simply because sio wa chama chao.
Hawa wanataka kodi zetu zikitafunwa mpaka aseme Lissu ndio wamuelewe, nje ya hapo, kwanza wanakutazama sura wewe ni nani, umetoka wapi!!
Wakati hata Lissu mwenyewe anaungana na mtu kama Mpina kukemea uhuni wa watawala bungeni, sisi huku chini tunahukumiana kwanza, huyu aliwahi kufanya nini kabla? kwao ni kama vile kuna malaika wapo sehemu ndio tunaowahitaji kwenye siasa zetu!.
- Hili taifa bado sana kujikomboa kifikra, achilia mbali kisiasa, na nyanja nyingine, tuna wasomi wengi wasiojua chochote, ndio maana miaka yote tume stack kwenye uchafu wa CCM.
Na ndio maana nasema, kama itatokea mpinzani yeyote akaamua kuondoka na aondoke, sitamlaumu, wameshatuamsha sana mpaka wamechoka, now ni kama wamegundua wanapoteza muda wao kuziamsha maiti.