KERO Namba ya Huduma kwa Wateja ya Wizara ya Ardhi haipokelewi, siku nyingine haipatikani

KERO Namba ya Huduma kwa Wateja ya Wizara ya Ardhi haipokelewi, siku nyingine haipatikani

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Screenshot 2024-11-22 114603.png
Kumekuwa na shida sana kwenye Namba za Huduma kwa wateja kwenye baadhi ya Wizara za Serikali, kama namba ya huduma kwa wateja Wizara ya Ardhi , mwananchi unapata shida ili upige simu upate msaada wa kitaalamu unakuta namba haiiti na wameitangaza kwenye website ya wizara, au namba inaita ila haipokelewi.

Shida nyingine za migogoro au utaalam wa masuala ya ardhi ni kwa wananchi tunakosa pa kupiga simu na kuuliza kwa haraka na kupata taarifa tunayoitafuta

Tunaomba Waziri wa Ardhi aangalie upande wa kutoa huduma kwa namba ya wateja haina utaratibu mzuri au haijaelewka ijulikane kama haipatikani au inapatikana tujue njia ambayo wanaipenda zaidi, kama wanapenda kila saa twende ofisi za wizara kuuliza mambo madogo madogo pia watuambie

Kuna wakati walikuja na namba ya msaada kwa Whatsapp nayo siku hizi haieleweki mara usijibiwe, wananchi wa kawaida tunashindwa kuelewa tufanye nini?

Tunaomba JamiiForums mpaze sauti kwa ajili yetu
 
Back
Top Bottom