kifupi kirefu
JF-Expert Member
- Oct 29, 2018
- 539
- 3,507
Nilikuwa nafuatilia huko Ulaya kuhusu namna wanafamilia wa watuhumiwa na hata wafungwa wanavyosaidiwa kuepusha adhabu ya makosa ya wazazi kwenda kuwaumiza watoto wasio na hatia. Mara nyingi watoto wa watuhumiwa hupatiwa michango ambapo husaidiwa kuendelea na masomo na kufarijiwa maana kutokufanya hivyo kumechangia watoto wengi kurithi au kujengeka hali ya kutaka kulipa kisasi pale wanapobaini wazazi wao walionewa.
Nichukue fursa kuleta wazo la anayefahamu namba za wake wa watuhumiwa azilete ili michango iweze kutumwa kuwasaidia watoto na kuwafanya wajitenge na kuona wao siyo sehemu ya tuhuma zinazowkabili wazazi wao.
Mbowe naamini anajiweza lakini watuhumiwa watatu waliobaki nadhani wanahitaji familia zao kupata faraja ya kiasi flani Cha kuendesha familia na kupata nauli yakwenda japo kumwona mpendwa wao.
Naamini hili siyo jukumu la chama Cha siasa kwa sababu watuhimiwa siyo wanasiasa na Wala wahanga siyo wanasiasa. Tutoe sadaka kusapoti ndugu zetu Hawa.
Lakini pia hii inafanyika kwa ndugu wengine wote wanaopitia matatizo Kama haya, tukijitoa na kuifanya hii kuwa sehemu ya sadaka zetu tutasaidia kupunguza wahalifu na watu wenye visasi kwenye jamii.
Nawasilishamo.