Namba zinanuka: Naunga mkono TANESCO ifumuliwe, na ikiwezekana ibinafsishwe kabisa, Makamba yupo sahihi 100000%. TANESCO ni janga

Kuna kitu kinaandaliwa kwa ustadi mkubwa sana, huoni puppets wa February wanazidi kujaa humu? Ngoja tusubiri
Mkuu kumbe umeona hee kuna mapapeti hasa yamo humo kuwasifia hao magubigubi
 
Ndio taratibi hizo kila taasis inafabya huvyo hata TRA ;NHIF ni mfumo mzuri wa mKousabyo ya fedha ina inaongeza uwazi .ukitaka kufanya Matumizi unakuwa na bajeti yako na mpango hamna shida yoyote hiyo
 
Ndio taratibi hizo kila taasis inafabya huvyo hata TRA ;NHIF ni mfumo mzuri wa mKousabyo ya fedha ina inaongeza uwazi .ukitaka kufanya Matumizi unakuwa na bajeti yako na mpango hamna shida yoyote hiyo

As long management haikuwa na power ya Ku invest vipaumbele na vibali vya matumizi
Tofauti na mishahara.. huwezi sema Sawa kulinganisha na hao waganda
 
Kwenye hili la centralization aliharibu sana, Ila at least hatukuingia tena ile mikataba ya akina iptl, Dowans, Wala richmond
 


Well actually TANESCO mwaka jana wametengeneza faida nadhani hiyo ndio mara yao kwanza tangia dunia iumbwe.
 
Muundo mzima wa taasisi na mashirika ya umma umejaa kina baba haambiliki, wajuaji, na watu wasiiongeza tija yoyote kwa taifa. Wanalipwa mishahara na wanaona ni haki yao kutokuwajibika.

Cha kushangaza hata wizarani na sehemu nyingine, watu kama hao wamejaa tele. Naangalia kwa makini nini kitatokea Tanesco. Pengine itakuwa ndio mwanzo wa kufanya restructuring ya idara na taasisi nyingine zote kwa manufaa ya Taifa letu
 
Wajinga ndo mtaendelea kumwabudu mwendazake. Yule bwana alikuwa muongomuongo na mlaghai mkubwa.

Hakuna kipindi ambacho ni ngumu kupata data za Tanzania km kipindi alichoongoza huyo mnaemwita shujaa na ukipata data basi lazima inakuwa zimechezewa.

Yule bwana alikuwa dikteta kwa tafsiri yoyote ile.
 
Wewe huna akili, huwezi kuelewa nilichokiandika hapa.

Chuki za Magufuli kukufukua mtaro na akakunyima hela zipeleke huko.

Hizo facts ziko wazi hata waziri amezisema juzi wewe unaleta chuki zako za kijinga hapa.

Kua rais basi na wewe usiwe dikteta, yeye alikua dikteta, shida iko wapi. Wewe kama unaona alikua dikteta mimi naona hakua dikteta, kila mtu abakie na mtazamo wake, tusilazimishane mitazamo.

Toka lini Tanzania ilikua chini ya rais asie dikteta? Ama unajiongelea tu hapa kipumbavu.
 
Kwanni mnalinganisha na miaka 5 iliyopita kwani TANESCO ilikuepo kwa miaka hiyo tu? Mbona hatuongelei kipindi cha unyonyaji wa kupindukia wa DOWANS, SYMBIONS, RICHMOND na IPTL.

Infact, TANESCO ilitoka kwenye kipindi cha unyonyaji na ilikua inaanza kurudi taratibu. Ndo maana mkakati wa kujenga Stieglers Gorge iliku ni sehemu ya kulifanya shirika hili lianze kutengeneza faida kubwa.

But sasa wapigaji wameingia katikati ya process wameanza kutoa hizo takwimu makusudi ili kuupotosha na kupata justification ya kufanya mambo yao. Anyway Time Will Tell!!
 
Hata kwa macho ya kawaida yasiyohitaji kuumiza kichwa..TANESCO ya mwendazake IMEOZA.

JMakamba ana mzigo mzito sana, akijichanganya na Siasa kwenye hii reformations anayotegemea kuifanya amekwenda na Maji.
Acha upuuzi wewe. Huyo Mwendazake aliipokea TANESCO ikiwa katika hali gani? Mbona hatukuona umeme ukikatika kama ilivyokua kipindi cha msoga? Mmeshasahau kina IPTL, SYMBION Walivyokua wanaiuzia TANESCO Umeme kwa gharama kubwa? Huyu mwendazake ndo akaja kuondoa huo upumbavu. Shwain wewe.
 
Kwenye bei regulator atabakia kuwa serikali,hapo serikali inataka wajiendeshe iache kuingilia kwenye management lakini haijawaambia wafanye upuuzi, EWURA iko pale pale.

Kama shirika linakula hasara serikali haiwezi kuliacha mbona ATCL wanakomaa nalo licha ya hasara ya Mabilioni..

Tanesco wanaweza pata faida kwa bongo kwa sababu Wana mtaji wa vyanzo vya umeme wa kutosha ,South kule umeme hata haitoshi.
 
Analysis yako iko biased aidha kwa kutokuchimba sababu za hiyo dismay petfomance au una agernda nyingine ya kutaka shirika liporwe kwa gia cha ubinafsishaji.

Tangu miaka ya tisini TANESCO haijawahi kuwa na maamuzi yake yenyewe. Bodi na menejumenti inapokea maagizo tu ya nini ifanye tena toka kwa wanasiasa ambao hata utaalamu hawana. Mikataba yote ya kifisadi kuanzia ule wa IPTL hadi hii ya sasa ni anri toka nje ya shirika. Hata manunuzi kipi kinunuliwe na wakati gani na wapi vinaamuliwa toka. nje ya shirika halafu unalaumu shirika!

Rudi kafanye anakysis yako vizuri nani hasa aliyelifikisha shirika hapo lilipo.
 
Hoja moja moja. Ewura wana regulate bei ya umeme kulingana na jinsi serikali inavyo subsidise bei ya unit. Sasa kama watu wapo kibiashara, serikali itaendelea ku-subsidise hiyo bei? Kwamba itaendelea kuweka ruzuku kule? Gharama halisi ya kuzalisha hiyo unit moja sio tsh 357. Sasa utazalisha unit moja kwa sh 500 halafu ukauze kwa 357? Ewura watabidi waone hali halisi kama ilivyo kwenye mafuta, wapo huko na watu wanapiga kelele bei ya mafuta, nini wanafanya?

ATCL? Wakina waziri waliliua shirika kwa makusudi ili Precision ifanye biashara.

Unafahamu SA wanatumia nyuklia kuzalisha umeme? Vyanzo vipi sasa hawana? Gesi za aina zote wanatumia wale jamaa.

Tanesco haiwezi kujiendesha kwa faida hata wakiwekwa wafanyabiashara bora kulisimamia shirika endapo halitapumzisha kutoka kwenye mifumo ya kiserikali ambapo itamaanisha mzigo wa kweli uende kwa mlaji.
 
Ndio inatakiwa watu kuwa tayari sasa kukaa mkao wa kibiashara,kama nchi zingine Serikalini zao hazitoi rusuku na huku kwetu ruzuku sio lazima maana hata kwenye kilimo walishaachana na mambo ya ruzuku..

Ewura wanaregulate bei za maji,mafuta na umeme watafanya hivyo..kwani unit ikouzwa 375 Kuna tatizo?
 
Nilimsikia January anasema haikuwa kazi rahisi kumpata MD wa Tanesco! Nilistaajabu kweli! Nikawaza MD anateuliwa na Rais huyu inakuwaje anasema hivi? Kumbe ye January ndiye kamtafuta banah na Bi mdasha kapelekewa jina tu kapitisha! MD wa sasa wa Tanesco qlishapiga maselfie kibao na Nape na isitoshe na washikaji kumbe na January....
 
Naunga mkono hoja , wafumuliwe wooote kabisa , kuanzia wale wa kwenye system ya LUKU, yaani kajamaa kanafanya kazi hakana hata mwaka mmoja kana ghorofa goba na kanaendesha Vogue , sio sawa TANESCO ni majizi , hili shirika likisimamiwa vizuri ni potential sana kwa nchi basi tu
 
Ewura wanaregulate bei za maji,mafuta na umeme watafanya hivyo..kwani unit ikouzwa 375 Kuna tatizo?
Hii 357 ambayo serikali ina mkono wake tu tayari ni mzigo, sasa ikiachwa halisi ambayo gharama za uzalishaji tu hazipungui 500, si utakuwa msiba kwetu kaka?
 
Unavyotoa changamoto na kasoro ni bora uwe na maoni nini kifanyike au ufumbuzi wake ni nini.

Nafikiria kama nia ni kuendesha TANESCO kibiashara basi miundombinu mingi inastahili kung'olewa kwani umeme umepelekwa vijijini kiasi ambacho kama ni mfanya biashara hawezi kupeleka umeme huko. Tukubaliane tu, shirika hili ni la kutoa huduma, kinachotakiwa ni kupunguza gharama zisizo muhimu, wizi na ufisadi. Kodi zetu ziendelee kuwasaidia mabibi na mababu zetu vijijini. Pia tukubali kwa upande mwingine TANESCO bado ipo katika investment prosess, yaani kujenga mabwawa, uzalishaji na usambazaji katika maeneo mbalimbali nchini.
Tunapiga kelele kwa vile tuko mijini nyuma ya kompyuta zetu lakini hatuwafikirii walioko vijijini.
 
SI[emoji3][emoji84][emoji84][emoji972][emoji306]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…