Naanto Mushi
JF-Expert Member
- Oct 16, 2015
- 6,236
- 15,677
Nimekuwa nikitafiti mwenendo wa performance wa shirika letu la umeme kwa muda mrefu, ila sikuweza kufanikiwa kupata takwimu kwa wakati. Nikimaanisha takwimu za kifedha za shirika letu hili. Nashukuru Mungu leo wameweka taarifa za kifedha na nimeweza kuendelea na utafiti wangu.
Ila kwa kweli ni kwamba hili shirika naweza kusema kabisa kwa performance kiduchu niliyoiona, nakubaliana kabisa na yeyote yule amabaye ana mtizamo wa kufanya mabadiliko kwenye shirika hili. Namba zinanuka zimeoza kabisa, kwa miaka mitano iliyopita hakuna performance yoyote ya kueleweka.
Ili tuweze kuelewa maana ya 'underperformance ya TANESCO, nimeamua kufananisha na shirika lingine la umeme la Uganda 'TANESCO ya UGANDA' ... yaani hii comparative analysis inaweza kukutoa machozi, na kuamini ni kwa jinsi gani watanzania tunakuwa wazembe kiasi hiki.
Siwezi kuandika naomba namba ziongee zaidi....
Ndo mana bado ntazidi kuamini ya kwamba nchi hii kuna mambo mengi sana tumepigwa mchanga wa macho.......
Maelezo kwa faida ya wengi
Hii maana yake ni kwamba, Tanesco ya Tanzania wamerundika amana (assets) nyingi ambazo hazitengenezi mapato yoyote na hali imekuwa hivo ndani ya miaka mitano iliyopita. (Huu ni ukichaa wa aina yake) And mind you, hizi amana zimekuwa zikiongezwa kwa kutumia pesa za walipa kodi kwa sababu Tanesco ni mali ya serikali... Umewaza nini hapo???? Watanzania tumekuwa tukilipia hii inefficiency ya Tanesco for years.... Ni sawa sawa mtoto na kuwa unauza shamba ngombe zako kupeleka Ngombe shule... Thats it...
Kwa faida ya wengi.

Kwa miaka karibu mitano (2016 - 2020): Tanesco ya Tanzania imekuwa ikikusanya mapato ambayo ni wastani wa pungufu ya 16% ya jumla ya mali zake zote. Wakati kwa Tanesco ya Uganda kwa kipindi hicho hicho wameweza kuwa wanakusanya mapato ambayo ni zaidi ya asilimia 63 ya jumla ya amana zake (Assets).
Hii maana yake ni kwamba, Tanesco ya Tanzania wamerundika amana (assets) nyingi ambazo hazitengenezi mapato yoyote na hali imekuwa hivo ndani ya miaka mitano iliyopita. (Huu ni ukichaa wa aina yake) And mind you, hizi amana zimekuwa zikiongezwa kwa kutumia pesa za walipa kodi kwa sababu Tanesco ni mali ya serikali... Umewaza nini hapo???? Watanzania tumekuwa tukilipia hii inefficiency ya Tanesco for years.... Ni sawa sawa mtoto na kuwa unauza shamba ngombe zako kupeleka Ngombe shule... Thats it...
| TANESCO YA UGANDA (UMEME) | |
| Revenue growth between (2016 - 2020) | 22.28% |
| Total assets growth (2016 - 2020) | 19.72% |
| TANESCO YA TANZANIA | |
| Revenue growth between (2016 - 2020) | 13.38% |
| Total assets growth (2016 - 2020) | 42.90% |
Kwa faida ya wengi.
Kati ya mwaka 2016 na 2020, Tanesco ya Tanzania mbali na kuongeza assets zake kwa karibu nusu, ila waliweza kuongeza mapato yao kwa asilimia 13 tu. (Ukilema wa hali ya juu) Inaonesha maamuzi ya kuongeza assets hayakuendana na namna ya kutumia hizi assets kuongeza mapato. (Inaonesha kulikuwa na ombwe kubwa la kufikiri na kufanya maamuzi)
Angalia Tanesco wa Uganda, ndani ya mda huo huo waliweza kuongeza assets zao kwa asilimia 19% na wakaweza kuongeza mapato kwa karibu asilimia 22% (Genius!!!!) Hii maana yake ni decisions za mtu anayefikiri, unanunua assets unaongeza mapato... ndo biashara inavofanywa hivi.