‘Namba zinanuka’ – Serikali imechangia kudumaza mifuko ya Hifadhi ya Jamii

‘Namba zinanuka’ – Serikali imechangia kudumaza mifuko ya Hifadhi ya Jamii

Naantombe Mushi

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2015
Posts
6,253
Reaction score
15,748
Habarini wakuu, nimefanikiwa kufanya utafiti ambao ulilenga kuchambua taarifa mbali mbali za kiuchumi za serikali na hususani kabisa zilizolenga taarifa ya kifedha ya serikali (Financial statements) kuanzia mwaka wa fedha wa June 2016 mpaka June 2019.

Takwimu nilizotumia kwenye uchambuzi nimezitoa website ya Wizara ya Fedha na Chache sana Banki kuu ya Tanzania.

Nimegundua mengi sana sana, hususani hata sababu ya kutekelezaji tata wa baadhi ya sera, kwa mfano ile ya ‘Mabadiliko yaliyotokea kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii katika kipindi cha ndani ya miaka 2 iliyopita.

Nitawasilisha taarifa moja baada ya nyingine ya uchunguzi wangu katika nyuzi tofauti ili watu waweze ku concentrate, nimegundua hoja nyingi sana ambazo zinahitaji kuhojiwa na wananchi ndo mana nimeanza na muhtasari ‘namba zinanuka – kutokana na mimi binafsi kutokuridhishwa na nilichokiona kwa uelewa wangu wa kiuchumi’

*******

Taarifa za fedha zinaonesha mwonendo usioridhisha kwenye hii mifuko kwa kuangalia kuanzia June 2016 mpaka June 2018 – mifuko imekuwa ikijiaendasha kwa nakisi (makusanyo ya wanachama yamekuwa pungufu ya benefits zote zilizotolewa na mifuko) hii ikiwa ina maanish kukosekana kwa ufanisi wa kujiendesha. Ingekuwa ni biashara binafsi ingekuwa ni 'Loss making business' Expenses zimezidi Revenues.

Hizi figure za nakisi zinazoonekana ni bilioni sio milioni.
Mwaka 2016 - Bilioni 839
Mwaka 2017 - Bilioni 924
Mwaka 2018 - Bilioni 526
net pension.JPG


Kwa miaka mitatu kuanzia 2016 mpaka 2018, mifuko ya hifadhi ya jamii ilitengeza nakisi jumla ya Shillingi Trilioni 2.29.

Ukiangalia kwa makini kwenye hizi takwimu, unaweza kuona haswa ni nini ilikuwa sababu ya mabadiliko ya hivi karibuni katika mifuko ya hifadhi ya jamii ikiwemo;
  • Kuunganisha mifuko,
  • Sheria tata kuhusu fao la kujitoa (ambalo kwa miaka ya hivi karibuni limekuwa na utata mkubwa)
Kwamba sababu kubwa ilitokana na kudorora kwa ufanisi mwaka hadi mwaka (June 2016 - June 2018). Ambayo ikachangia kuongeza risk kubwa sana ya survival ya hii mifuko.


Kuna swali la kujiuliza hapa
  • Je, kwa kiasi gani serikali kuu inachangia kudumuza hii mifuko?
Again namba zinatuambia kwamba, serikali kuu haiwezi kujitenga na lawama za kudumaza hii mifiko. Serikali imekuwa na malimbikizo makubwa ya madeni kwenye hii mifuko kiasi cha kuendelea kuhatarisha uendeshaji wake.

Madhara ya madeni mlimbikizo ya serikali kwenye hii mifuko, yanasababisha kwa kiasi kikubwa ukata kwenye hii mifuko, kiasi cha kushindwa kutimiza kikamilifu shughuli zao nyingine za uwekezaji.

Haina tofauti na mtu una pesa nyingi lakini umezikopesha kwa watu ambao hawakulipi, ni wazi kwamba kama kuna maendeleo ulipaswa kuyafanya kama kujenga nyumba, ina maana kutakuwa na pesa za kufanya hivo. Utakuwa huna tofauti na TAJIRI AMBAYE NI MASKINI.

pension obligations.JPG



Hii ina maana gani?
  • Kama serikali, haitachukua hatua za kulipa kwa wakati madeni yake kwenye mifuko ya hifandhi ya jamii, ina maana ya kwamba ufanisi katika mifuko hii utazidi kuendelea kudorora, na hii ikimaanisha pia kudumaa pia kwa huduma za mifuko hii kwa wanachama wao. (Hasara kwa wafanyakazi).
  • Kushuka kwa uwezo wa mifuko hii katika kufanya shughuli zao za uwekezaji. Hii inaenda kupelekea kushuka kwa ‘value creation’ ambayo ingepaswa kufanyika na hii mifuko. Ikumbukwe maana halisi ya kuwa hii mifuko ni pia kukuza michango ya wanachama kupitia nyia ya uwekezaji. Lakini sasa, kwa kuwa serikali imekopa hiyo michango na haiirudishi kwa wakati, ina maana mifuko inakosa ukwasi wa kuwekeza.

Nimalizie kusema kwamba, kuna mambo mengi sana yamejificha kwenye namba ukiachana na siasa za kishabiki na kishangiliaji, mambo ambayo yanatugusa watanzania na yanahusiana moja kwa moja na mwenendo wa uchumi wetu.

Nazidi kujitenga na waoamini kwamba uchumi wetu upo stable. Nikimaliza kutoa nyuzi zangu, nadhani tutakubaliana kwenye hili. Uchumi upo weak sana, ukifuatilia hizi hizi takwimu za serikali.
 
Hiyo mifuko soon itakufa.

Wastaafu humiza miaka hawajaanza kulipwa mafao yao.

Serikali ya wanyonge imekopa kwenye hiyo mifuko inaenda kuifilisi.

Mifuko ndio tegemeo la pesa kwa serikali ya wanyonge. Ndio maana kila kukicha ni sheria juu ya mifuko.

Independent audit ikifanyika juu ya mifuko itaonyesha hali halizi, mifuko iko icu.
 
Nina shemeji yangu alikuwa anafuatilia fao lake la uzazi mpaka kaamua mwenyewe kuachia. Baada ya trip kadhaa za nenda rudi kuna msamaria aliamua kumwambia ukweli kuwa rudi tu kazini dada huku pesa hakuna.
 
Nina shemeji yangu alikuwa anafuatilia fao lake la uzazi mpaka kaamua mwenyewe kuachia. Baada ya trip kadhaa za nenda rudi kuna msamaria aliamua kumwambia ukweli kuwa rudi tu kazini dada huku pesa hakuna.
Hii mifuko haina sustainability, ndo mana mi huwa nawaambia watu kwa utani. 'Hivi una uhakika gani ukistaafu utapata pension'?

Hii mifuko ipo kwa majina tu, ila ipo kwenye maporomoko ya kufa kwenye operations
 
Jamaa wamekomba pesa huko halafu kila siku wanasema tuna maheraaaa mengi sana huku wastaafu wanasotea mafao yao kwa miaka mingi.

Lkn wabunge wao jana hio hio wameshaingiziwa pesa zao.
Hii mifuko ni mfu.. ni lazima wawalipe wabunge maana wanaogopa kusemwa vibaya na wanasiasa, ila tunaoumia ni wanyonge maana hatuna ushawishi wowote
 
Naomba kuuliza hii mifuko iko na fao la kujitoa?
Hizo zipo kwenye makaratasi tu ila ki uhalisia, fao la kujitoa ni kama hakuna kwa sasa hivi, na hata wanaofuatilia uliza danadana wanazopigwa.

Ni kwamba aliyesababisha haswa ni serikali, kama isingelikuwa serikali imekopa madeni kwenye mifuko na kushindwa kuyalipa, ina maana ya kwamba, mifuko ingekuwa na uwezo wa kutoa mafao ya kujitoa.

Maana technically ukifikiria, pesa ni za wanachama, sasa kwanini ukizitaka huwezi pata?

Mi nasikitikia watu wanazidi kuishabikia hii serikali badala ya kufanya ukosoaji wa aina hii
 
Hizo zipo kwenye makaratasi tu ila ki uhalisia, fao la kujitoa ni kama hakuna kwa sasa hivi, na hata wanaofuatilia uliza danadana wanazopigwa.

Ni kwamba aliyesababisha haswa ni serikali, kama isingelikuwa serikali imekopa madeni kwenye mifuko na kushindwa kuyalipa, ina maana ya kwamba, mifuko ingekuwa na uwezo wa kutoa mafao ya kujitoa.

Maana technically ukifikiria, pesa ni za wanachama, sasa kwanini ukizitaka huwezi pata?

Mi nasikitikia watu wanazidi kuishabikia hii serikali badala ya kufanya ukosoaji wa aina hii
Unajua sijajua sheria ya hii mifuko ya mafao,hivi unaweza kufanya chaguzi mana mifuko ya mafao iko mingi,mana nataka kuzungumzia kitu hapa
 
Ukiona wanaunganisha jua mambo si mambo. Utashangaa TTCL na Airtel zikiwa kampuni 1. TTCL inanunua kila kitu alicho nacho Airtel
 
Unajua sijajua sheria ya hii mifuko ya mafao,hivi unaweza kufanya chaguzi mana mifuko ya mafao iko mingi,mana nataka kuzungumzia kitu hapa
Huwezi kufanya uchaguzi, mifuko ni 2 tuu hivyo ukiwa govt unakua PSSF, ukiwa private unakua NSSF
 
Serikali isitishe mara moja kuchangia 15% ya mshahara wa Mwanachama.

Badala yake iwe 10% ya mchango, kama kwenye sekta binafsi.

Itapunguza mzigo wa madeni kwa 33%.
 
Kama serikali kila mwaka inachota pesa kwenye hiyo mifuko na hawarudishi nakisi haiwezi kukosekana, japo huwa hawasemi kwa kuogopa lawama.

Ndio maana kila siku wastaafu wanalalamika hawajalipwa mafao yao, hii serikali sijui ni ya "wanyonge" wa kijiji gani!.
 
Alivyowafanyia watumishi hakika Mungu yupo.Miaka yote 5 ni kapa huku wakidhalilika kwa hali ngumu ya maisha huko mtaani.Poleni walimu,madaktari,wauguzi etc
Na kwa hali hii ya hii mifuko, Sioni hatma nzuri ya wastaafu. Hakuna kipindi kinaenda kuwa kigumu kwa wastaafu kama hiki.
 
Back
Top Bottom