‘Namba zinanuka’ – Serikali imechangia kudumaza mifuko ya Hifadhi ya Jamii

Ukiona wanaunganisha jua mambo si mambo. Utashangaa TTCL na Airtel zikiwa kampuni 1. TTCL inanunua kila kitu alicho nacho Airtel
Hata sekta ya bank (TIB na TPB) Hii inayofanyika ya kuanganisha hizi taasisi mfu ni kwamba Wana dilute mabovu na yenye afadhali. Kama ilivofanyika kwenye mifuko
 
Hali hii inaleta mashaka makubwa kwa watu wanaotarajia kustaafu....
Kila mfanyakazi mwenye ndoto za kustaafu lazima anapaswa kuogopa. Hakuna anayependa kuishi uzee wa mateso.

Watanzania wafanyakazi wametoka jasho sana kwenye hii mifuko. Kinachofanyika na serikali sio fair kwa wafanyakaz
 
Kama serikali kila mwaka inachota pesa kwenye hiyo mifuko na hawarudishi nakisi haiwezi kukosekana, japo huwa hawasemi kwa kuogopa lawama.

Ndio maana kila siku wastaafu wanalalamika hawajalipwa mafao yao, hii serikali sijui ni ya "wanyonge" wa kijiji gani!.
Hivi ndo vitu watu wanapaswa wahoji.. lakini utashangaa kila kukicha na mambo ya kijinga ya wanasiasa wakizidi kutuhadaa.
 
Wafanyakazi wenyewe si wafuatiliaji wa habari za siasa na wanasiasa hivyo haya wengi hawayajui kwa undani.
Yaah inahitaji kuchambua pia.. kuna report nyingi sana zinatolewa kila kukicha na serikali lakini watu hawazifuatilii..

Najua itakuwa ni ngumu sana kwa watu wengi kuelewa haya masuala maana yamekaa ki technical.

Watu watashtuka itakuwa ni too late.
 
Hizo zipo kwenye makaratasi tu ila ki uhalisia, fao la kujitoa ni kama hakuna kwa sasa hivi, na hata wanaofuatilia uliza danadana wanazopigwa.

Ni kwamba aliyesababisha haswa ni serikali, kama isingelikuwa serikali imekopa madeni kwenye mifuko na kushindwa kuyalipa, ina maana ya kwamba, mifuko ingekuwa na uwezo wa kutoa mafao ya kujitoa.

Maana technically ukifikiria, pesa ni za wanachama, sasa kwanini ukizitaka huwezi pata?

Mi nasikitikia watu wanazidi kuishabikia hii serikali badala ya kufanya ukosoaji wa aina hii
Mbona watu wanalipwa ila sio wale wenye professional
 
Was
Habarini wakuu, nimefanikiwa kufanya utafiti ambao ulilenga kuchambua taarifa mbali mbali za kiuchumi za serikali na hususani kabisa zilizolenga taarifa ya kifedha ya serikali (Financial statements) kuanzia mwaka wa fedha wa June 2016 mpaka June 2019.

Takwimu nilizotumia kwenye uchambuzi nimezitoa website ya Wizara ya Fedha na Chache sana Banki kuu ya Tanzania.

Nimegundua mengi sana sana, hususani hata sababu ya kutekelezaji tata wa baadhi ya sera, kwa mfano ile ya ‘Mabadiliko yaliyotokea kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii katika kipindi cha ndani ya miaka 2 iliyopita.

Nitawasilisha taarifa moja baada ya nyingine ya uchunguzi wangu katika nyuzi tofauti ili watu waweze ku concentrate, nimegundua hoja nyingi sana ambazo zinahitaji kuhojiwa na wananchi ndo mana nimeanza na muhtasari ‘namba zinanuka – kutokana na mimi binafsi kutokuridhishwa na nilichokiona kwa uelewa wangu wa kiuchumi’

*******

Taarifa za fedha zinaonesha mwonendo usioridhisha kwenye hii mifuko kwa kuangalia kuanzia June 2016 mpaka June 2018 – mifuko imekuwa ikijiaendasha kwa nakisi (makusanyo ya wanachama yamekuwa pungufu ya benefits zote zilizotolewa na mifuko) hii ikiwa ina maanish kukosekana kwa ufanisi wa kujiendesha. Ingekuwa ni biashara binafsi ingekuwa ni 'Loss making business' Expenses zimezidi Revenues.

Hizi figure za nakisi zinazoonekana ni bilioni sio milioni.
Mwaka 2016 - Bilioni 839
Mwaka 2017 - Bilioni 924
Mwaka 2018 - Bilioni 526
View attachment 1481501

Kwa miaka mitatu kuanzia 2016 mpaka 2018, mifuko ya hifadhi ya jamii ilitengeza nakisi jumla ya Shillingi Trilioni 2.29.

Ukiangalia kwa makini kwenye hizi takwimu, unaweza kuona haswa ni nini ilikuwa sababu ya mabadiliko ya hivi karibuni katika mifuko ya hifadhi ya jamii ikiwemo;
  • Kuunganisha mifuko,
  • Sheria tata kuhusu fao la kujitoa (ambalo kwa miaka ya hivi karibuni limekuwa na utata mkubwa)
Kwamba sababu kubwa ilitokana na kudorora kwa ufanisi mwaka hadi mwaka (June 2016 - June 2018). Ambayo ikachangia kuongeza risk kubwa sana ya survival ya hii mifuko.

Kuna swali la kujiuliza hapa
  • Je, kwa kiasi gani serikali kuu inachangia kudumuza hii mifuko?
Again namba zinatuambia kwamba, serikali kuu haiwezi kujitenga na lawama za kudumaza hii mifiko. Serikali imekuwa na malimbikizo makubwa ya madeni kwenye hii mifuko kiasi cha kuendelea kuhatarisha uendeshaji wake.

Madhara ya madeni mlimbikizo ya serikali kwenye hii mifuko, yanasababisha kwa kiasi kikubwa ukata kwenye hii mifuko, kiasi cha kushindwa kutimiza kikamilifu shughuli zao nyingine za uwekezaji.

Haina tofauti na mtu una pesa nyingi lakini umezikopesha kwa watu ambao hawakulipi, ni wazi kwamba kama kuna maendeleo ulipaswa kuyafanya kama kujenga nyumba, ina maana kutakuwa na pesa za kufanya hivo. Utakuwa huna tofauti na TAJIRI AMBAYE NI MASKINI.

View attachment 1481504

Hii ina maana gani?
  • Kama serikali, haitachukua hatua za kulipa kwa wakati madeni yake kwenye mifuko ya hifandhi ya jamii, ina maana ya kwamba ufanisi katika mifuko hii utazidi kuendelea kudorora, na hii ikimaanisha pia kudumaa pia kwa huduma za mifuko hii kwa wanachama wao. (Hasara kwa wafanyakazi).
  • Kushuka kwa uwezo wa mifuko hii katika kufanya shughuli zao za uwekezaji. Hii inaenda kupelekea kushuka kwa ‘value creation’ ambayo ingepaswa kufanyika na hii mifuko. Ikumbukwe maana halisi ya kuwa hii mifuko ni pia kukuza michango ya wanachama kupitia nyia ya uwekezaji. Lakini sasa, kwa kuwa serikali imekopa hiyo michango na haiirudishi kwa wakati, ina maana mifuko inakosa ukwasi wa kuwekeza.

Nimalizie kusema kwamba, kuna mambo mengi sana yamejificha kwenye namba ukiachana na siasa za kishabiki na kishangiliaji, mambo ambayo yanatugusa watanzania na yanahusiana moja kwa moja na mwenendo wa uchumi wetu.

Nazidi kujitenga na waoamini kwamba uchumi wetu upo stable. Nikimaliza kutoa nyuzi zangu, nadhani tutakubaliana kwenye hili. Uchumi upo weak sana, ukifuatilia hizi hizi takwimu za serikali.
Washangiliaji walisema kuunganisha hii mifuko ni kuiimarisha,ila dalili zilizo dhahiri ni kwanba imekuwa dhaifu zaidi.Hatuambiwi mifuko iliyovunjwa ilikuwa na mtaji kiasi gani kila moja kabla ya kuunganishwa. Je,walikokotoa kila mwanachama alikuwa anamiliki kiasi gani kabla na baada ya kuunganisha mifuko?
Hii mifuko ya hifadhi ya jamii has a ni Mali ya serikali au wanachama(wachangiaji)?Je,hii mifuko inapotoa mikopo aidha kwa serikali au watu binafsi inatoza riba?Sheria ya fedha inaruhusu hiyo biashara?
Je,mifuko hii inapowekeza kwenye miradi mbalimbali kama Real Estate Businesses, madaraja kama like LA Kigamboni au viwanda nani anakusanya mapato na faida ya uwekezaji ni vya nani?Uhusika wa serikali kwenye hii mifuko ni wa umiliki,uchangiaji au?
Kiujumla nadhani kuunganishwa kwa hii mifuko ni njia mojawapo ya ufisadi wa kidola/kimfumo.Kina mchezo mchafu hapo.Tunatakiwa kupatiwa ukweli,nchi hii inakoelekea ni Mungu tu pekee ndiye afahamuye.Inavyoonekana hata wananchi wa Tanzania na wale wanaojiita viongozi hawafahamu tunatika wapi,tunaelekea wapi na njia IPI bora inayoweza kutufikisha huko.
 
Mad
Jamaa wamekomba pesa huko halafu kila siku wanasema tuna maheraaaa mengi sana huku wastaafu wanasotea mafao yao kwa miaka mingi.

Lkn wabunge wao jana hio hio wameshaingiziwa pesa zao.
Madikteta wote ndivyo wanavyoendesha Tawala zao,wastaafu na watumishi(wachangiaji) wa mifuko ya hifadhi ya jamii wanahangaikia mafao yao kwa damu,jasho na uhai wao,wakati wakidaiwa vyeti,barua nk ili makusanyo yatakayopatikana yanaweza kuokoa jahazi.Lakini linapokuja suala la Gratitude Benefits, haipiti hata siku moja wanapewa 100%+
 
Inaudhi sana.. lakini pia ukifikiria watu wanazidi kuwashabikia hawa watu.. mtu ndo unachoka kabisa
 
Habarini wakuu, nimefanikiwa kufanya utafiti ambao ulilenga kuchambua taarifa mbali mbali za kiuchumi za serikali na hususani kabisa zilizolenga taarifa ya kifedha ya serikali (Financial statements) kuanzia mwaka wa fedha wa June 2016 mpaka June 2019.

Takwimu nilizotumia kwenye uchambuzi nimezitoa website ya Wizara ya Fedha na Chache sana Banki kuu ya Tanzania.

Nimegundua mengi sana sana, hususani hata sababu ya kutekelezaji tata wa baadhi ya sera, kwa mfano ile ya ‘Mabadiliko yaliyotokea kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii katika kipindi cha ndani ya miaka 2 iliyopita.

Nitawasilisha taarifa moja baada ya nyingine ya uchunguzi wangu katika nyuzi tofauti ili watu waweze ku concentrate, nimegundua hoja nyingi sana ambazo zinahitaji kuhojiwa na wananchi ndo mana nimeanza na muhtasari ‘namba zinanuka – kutokana na mimi binafsi kutokuridhishwa na nilichokiona kwa uelewa wangu wa kiuchumi’

*******

Taarifa za fedha zinaonesha mwonendo usioridhisha kwenye hii mifuko kwa kuangalia kuanzia June 2016 mpaka June 2018 – mifuko imekuwa ikijiaendasha kwa nakisi (makusanyo ya wanachama yamekuwa pungufu ya benefits zote zilizotolewa na mifuko) hii ikiwa ina maanish kukosekana kwa ufanisi wa kujiendesha. Ingekuwa ni biashara binafsi ingekuwa ni 'Loss making business' Expenses zimezidi Revenues.

Hizi figure za nakisi zinazoonekana ni bilioni sio milioni.
Mwaka 2016 - Bilioni 839
Mwaka 2017 - Bilioni 924
Mwaka 2018 - Bilioni 526
View attachment 1481501

Kwa miaka mitatu kuanzia 2016 mpaka 2018, mifuko ya hifadhi ya jamii ilitengeza nakisi jumla ya Shillingi Trilioni 2.29.

Ukiangalia kwa makini kwenye hizi takwimu, unaweza kuona haswa ni nini ilikuwa sababu ya mabadiliko ya hivi karibuni katika mifuko ya hifadhi ya jamii ikiwemo;
  • Kuunganisha mifuko,
  • Sheria tata kuhusu fao la kujitoa (ambalo kwa miaka ya hivi karibuni limekuwa na utata mkubwa)
Kwamba sababu kubwa ilitokana na kudorora kwa ufanisi mwaka hadi mwaka (June 2016 - June 2018). Ambayo ikachangia kuongeza risk kubwa sana ya survival ya hii mifuko.

Kuna swali la kujiuliza hapa
  • Je, kwa kiasi gani serikali kuu inachangia kudumuza hii mifuko?
Again namba zinatuambia kwamba, serikali kuu haiwezi kujitenga na lawama za kudumaza hii mifiko. Serikali imekuwa na malimbikizo makubwa ya madeni kwenye hii mifuko kiasi cha kuendelea kuhatarisha uendeshaji wake.

Madhara ya madeni mlimbikizo ya serikali kwenye hii mifuko, yanasababisha kwa kiasi kikubwa ukata kwenye hii mifuko, kiasi cha kushindwa kutimiza kikamilifu shughuli zao nyingine za uwekezaji.

Haina tofauti na mtu una pesa nyingi lakini umezikopesha kwa watu ambao hawakulipi, ni wazi kwamba kama kuna maendeleo ulipaswa kuyafanya kama kujenga nyumba, ina maana kutakuwa na pesa za kufanya hivo. Utakuwa huna tofauti na TAJIRI AMBAYE NI MASKINI.

View attachment 1481504

Hii ina maana gani?
  • Kama serikali, haitachukua hatua za kulipa kwa wakati madeni yake kwenye mifuko ya hifandhi ya jamii, ina maana ya kwamba ufanisi katika mifuko hii utazidi kuendelea kudorora, na hii ikimaanisha pia kudumaa pia kwa huduma za mifuko hii kwa wanachama wao. (Hasara kwa wafanyakazi).
  • Kushuka kwa uwezo wa mifuko hii katika kufanya shughuli zao za uwekezaji. Hii inaenda kupelekea kushuka kwa ‘value creation’ ambayo ingepaswa kufanyika na hii mifuko. Ikumbukwe maana halisi ya kuwa hii mifuko ni pia kukuza michango ya wanachama kupitia nyia ya uwekezaji. Lakini sasa, kwa kuwa serikali imekopa hiyo michango na haiirudishi kwa wakati, ina maana mifuko inakosa ukwasi wa kuwekeza.

Nimalizie kusema kwamba, kuna mambo mengi sana yamejificha kwenye namba ukiachana na siasa za kishabiki na kishangiliaji, mambo ambayo yanatugusa watanzania na yanahusiana moja kwa moja na mwenendo wa uchumi wetu.

Nazidi kujitenga na waoamini kwamba uchumi wetu upo stable. Nikimaliza kutoa nyuzi zangu, nadhani tutakubaliana kwenye hili. Uchumi upo weak sana, ukifuatilia hizi hizi takwimu za serikali.
Magufuli amefanikiwa kwenye propaganda tu na ataaibika mno atakapomaliza muda wake.
 
Hivi hamna namna ya kuishitaki hii mifuko inapochelewesha madai ya mwanachama na kuidai fidia
 
Back
Top Bottom