Habarini wakuu, nimefanikiwa kufanya utafiti ambao ulilenga kuchambua taarifa mbali mbali za kiuchumi za serikali na hususani kabisa zilizolenga taarifa ya kifedha ya serikali (Financial statements) kuanzia mwaka wa fedha wa June 2016 mpaka June 2019.
Takwimu nilizotumia kwenye uchambuzi nimezitoa website ya Wizara ya Fedha na Chache sana Banki kuu ya Tanzania.
Nimegundua mengi sana sana, hususani hata sababu ya kutekelezaji tata wa baadhi ya sera, kwa mfano ile ya ‘Mabadiliko yaliyotokea kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii katika kipindi cha ndani ya miaka 2 iliyopita.
Nitawasilisha taarifa moja baada ya nyingine ya uchunguzi wangu katika nyuzi tofauti ili watu waweze ku concentrate, nimegundua hoja nyingi sana ambazo zinahitaji kuhojiwa na wananchi ndo mana nimeanza na muhtasari ‘namba zinanuka – kutokana na mimi binafsi kutokuridhishwa na nilichokiona kwa uelewa wangu wa kiuchumi’
*******
Taarifa za fedha zinaonesha mwonendo usioridhisha kwenye hii mifuko kwa kuangalia kuanzia June 2016 mpaka June 2018 – mifuko imekuwa ikijiaendasha kwa nakisi (makusanyo ya wanachama yamekuwa pungufu ya benefits zote zilizotolewa na mifuko) hii ikiwa ina maanish kukosekana kwa ufanisi wa kujiendesha. Ingekuwa ni biashara binafsi ingekuwa ni 'Loss making business' Expenses zimezidi Revenues.
Hizi figure za nakisi zinazoonekana ni bilioni sio milioni.
Mwaka 2016 - Bilioni 839
Mwaka 2017 - Bilioni 924
Mwaka 2018 - Bilioni 526
Kwa miaka mitatu kuanzia 2016 mpaka 2018, mifuko ya hifadhi ya jamii ilitengeza nakisi jumla ya Shillingi Trilioni 2.29.
Ukiangalia kwa makini kwenye hizi takwimu, unaweza kuona haswa ni nini ilikuwa sababu ya mabadiliko ya hivi karibuni katika mifuko ya hifadhi ya jamii ikiwemo;
- Kuunganisha mifuko,
- Sheria tata kuhusu fao la kujitoa (ambalo kwa miaka ya hivi karibuni limekuwa na utata mkubwa)
Kwamba sababu kubwa ilitokana na kudorora kwa ufanisi mwaka hadi mwaka (June 2016 - June 2018). Ambayo ikachangia kuongeza risk kubwa sana ya survival ya hii mifuko.
Kuna swali la kujiuliza hapa
- Je, kwa kiasi gani serikali kuu inachangia kudumuza hii mifuko?
Again namba zinatuambia kwamba, serikali kuu haiwezi kujitenga na lawama za kudumaza hii mifiko. Serikali imekuwa na malimbikizo makubwa ya madeni kwenye hii mifuko kiasi cha kuendelea kuhatarisha uendeshaji wake.
Madhara ya madeni mlimbikizo ya serikali kwenye hii mifuko, yanasababisha kwa kiasi kikubwa ukata kwenye hii mifuko, kiasi cha kushindwa kutimiza kikamilifu shughuli zao nyingine za uwekezaji.
Haina tofauti na mtu una pesa nyingi lakini umezikopesha kwa watu ambao hawakulipi, ni wazi kwamba kama kuna maendeleo ulipaswa kuyafanya kama kujenga nyumba, ina maana kutakuwa na pesa za kufanya hivo. Utakuwa huna tofauti na TAJIRI AMBAYE NI MASKINI.
Hii ina maana gani?
- Kama serikali, haitachukua hatua za kulipa kwa wakati madeni yake kwenye mifuko ya hifandhi ya jamii, ina maana ya kwamba ufanisi katika mifuko hii utazidi kuendelea kudorora, na hii ikimaanisha pia kudumaa pia kwa huduma za mifuko hii kwa wanachama wao. (Hasara kwa wafanyakazi).
- Kushuka kwa uwezo wa mifuko hii katika kufanya shughuli zao za uwekezaji. Hii inaenda kupelekea kushuka kwa ‘value creation’ ambayo ingepaswa kufanyika na hii mifuko. Ikumbukwe maana halisi ya kuwa hii mifuko ni pia kukuza michango ya wanachama kupitia nyia ya uwekezaji. Lakini sasa, kwa kuwa serikali imekopa hiyo michango na haiirudishi kwa wakati, ina maana mifuko inakosa ukwasi wa kuwekeza.
Nimalizie kusema kwamba, kuna mambo mengi sana yamejificha kwenye namba ukiachana na siasa za kishabiki na kishangiliaji, mambo ambayo yanatugusa watanzania na yanahusiana moja kwa moja na mwenendo wa uchumi wetu.
Nazidi kujitenga na waoamini kwamba uchumi wetu upo stable. Nikimaliza kutoa nyuzi zangu, nadhani tutakubaliana kwenye hili. Uchumi upo weak sana, ukifuatilia hizi hizi takwimu za serikali.